March 2005
Monthly Archive
Tue 29 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Profesa Amina Wadud wa chuo kikuu cha Virginia Commoweath amegusa hisia za baadhi ya waislamu baada ya kuendesha sala ya kiislamu ndani ya kanisa na bila kutenganisha wanaume na wanawake. Ulinzi katika chuo hicho umeimairishwa kutokana na vitisho kufuatia sala hiyo. Kosa lake kubwa ni 1. kuendesha sala ya kiislamu kanisani 2. kuendesha sala wakati yeye ni mwanamke 3. kutotenganisha wanawake na wanaume. Soma habari zaidi hapa.
Tue 29 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Tovuti hii ni muhimu sana kwa waandishi wa habari, wapiga picha, watengeneza filamu, na wale wanaotafiti maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano na habari. Bonyeza hapa.
Tue 29 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Wanasema hivi ni vita vya kitamaduni kati ya Wafaransa na lugha ya kiingereza inayotawala katika mtandao wa tarakilishi. Soma maamuzi ya rais wa Ufaransa yaliyofanya watu wadai kuwa katangaza vita. Hapa.
Mon 28 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla kumejaa watu wenye vipaji na uwezo wa juu sana katika mambo mbalimbali. Tatizo ni mazingira ya kisiasa, kiuchumi, kielimu, na kijamii. Sera za kuwezesha watu wenye mitaji midogo zimebaki kwenye pambaja za midomo za watawala wa bara la Afrika. Soma habari hii ya walemavu hawa na maajabu yao ya kazi ya kuchomea vyuma. Hapa.
Picha za kazi zao ziko hapa.
Mon 28 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Wale wapenda soka au gozi la ng’ombe, nendeni hapa.
Kuna mechi za moja kwa moja, picha, ratiba, na mengineyo. Nenda hapa usome habari za fujo za washabiki wa soka nchini Mali.
Mon 28 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kwanini haiwezekani?
Wananiambia kuwa haiwezekani. Kwanini?
Eti wananiambia kuwa haiwezekani ukawa hauko CCM na ukawa hauko upande wa upinzani.
Haiwezekani. Lazima uwe na upande. Lazima uwe kushoto au kulia. Ukiikosoa CCM wanakuja juu na kusema, “Wewe unashabikia upinzani.” Ukikosoa upinzani wanakuja juu, “Umetumwa na CCM.” Ukikosoa upinzani na CCM kwa pamoja wabaki mdomo wazi. Wanasema, “Haiwezekani!”
Jambo gani gumu kuelewa? Nawauliza.
Kwani ni kosa kutokuwa upande wowote? Naendelea kuwauliza.
Wananiambia lazima nichague shetani mwenye afadhali. Lazima nitafute mwivi na muongo mwenye afadhali. Lazima nichague shetani mmoja kati ya wawili.
Kwanini kuwe na ulazima huo? Naendelea kuuliza.
Mimi sitaki shetani wa upande wa kuume wala shetani wa upande wa kushoto. Awe ni shetani mwenye afadhali au shetani asiyefaa kabisa. Sitaki muongo au mwivi bora zaidi ya mwingine.
Inawezekana.
Mon 28 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Watakujia juu, “Haiwezekani!”
Haiwezekani. Kivipi. Hawatakubali. Mishipa itawatoka. Maswali watakurushia. Utashangaa, iweje hawaelewi jambo rahisi namna hii?
“Haiwezekani mtu asiwe na dini!” Watakwambia huku wakijiweka tayari kwa ubishi. Ubishi. Wanabisha jambo linalohusu nafsi yako. Wewe unawaambia kuwa nafsini mwako huamini kitu kinachoitwa dini. Na huna dini, sio muislamu wala mkristo (maana dini kwao ni hizi mbili tu).
Wanakataa. Haiwezekani. Kila binadamu ana dini.
“Hawezekani kivipi wakati mimi ni binadamu na sina dini?” Unawauliza.
Wanajibu, “Acha kutuhadaa, kila binadamu ana dini. Ina maana huamini kuwa kuna mungu?”
Wakiuliza swali hili lazima nicheke kwanza. Hapo wanakuwa wamekwenda ninapotaka. Ndipo ukombozi wa akili toka kwenye mtazamo ulioletwa na dini za kuja unapotakiwa kuanza. Watu wengi wanadhani kuwa ukiwa huna dini basi humwamini mungu.
Mahesabu yake:
binadamu+ dini = imani juu ya mungu (yaani mungu yupo)
binadamu- dini = mungu hayupo
Hawajui kuna tofauti kubwa sana kati ya dini na kumwamini mungu. Wakati wengi wetu tunadhani kuwa dini kazi yake ni kutufanya tumjue mungu, kumwamini na kumtii, ukweli ni kuwa dini nyingi zinatuwekea ukuta wa chuma usionekana ambao unatuzuia tusimjue mungu. Ukiwa hutaki kumjua mungu, nitakushauri uwe na dini. Ukiwa unataka kumjua mungu, acha nazo. Najua sentenso hiyo ya mwisho inaweza kukufanya ujiulize kama “zimenitoka” au bado “zipo.”
