Ninaamini kuwa waliokuwa wakitaka kumsoma Padri Karugendo wanatabasamu. Bado ziko makala zake nyingi za kuweka hapa na habari nyeti kuhusu uhusiano wake na kanisa lisilopenda mabadiliko linaloongozwa na wanaume wasiooa la Katoliki. Soma makala yake mpya iitwayo: PESA ZA KUNUNULIA KURA ZINATOKA WAPI? kwa kubonyeza hapa. Kuna makala zake nyingine katika safu yake iitwayo Kalamu ya Padri Karugendo (iliyoko mkono wa kuume hapa bloguni, shuka chini ya makala zangu na za Freddy Macha utakuta safu hiyo).
February 2005
Mon 28 Feb 2005
Mon 28 Feb 2005
Mon 28 Feb 2005
MAHOJIANO KATI YANGU NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA TANZANIA LABOUR PARTY, AUGUSTINE LYATONGA MREMA:
Ndesanjo: Jina lako nani vile?
Mrema: Agustino Lyatonga Mrema.
Ndesanjo: Agustino? Inaandikwa A-G-U-S-T-I-N-O au inaandikwa A-U-G-U-S-T-I-N-E?
Mrema: Hembu rudia…
Naamua kumwandikia kabisa. Anasoma kisha anasema kuwa jina lake ni Augustine. Nami namwambia mbona haitamkwi Agustino?
Mrema: Tuendelee na masuala ya maana yaliyokuleta hapa ndugu mwandishi.
Ndesanjo: Hili ni moja ya masuala ya maana yaliyonileta hapa. Suala hili linaitwa utumwa wa
akili. Kwanini unakuwa na jina ambalo hata kulitamka huwezi? Unadhani kuwa hili
sio suala la maana?
Mrema: Wewe umetumwa na CCM! Lazima ni shushushu wa CCM.
Ndesanjo: Hapana, nimetumwa na mizimu ya mababu zako. Wanasikitika mno. Wanatoa
machozi kila kukicha na kabla ya kwenda kulala. Wanasema
mambo unayofanya yanasikitisha sana. Kwa mfano, niambie kirefu cha jina la kile
chama ulichohamia baada ya kuondoka CCM (yaani NCCR). Wananiambia kuwa
uliingia chama chenye jina ambalo hata kusema kirefu chake ulikuwa hujui.
** Inaendelea baadaye. Nimekuonjesha utamu kidogo.
Mon 28 Feb 2005
Watawala wa nchi fulani za Afrika ambazo sitaki kuzitaja hasa ile yenye jina linaloanzia na T wasije wakadhani kuwa mambo kama yanayotokea Lebanon hivi sasa yanatokea kwa wengine tu. Usicheze na nguvu ya umma. Hoja yangu kubwa siku za hivi karibuni imekuwa ndio hii: wananchi wana nguvu kubwa kushinda nguvu za dola, nguvu za pesa viongozi walizoiba kwa wananchi…wana nguvu kushinda hata hofu ya kifo. Nguvu yao na kauli yao inashinda kitu chochote kile.
Inachukua muda wananchi kujua nguvu waliyonayo, ila wakishajua hakuna kurudi nyuma. Tazama nguvu ya umma huko Lebanon kwa kubonyeza hapa.
Mon 28 Feb 2005
Nilijaribu kutuma kwa njia ya simu baadhi ya vipande toka kwenye hutba (uliyenipa neno hili unajijua, uko Texas) ya Louis Farrakhan wa Taifa la Waislamu. Vipande vyenyewe ni vifupi kwa sababu mbili: 1. Unapotuma ujumbe kwenye blogu kwa njia ninayotumia huwezi kutuma kwa muda mrefu.
2. Kwakuwa nilikuwa na Ndesanjo mdogo, Ukweli Macha, ambaye ana miaka miwili na nusu, kuna wakati alikuwa akitaka kuishika simu ili acheze nayo. Ilikuwa ikitokea anaitaka simu inabidi nitume na kuizima simu.
Kuna baadhi ya vipande nimeviondoa maana sauti ya Ukweli ilikuwa inasikika zaidi ya Louis Farrakhan, nami leo sikuwa na nia ya kuwasikilizisha Ukweli bali Farrakhan.
Baadaye nitaandika kwa ufupi aliyoyasema. Hata hivyo, sikiliza vipande vichache nilivyoviweka.
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
FARRAKHAN: MUISLAMU NI NDUGU YANGU, ILA MTU MWEUSI NI DAMU YANGU
Na , Maudhui: UncategorizedToa Maoni
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
FARRAKHAN: MTUME ALIYETABIRIWA ANAYEFANANA NA MUSA SIO MUHAMMAD
Na , Maudhui: UncategorizedToa Maoni
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
FARRAKHAN: ITIKADI YA UTENGANO YA TAIFA LA WAISLAMU NI KAMA YA YESU
Na , Maudhui: UncategorizedToa Maoni
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005
Sun 27 Feb 2005