Dini inakufanya umjue mungu kupitia mawazo na mitazamo ya watu wengine (karibu wote ni wanaume) ambao wanavaa kanzu na majoho wakiongea kwa utaratibu ili uone kuwa wana tofauti sana na wewe na kuwa wana ukaribu na mungu. Werngine hudiriki kutuambia kuwa huongea na mungu. Ila ukiwaambia wakuite saa wanaongea naye ili usikilize au kushiriki, watakwambia kuwa kama huna roho safi huwezi kuongea naye. Lakini ninaposoma busara za Yeshua (Yesu/Isa) nakuta akisema kuwa mungu anatafuta wale waliopotea. Na ndio maana Yeshua alikuwa akishinda vijiweni na wacheza kamari na wachakaramu wengine. Miyahudi ikamjia juu, “He, wewe mbona unajumika na wenye dhambi?” Unajua aliwajibu nini? Kasome kitabu unachoamini kuwa ndio ramani na dira yako hapa dunini ingawa kinakusanya vumbi. Kila siku unahangaika na magazeti ya ushambenga lakini kitabu unachodai kimeandikwa na mungu mwenyewe hukisomi…turudi kwenye hoja ya msingi.
Kwahiyo unachojua kuhusu dini ni mawazo ya viongozi wa dini yako. Mawazo yao hayo ndio yanakuwa dira yako wewe ambaye una akili na uwezo wa kujitafutia ukweli mwenyewe. Dini inakufanya uwe mvivu. Hutasoma biblia au kurani kwasababu kuna viongozi wa dini yako ambao kazi yao ni kusoma vitabu hivyo na kukutafsiria mara moja kwa juma. Au wakati mwingine mara moja kwa mwaka…kama wewe ni wale wanaoenda kanisani misa ya usiku au siku ya krisimasi.
Dini inakufanya udhani kuwa kuna mashindano kati yako wewe mkristo wa kilutheri na mkristo wa kiangikana, au shahidi wa yehova dhidi ya mkatoliki, au mashindano kati ya muislamu wa sunni na yule wa shia, au mashindano kati ya muislamu na mkristo…mashindano ya kwenda mbinguni. Dini inakufanya uamini kuwa watu wote wasio na imani kama yako watakwenda unakoita motoni. Wewe na wenzako ndio mnajua hiyo njia nyembamba iliyozungukwa na malaika weupe (ndio malaika weupe, hakuna mweusi) wenye mavazi meupe ya kuelekea kwenye uzima wa milele. Pengine ndio maana tunajichubua ili tufanane na hao malaika.
Kuna watu ambao huniambia kuwa dini huleta amani. Jamani, hivi Rwanda watu hawana dini? Je Sudan? Je Kashmir? Je Iraki? Serikali ya Marekani inayopenda vita kama sijui nini inaongozwa na watu wasio na dini? Tuache nchi hizo, twende kule zilikozaliwa dini zinazoitwa “kuu” duniani: uislamu, ukristo, na uyahudi. Twende kule walikotokea manabii wa dini hizi. Kule walikotembea na kufundisha. Twende kule mnakotumia mamilioni kwenda kuhiji. Twenda Mashariki ya Kati. Twende Palestina. Twende Yerusalemu. Huko kila mtu ana dini. Kama sio mkristo, basi ni muislamu, kama sio muislamu basi ni myahudi.
Dini moja inafundisha amani (uislamu), nyingine upendo (ukristo) na nyingine kushika amri kumi. Twende huko tutazame jinsi ambavyo dini inaleta amani!
Nyooshea kidole nchi yenye amani kutokana na watu wake kuwa na dini. Tazama Indonesia, nchi inayoongoza kwa idadi kubwa ya waislamu, je inaoongoza pia kwa amani? Tazama Ufilipino, karibu kila mtu ni mkatoliki, je wanaongoza kwa upendo aliohubiri Yesu? Hivi Kongo hawana dini? Kama dini inaleta amani, nchi zenye watu wachache wenye dini zingekuwa zinaongoza kwa vita. Lakini ajabu ni kuwa nchi zenye watu wachache wanaojihusisha na mambo ya dini zinaonekana kuwa na amani zaidi ya nchi ambazo karibu wananchi wake wote wana dini. Au tuseme wanajifanya wana hiki kitu kiitwacho dini.
Kwahiyo watu wengi wanaamini kuwa kama binadamu wasingekuwa na dini, wangekuwa watu wabaya na waovu sana. Mimi hujiuliza, binadamu anaweza kuwa mwovu zaidi ya alivyo sasa? Kuna uovu gani uliobakia? Au mnadhani yanayotokea Palestina, Iraki, Sudani, Kongo, yaliyotokea Rwanda, Cambodia, Vietnam, Aghanistan, Ujerumani ya Hitler ni hadithi? Maovu makubwa kabisa kwenye historia tunayoijua yametokea katika kipindi ambacho wanadamu wana hiki kitu mnaiita dini.
Biashara ya utumwa ya Atlantiki miaka zaidi ya 400. Ile ya waarabu ilichukua miaka mingi zaidi maana ilianza kabla hii ya Atlantiki. Mauaji ya wayahudi na Hitler. Bomu la atomiki huko Japani. Ubaguzi wa rangi Marekani na Afrika Kusini. Vita vya Wazungu vya Kwanza na vya Pili (wengine mnaviita vita vya dunia…wazungu (na baadhi ya waasia) vita vyao wanataka kubebesha lawama dunia nzima kwa kuiita vita vya dunia. Nanyi mnakubali. Yaani hawataki tugawane mali waliyotuibia bali tugawane historia ya damu.) Mauaji ya halaiki Rwanda. Ukoloni. Yote haya yamefanyika katika kipindi ambacho wanadamu wengi wanasema kuwa wana dini.
Hivi wezi wanaoiba sirikalini na wengine kuuza nchi hawana dini? Wananchi wenye hasira kali wanaoua binadamu wenzao bila huruma kwa kuwa wamedaiwa kuwa wezi, hawana dini? Wala rushwa na wana magendo, hawana dini?
Najua moja ya hoja inayotolewa ninaposema mambo haya ni hii, “Vita na maovu hayo hayajaletwa na dini.” Nakubaliana kwa kiasi fulani. Nasema kwa kiasi fulani kwakuwa historia iko wazi juu ya maovu yaliyoletwa na dini. Ila hata kama maovu hayo hayakuletwa na dini, tunaweza kujiuliza: kama dini inaleta amani iweje mambo hayo yote yanayoharibu amani yatokee?
Tukichimba zaidi hoja hii tunaweza kwenda kwenye hoja nyingine ambayo sitaiingilia kwa undani. Hoja hiyo ni kuwa huenda watu “wenye dini” ukweli ni kuwa “hawana dini.”
Kwa upande mwingine unapochunguza sana kitu tunachoita dini unagundua kuwa dini ni pazia. Linakuzuia usimjue mungu wako wala manabii zako. Hapa ninazungumzia Waafrika.
Hivi wewe na akili zako zote unadhani Afrika nzima haijawahi kuwa na manabii?
Kwanini sina dini? Kama wewe ni mwafrika, huhitaji dini. Uafrika ni utamaduni. Utamaduni huu unatupa mwongozo kwa kila jambo, yakiwemo masuala ya kiroho. Wewe unaweza kuyaita dini. Kwahiyo uafrika una misingi na falsafa yake kuhusu mungu unayedhani kuwa simwamini kwakuwa nasema kuwa sina dini. Falsafa na miongozo kuhusu mungu iliyoko katika utamaduni wa Mwafrika, kwa mtazamo wangu, vinatosheleza. Hakuna kitu kipya ambacho uislamu, ukristo au uyahudi unaweza kunifundisha. Kwanza amri kumi ambazo ni msingi wa dini hizi zinazoonekana kuwa ni “bora” zaidi ya nyingine zilikuwa Afrika miaka mingi kabla Musa, aliyesema kuwa kapewa mlimani na yehova, hajazaliwa. Ngoja nirudie ili usidhani nimekosea: NINASEMA KUWA AMRI KUMI “ZA MUSA” ZILIKUWEPO AFRIKA KABLA MUSA HAJAZALIWA! Ni kati ya amri 147 zilizokuwa zikitawala maisha ya Waafrika katika bonde la mto Nile (Misri ya zamani, Nubia, Ethiopia, n.k.).
Soma historia. Sio ile unayodanganywa shuleni na walimu waliodanganywa shuleni kama wewe na vyuo vya ualimu. Tafuta historia yeu.
Wakati dini yako inakupa amri isemayo, “Mpende jirani yako kama nafsi yako,” utamaduni wa Afrika unakupa falsafa hii: Mtu sio mtu bila watu (Kwa Ki-Xhosa, “Umtu Ngumtu Ngabantu). Kwa maneno mengine tunaambiwa tupendane. Falasafa hiyo ndio inakupa ujamaa, harambee, n.k. Marasta wao wanakuja na dhana kama hiyo wanaposema, “I and I.”
Unadhani kanuni ya mtu sio mtu bila watu imetoka kwa shetani?
Mon 28 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Nimeweka makala mpya iitwayo: Mapinduzi bila damu wala wafadhili. Bonyeza hapa uisome. Makala nyingine ziko upande wa kuume katika kona ya makala zangu.
Mon 28 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kuna habari katika inayosikitisha sana kuhusu walimu na elimu nchini Tanzania. Mengi yaliyosemwa katika habari hii sio mapya. Ninafahamiana na walimu wengi, marafiki na ndugu. Ninajua mtazamo wa sirikali ya Tanzania katika masuala ya elimu kwa wote. Kama tunataka nchi yetu iondoke katika orodha ya nchi fukara zisizo na mbele wala nyuma duniani lazima turekebishe mfumo wa elimu na kuwapa walimu heshima zaidi na kuwapa ujira halali kwa kazi kubwa wanayofanya. Soma habari yenyewe hapa.
Unaweza pia kutembelea tovuti ya shirika lisilo la kisirikali, HakiElimu,
linalojihusisha na masuala ya sera na mfumo wa elimu Tanzania. Hapa. Taarifa nilizonazo ni kuwa kazi ya shirika hili inahitaji pongezi. Nawapa pongezi zangu. Lakini sitaacha kuzungumzia suala hili: utaona kuwa tovuti yao ina tatizo lile ninalozungumzia kila kukicha. Wakati dhumuni kubwa la Hakielimu ni kuhimiza ushirikishwaji wa umma katika uendeshaji wa sekta ya elimu, tovuti yao ni ya kiingereza. Lugha inayotumiwa kila siku na huo “umma” katika mabasi, baa, makanisani na misikitini, majumbani, ndotoni, mikutano ya hadhara ya kisiasa, vijiweni, n.k. ni Kiswahili. Sijui kuna ugumu gani wa wanaharakati wetu kuelewa jambo hili rahisi namna hii: Watanzania wanaelewa Kiswahili zaidi ya kiingereza. Kwisha! Sisemi kuwa kiingereza ni lugha isiyofaa, hata kidogo. Hii ni lugha tunaweza kutumia tunapokuwa na maingiliano na wengine wasiojua Kiswahili. Ila tunapokuwa tunaongea sisi kwa sisi, kuna ugumu gani wa kutumia Kiswahili? Kuna hoja kuwa lugha ya kiingereza inatumiwa katika tovuti nyingi Tanzania (kama ya bunge, ikulu, ofisi ya waziri mkuu, KKKT, n.k.) maana watu wanaotumia teknolojia ya mtandao wa tarakilishi (intaneti) wengi ni wasomi wanaojua kiingereza. Hii ni sawa na kusema kuwa kwakuwa Wafaransa wengi wanaotumia mtandao wa tarakilishi wanajua kiingereza, kwahiyo tovuti ya serikali na bunge la Ufaransa na kila kitu nchini humo viwe kwa lugha ya kiingereza! Hoja hii (ya kuwa Watanzania wanaotumia mtandao huu wanajua kiingereza ndio maana tovuti ni za kiingereza) tuiweke kiporo kwa sasa, nitaikabili kichwa kichwa hivi karibuni.
Sat 26 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kuna makala mpya nzuri sana ya Padri Karugendo iitwayo: Dakta Salim, Sema Ukweli. Makala nyingine za Karugendo zinapatikana kwenye kona yake hapa bloguni iitwayo Kalamu Ya Padri Karugendo. Kongoli hapa usome makala yake hiyo mpya.
Fri 25 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Rafiki yangu Da’ (unajijua) umenitajia Jhiko Manyika. Nimemsikiliza sana leo. Kuna nyimbo zake mbili nadhani lazima azirekodi tena. Hasa wimbo wa Uongo huo. Leo nimeusikiliza vizuri sana. Nitawapigieni hapa siku moja. Ngoja niwapeni maneno ya wimbo huo. Kabla sijawapa, kwa wasiomjua, Jhiko Manyika ni mwanamuziki wa Rege nchini Tanzania. Tazama picha yake hapa.UONGO HUOUongo huo, uongo huo, uongo huo,Tusisumbukie uongoTuijue kweli na hiyo kweliItatuweka huruWale Waafrika tusio makini Tumedanganyika,Wakati ndugu zetu wanadai utu wetuSisi tunalalamika,Wale Waafrika tusio makiniTumedanganyika,Wakati ndugu zetu wanadai utu wetuSisi tunakasirikaTamaduni zetu Tunasema ni za kishenzi,Wazee wa kuwapa heshimaTunasema ni wachawi wanatuuaUongo huo, uongo huo, uongo huo,
Tusisumbukie uongo
Tuijue kweli na hiyo kweli
Itatuweka huruWale Waafrika tusio makini
Tumedanganyika,
Wakati ndugu zetu wanadai utu wetu
Sisi tunalalama,
Wale Waafrika tusio makini
Tumedanganyika,
Wakati ndugu zetu wanadai utu wetu
Sisi tunalalamikaTunathamini vituTunasahau utuUongo huo, uongo huo…
Thu 24 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kwa sasa siwezi kujua kama haya ni mapinduzi ya umma kwa faida ya umma au ni mchezo wa kuondoa wezi hawa na kuingiza wezi wale. Imetokea leo hii huko Kyrgyzstani. Historia ya mapinduzi kama haya ni ndefu. Kwa miaka ya karibuni tuna mifano michache. Yalitokea kule Jojia. Kongoli hapa.
Kisha tukasikia Ukraine nako. Hapa.
Halafu ikaja zamu ya Lebanoni. Hapa.
Na sasa imetokea Kyrgyzstani. Hapa.
Baadaye itakuwa wapi? Swali ninalojiuliza ni hili: mapinduzi haya ni kwa faida ya nani? Kitendo cha Marekani kushabikia mapinduzi ya Ukraine na kule Lebanoni kinafanya watu wengi wasite kufurahia kuwa umma umetwaa madaraka toka mikononi mwa wezi wachache. Tuna macho, tuna akili, tusubiri. Jambo la kushukuru katika yote haya ni kuwa hakuna watu walionyanyua silaha na kuingia msituni.
Wed 23 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Rafiki yangu mmoja kanikumbusha jina langu jipya nililopewa na Mloyi katika maandalizi ya kurudisha tawala za kikoloni barani Afrika. Jina hilo ni: Nesto McChair. Unaona karibu linafanana na Ndesanjo Macha. Kuna ukaribu fulani.
Maandalizi ya kurudisha tawala za kikoloni yanaendelea vizuri. Tenda ya ujenzi wa kiwanda cha dawa za kujichubua imeshatangazwa na sirikali ya Tanzania. Tayari tumeshapata washauri kuhusu kujichubua toka (zamani iliitwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) Jamhuri ya Kidemokrasia Iliyo Katika Vita Vya Wenyewe kwa Wenyewe ya Kongo. Pia sirikali imeamua kuwa itamchagua mwanamuziki Maiko Jakisoni kuwa waziri wa nchi wa masuala ya kuondoa nuksi ya rangi nyeusi. Kumbuka shetani rangi yake ni nyeusi, na kamwe binadamu mwenye akili zake hawezi kukubali kuwa na rangi moja na shetani.
Halafu ule mradi wa kuandika biblia upya ili kuweka habari za mashirika yanayofanya kazi inayoendana na ule mfano wa Yesu wa Msamaria Mwema, yaani Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani unaendelea vizuri. Pia ili majina ya nabii Musa wa zama hizi, Tony Blair, anayetaka kuwakomboa wana wa Israeli huko Zimbabwe toka katika mikono ya Farao Mugabe yaingia kwenye kitabu hiki kitakatifu. Pia jina la Joji Kichaka ambaye ni Musa wa karne hii anayewasaidia Wairaki kuelekea kwenye zama za asali. Mradi huu unaenda polepole kutokana na ukweli kuwa aya zinashushwa taratibu sana. Sijui ni tatizo la mitambo ya mawasiliano au ni nini.
Kabla sijasahau, ile barabara mliyoiita Barabara ya Nyerere tuko mbioni kuibadili jina. Lazima Nyerere tumwondoe kwenye historia yetu kwa jinsi “alivyotulostisha.” Kimbelembele chake cha kugombea uhuru kimetuletea umasikini mtupu. Napandwa na hasira. Siwezi kuendelea kuandika. Ngoja nilie kwanza halafu nitafute picha yake niliyonayo niichanechane. Na nikisikia mtu anasema, “Ujamaa ni kujitegemea ndio njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru” huyo mtu ajue tutakosana. Zitakunjwa. Ama zangu, ama zake. Ngoja nikanywe maji nipunguze ghadhabu niliyonayo dhidi ya Maumau, Nkrumah, Neto, Toure, n.k. kwa kimbelembele chao cha kudai uhuru.
Tazama Mwalimu Nyerere alivyotufanya tukawa tunakimbia mchakamchaka huku tukiimba Kaburu matata iya! Tulikuwa na nyimbo kibao za kuwasakama na kuwabeza makaburu. Sasa hivi majuzi tumekuja kujua kuwa kumbe ni watu wazuri sana. Tena wacha mungu. Halafu hawana kinyongo na sisi hata kidogo. Nadhani wanafuata mafundisho ya biblia yasemayo, “Samehe hata mara saba u sabini.” Wamatusamehe na kuamua kuja nchini kwetu kutusaidia kuchimba madini ya Tanzanite kwa faida yetu!
Tue 22 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Wanasema hatuwezi kupiga hatua kuthaminiwa wala kutambuliwa,
Eti sababu sisi ni watu weusi Eeeh!
Ulimwenguni tumepewa laana,
Usiseme hivyo hebu acha kukufuru,
Kwani aliyetuumba hapendezwi hivyo.
Bob Marley naye Peter Tosh, niambie mizimu yao ilitoka wapi?
Mwalimu Nyerere, Nelson Mandela, niambie mizimu yao ilitokea wapi?
Kwame Nkrumah na Haile Selasie, niambie mizimu yao ilitoka wapi?
Martin Luther King na Marcus Garvey, niambie mizimu yao ilitokea wapi?
Kaza moyo ndugu Eeeh bado safari ni ndefu…
- Marehemu Justin Kalikawa katika wimbo wa Mizimu.
Tue 22 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Tunawajengea magereza,
Tunajenga shule zenu,
Mnatupa elimu ya kutupumbaza,
Mnatutuza chuki kwa upendo wetu
Mkitusimulia juu ya mungu wenu aliye mbinguni…
- Bob Marley katika wimbo wa Crazy BaldHead
Tue 22 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Mwanaharakati wa haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari anayetumia mtandao wa kompyuta (cyber-dissident) wa nchini Tunisia, Zouhair Yahyaoui (36), amefariki dunia hivi karibuni. Aliaga dunia tarehe 13 mwezi huu kwa ugonjwa wa moyo. Yahyaoui atakumbukwa kwa mchango wake katika kupigania haki na uhuru wa habari nchini Tunisia. Yeye ndiye mwanzilishi wa webu ya tunezine.com.
Yahyaoui alikuwa ndiye mtu wa kwanza kushinda tuzo mpya ya Cyber-Freedom mwaka juzi. Tuzo hii hutolewa na shirika la Waandishi Wasio na Mipaka (Reporters sans frontières ). Ukibonyeza hapa utaona webu mbalimbali zenye habari zaidi juu ya wanaharakati wanaotumia teknolojia ya kompyuta na nguvu za dola zinazotumiwa dhidi yao.
Tue 22 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Mwanafunzi wa Mlimani, Edumedus Nyonyi kamwandikia Padri Karugendo waraka wenye kichwa hiki: Ujumbe Toka Makaburini. Karugendo kasoma ujumbe huo na kutumia marafiki zake. Nami nimeusoma na kuamua kuuweka ndani ya blogu nanyi muusome.
Mpendwa Padri shikamoo.
Mwezi januari nilibahatika kutembelea eneo la mazimbu Morogoro yalipo makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini. Hakika baada ya kutoka huko naona sina raha maishani mwangu. Hata hivyo nimeonelea nikushirikishe sauti hii niliyoisikia hata kama huenda ulishawahi kufika na kushuhudia mwenyewe nakuhakikishia mwangwi wake umebadilika.
Baada ya kufika makaburini ambayo yanatunzwa vema kuliko ya ndugu zetu wanaozikwa Kinondoni au Mburahati, niliona kibao chenye ujumbe ambao umeweka alama katika maisha yangu. Maneno haya yalisomeka hivi”Ours was not for grory nor personal distinction but it was due for the noble cause of our time and the liberation of humanity of the entire community of South Afrika.”
Wakati bado nimepigwa ganzi na ujumbe huo huku nisijue la kufanya, wenzangu niliokuwa nao yapata kama ishirini hiv,i wao walikuwa wanashughulika na kupiga picha za ukumbusho. Nilidhani labda mimi ni mjinga kushughulika na kisicho na maana badala ya kuweka kumbukumbu ili nije nikawaonyeshe watu kwamba nani nilishawahi kutembea.
Hata hivyo nilihitimisha kuwa mtu mwenye akili hawezi kushughulika na mambo mengine na kuacha ujumbe wa kutisha, wa kijasiri wa kizalendo, wa kujitoa mhanga kama huo. Basi nilijua ndio elimu yetu ya siku hizi maana imekaa kiutandawazi.
Kumbe vifo vyao havikuwa ili waandikwe kwenye majina ya vitabu vya historia waka kutungwa kwenye nyimbo huku wakisifiwa kila mara! Kumbe kufungwa kwa mandela hakukuwa kukuza jina la ukoo. Bila shaka walijua wazi kuwa wanacho kipigania wanaweza wasikifaidi lakini kwa utu wao na vizazi vijavyo walilala mistuni kama wanyama.
Swali lilinijia kuwa Je ukombozi wa utu wa mwanadamu sasa umekwisha.Uliondoka na kuisha kwa ubaguzi?. La hasha bado tu watumwa wa wageni na hata ndugu zetu. Ndipo nikaenda mbali kuwa watu wanalala darasani ili wapate madgrii wawe maprofesa kwa ajili ya kukomboa wenzao au kukuza jina tu. Na rais na wabunge wanataka nafasi hiyo kama ujumbe wa makaburi ulivyo au ni “for grory and personal distinction”.
Niliwahi kukuandikia kuwa nataka kuingia kwenye siasa. Na sababu ni hicho kilio cha makaburi. Nataka nione kama walau elimu yangu naweza kuitumia kuukomboa utu wa mwanadamu tena bila kujulikana kama ikibidi. Nilipanga mwaka huu kugombea udiwani Kanyigo au hata popote ambapo wangelinikaribisha. Niliwaandikia ndugu zangu waanze maandalizi wakadhani nimechanganyikiwa. Hivyo kwa mwaka huu na shughuliza kumalizia masomo naona nitakwama. Wasalaam Nyonyi.
Tue 22 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Nimeweka makala mpya ya Padri Privatus Karugendo. Makala hii iliandikwa baada ya kufariki kwa mwanamuziki wa Rege, Justin Kalikawe. Alifariki Agosti 12, 2003. Ingawa makala ni ya muda mrefu, ujumbe wake una uhai hadi leo. Nakumbuka mara ya kwanza kumsikiliza Kalikawe, ilikuwa ni 1991/92 nikiwa Ilboru. Nadhani Tunga ndiye alikuwa na kanda moja yenye nyimbo zake ambazo sijui kama alikuja kuzirekodi rasmi. Nilijua kuwa nyota mpya ya Rege Tanzania inachomoza. Wimbo wake wa Mizimu ambao Padri Karugendo kauzungumzia unaweza ni wimbo wake ninaoupenda kuliko zote. Wimbo wake wa Machinga nakumbuka ulipigwa sana katika mitaa ya jiji la Dasalama. Na wimbo wa MV Bukoba ulitukumbusha msiba mkubwa wa taifa uliotokea kwenye lile ziwa lenye jina la Malikia wa Uingereza, Vikitoria (au Vikii kwa kifupi). Bonyeza hapa usome makala hiyo ya Kalikawe. Bonyeza hapa usikilize baadhi ya nyimbo zake. Ukifika kwenye webu ya Mzibo, bonyeza juu ya picha ya Kalikawe. Kumbuka makala nyingine za Karugendo ziko kwenye safu yake hapa bloguni iitwayo Kalamu ya Karugendo.
Mon 21 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Wamisionari walipofika Afrika walitakiwa kwanza wakae chini waelimishwe. Hakutuelewa hata kidogo. Tatizo lao kubwa lilikuwa ni wanatumia tamaduni zao kama kipimo cha ukweli, ustaarabu, na ubinadamu. Kutokana na kutumia tamaduni zao karibu kila jambo toka katika tamaduni zetu lilionekana kuwa ni la kishenzi. Wakatuita wapagani. Wakasema mungu wa kweli hatumjui wao ndio wanamjua. Wakatuambia tumfuate huyo mungu wanayemwabudu wao. Laiti wangejishusha na kuamua kujifunza tamaduni zetu, falsafa, na mantiki zake, toka kwetu.
Kwa mfano walidhani kuwa Waafrika wote wanaabudu miungu wengi. Waliposikia tunasema kuwa kuna mungu wa uzazi, mungu wa mvua, mungu wa mazao, mungu wa maji, mungu wa jua, n.k. wakadhani tuna miungu kibao, pengine isiyohesabika. Kumbe Waafrika wengi tunaposema mungu wa hiki na mungu wa kile tunamzungumzia mungu mmoja. Mungu ni mmoja ila sifa na kazi zake ni nyingi. Tunaamini kuwa nguvu tunayoiita mungu ni vigumu sana kuielewa kwa fikra za kibinadamu. Hatuwezi kabisa kuielewa nguvu hii kwa kufikiria tu na kuunda taswira fulani kichwani huku nguvu yenyewe hatujaiona kwa macho. Kutokana na ugumu huu, Mwafrika anajaribu kumwelewa mungu kupitia kazi zake mbalimbali kama vile uumbaji (hapo ndio unakutana na mungu wa maji, uzazi, mazao, mito, n.k.) Tuliamini kuwa yeye ndiye anatupa maji. Kutokana na kazi yake hiyo tunamwita mungu wa maji. Yeye ndiye katupa mbegu, hapo tukamwita mungu wa mazao. Lakini ni mungu huyo huyo mmoja. Kwahiyo mungu kwetu ni muumbaji na kazi zake za uumbaji tunaziona na hapo ndipo tunamwona yeye. Kwahiyo Waafrika tunamjua mungu kupitia kazi zake mbalimbali, lakini mungu huyo ni mmoja.
Wamisionari waliposikia kuwa tuna mungu wa maji, na uzazi, na mavuno walituambia tuachane na imani hizo maana kuamini mungu zaidi ya mmoja ni kinyume na amri yake. Wakadai kuwa huko ni kuvunja amri ya kwanza. Ajabu ni kuwa baada ya kutuambia tuachane na mungu wa maji, mungu wa uzazi, na mungu wa mazao walitupa mungu baba, mungu mwana, mungu roho mtakatifu wakatuambia kuwa huyo ni mmoja. Kama falsafa yetu ya mungu wa uzazi, mungu wa maji, na mungu wa mazao, haimaanishi mungu mmoja, iweje mungu baba, mungu mwana, mungu roho mtakatifu awe ni mungu mmoja? Halafu tulipofungua kitabu cha Mwanzo katika biblia tukakuta inasema: “Na tuumbe mtu kwa mfano wetu.” Inakuwaje mungu mmoja anasema “… kwa mfano wetu?” Wetu wangapi? Mmoja? Waulize swali hili wafuasi wao. Ninajua watakavyokujibu,
Ukiwavalia njuga suala la mungu baba, mungu mwana, na mungu roho mtakatifu kuwa mmoja (lakini mungu wa uzazi, mazao, na maji sio mungu mmoja) watakuambia kuwa hiyo ni siri. Ni fumbo. Wanaita fumbo la utatu. Kwa ufupi, wamisionari walikuwa na uelewa finyu sana na dharau. Kazi tulionayo sasa ni kuelimisha wale walioamua kufuata falsafa, na teolojia zao.
Mon 21 Mar 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Binadamu tusipofanya kazi kwa kujiwagia au kugawana kazi kama siafu au mchwa, tunaweza kujikuta wote tunafanya kazi moja. Kwahiyo katika nchi wote tukiwa waimba mapambio na nyimbo za chipukizi za kusifu watawala mapambia na nyimbo hizo vitakuwa ni kelele. Jamani, wote msijiunge na kwaya au chipukizi. Wengine mkikimbia mchakamchaka msiibe. Tukiimba wote hatutasikilizana. Wengine waimbe, wangine wasikilize, wengine waongee, wengine waandike, wengine wapime, wengine wakosoe, wengine wapinge, wengine watazama tu…
Kwa mfano, kuna wanaosifia jinsi Tanzania “inavyokwenda mbele.” Soma gazeti la uhuru na sikiliza hotuba za viongozi kama unataka kusikia jinsi Tanzania inaelekea kukamilisha Dira ya Kitaifa Ya Maendeleo ya 2020. Waombe watu wanaowandikia hotuba zao wawe wanakutumia nakala za hotuba zao. Kwahiyo viongozi hawa na gazeti kama Uhuru wanafanya kazi nzuri ya kusifu. Sasa kuna wengine kazi yao sio kusifu bali kuzungumzia ile asilimia nyingine ambayo watawala na wanasiasa huwa hawasemi. Kawaida wanatuambia mambo yanayowahakikishia nafasi walizonazo. Ile asilimia wasiyotaka ujue, pale wanapotaka uamini kabisa kuwa nchi yako inakwenda mbele kwa kasi, inatolewa na wengine. Hawa wanaifurahia sana kazi hiyo na inapokuwa mshale wa moto kuwaingia wale wanaoamini wimbo wa “Tanzania inapiga hatua za maendeleo” ndio wanafurahi zaidi maana ndio moja ya kazi zao. Watu hawa lazima tuwachome kwa mshale wa moto. Pambio la Tanzania kuendelea limewaingia katika nafasi zao kiasi ambacho wakisikia mtu anasema kuwa Watanzania wana haki ya kuwa daraja la juu zaidi ya walipo wanaona kama vile wametukanwa. Inakuwa ni kinyume na imani waliyojengewa. Mbaya zaidi ni pale mtu huyo huyo anakuwa anapata mishale unapoongelea sio siasa tu bali dini. Anapata tabu sana. Anapata ghadhabu. Hajui afanye nini. Anaandamwa hadi kwenye imani ya nafsini mwake. Inavunjwavunjwa. Teolojia yake inahojiwa. Inarushwa huku na kule. Kitabu chake anakuta kumbe wala hakijui sawasawa. Anashtuka pia kujua kuwa hatuogopi kuwasema viongozi wake wa dini kuwa ni waongo. Au wanakandamiza wanawake. Kama ni mkatoliki unamuuliza, “Kuna kosa gani mwanamke akiwa Padri?” Mtazame atakavyojilambala mdomo. Kama ni muislamu mwambie, “Kurani inasema mwanamke akikosea una mambo matatu ya kufanya: 1.kataa kulala naye kitanda kimoja 2. muonye 3. mpige.” Hiyo namba tatu ndio ninaipenda sana. Muulize, “Je mwanaume akikosea kwenye uislamu anafanywe nini?”
Nimeamua kuwa nitaanza kutafuta kipaji cha kusifia. Ingawa kipaji hiki sikipendi sana, nitakitafuta ili niridhishe kila upande.
— Next Page »