NEWS: Discount viagra europe Discount phentermine prescription Discount viagra perscription drug Order phentermine on line? 92 accepted cod phentermine Compare viagra prices, Pharmacy online phentermine Purchase tramadol online. Phentermine sites that ship cash on delivery Viagra retail discount Home made viagra Valium vs xanax Xanax no prescription Viagra sales online Erection viagra Free viagra without prescription Phentermine fda Xanax withdrawl Effects phentermine side strong Information viagra woman What does phentermine do to your heart Long term phentermine use Viagra testimony Phentermine very cheap Buying phentermine Cialis pill? Discount online phentermine Buy cheap phentermine yellow Tramadol hcl tab Phentermine hydrochloride ship to missouri: Buy viagra prescription online Compare phentermine prices Cialis compare levitra viagra Picture of generic xanax Tramadol uses Recreational viagra use Generic india viagra Cheap viagra generic Cialis drug Natural phentermine Phentermine cheapest price 5 no perscription! Cialis and pomegranate interaction Viagra for woman? Ionamin phentermine Cheapest xanax online! Xanax drug interactions Buy cod phentermine Phentermine online Methadone and xanax Recreational viagra Viagra online sales Mexican phentermine Cod tramadol! Phentermine mexican pharmacies online Phentermine pictures Cheap phentermine without a prescription Compare viagra cialis levitra. Xanax master card Long term effects of xanax, Viagra cialis levitra comparison dosages Does viagra woman work 5 in round white tablets no imprint code 50 mg viagra Phentermine shipped cod Phentermine for less Viagra information Phentermine free consultation? Viagra kaufen Is tramadol a narcotic Cheap quality viagra Phentermine and topiramate for weightloss Diet loss phentermine pill weight Diet phentermine pill sale Kevin harvick viagra Xanax withdrawls Purchase viagra online Cialis new viagra. Viagra for woman information Online ordering viagra Viagra prescription uk Buying phentermine: Can i take xanax with zocor and procardia Phentermine overnight Does viagra work Low natural resources for the drug phentermine Viagra treatment migraine headache Buy in online uk viagra, Apcalis cialis 180 phentermine Black market costa rica pharmacy phentermine no imprint code Buying tramadol online Loss phentermine story success weight How much weight will you lose on phentermine Online xanax prescription Cialis compared to viagra Paxil with phentermine interactions Xanax addiction treatment. 0 buy by popl powered viagra wordpress Cheap tramadol 180 Viagra in woman Lethal doses of klonopin and xanax Stopping xanax Cialis overnight! Phentermine and urine drug screen Smoking xanax: Ingredient phentermine Saturday delivery phentermine Viagra prescription medication Free cialis 25 mg Viagra uses Xanax detoxification Viagra pictures Pfizer viagra online Online adipex phentermine prescriptions. Side effects of tramadol hydrochloride On line prescription viagra 100 phentermine Female spray viagra Tramadol hc Free viagra sample I need to find cheap phentermine delivered to fl Online pharmacy phentermine xenical meridia Compare phentermine prices Canada cialis generic? Xanax shipped cod No perscription xanax cheap Acquisto cialis Generic india viagra Buy cheap purchase uk viagra Viagra price Online phentermine pharmacy best cheapest Tramadol 50mg. Buy viagra online get prescription Addiction recovery xanax, Price for generic viagra Diet inexpensive phentermine pill Generic viagra canada No prescription phentermine Phentermine withdrawal symptoms Cheap viagra order online Cheapest viagra price Phentermine online doctor prescribed? Buy cialis uk Fast delivery phentermine, Keyword prescription qoclick tramadol without Tramadol dog Phentermine wholesale Snorting phentermine Discount phentermine online Tramadol online Cheap tramadol no prescription Cialis comparison levivia viagra Cheapest viagra online 92 accepted cod phentermine Cheap phentermine with online consultation Viagra alternatives uk Buy prescription tramadol without Buying viagra in the uk Xanax description Oxycontin xanax bars perclesept and lortab wha Generic viagra cialis Generic lowest price viagra Phentermine at cost with no prescription Picture of xanax pill Phentermine shortage Phentermine cheap free shipping Phentermine yellow 30 mg Addiction tramadol Tramadol hydrochloride tablet Phentermine cod delivery Online phentermine order Cyber pharmacy viagra Dangers of phentermine heart Buy cheap tramadol Xanax alcohol Cialis generic Tramadol prescription Free phentermine prescriptions 50 mg viagra Phentermine studies Viagra and levivia Phentermine feedback How long between phentermine and meridia Low cost phentermine Phentermine and topiramate for weightloss Tramadol hc Viagra overnight delivery Phentermine success stories Viagra cheap prescription Tramadol hydrochloride capsules Free shipping phentermine Diet pill addiction phentermine? Generic cialis soft tabs Side effects of xanax xr: Phentermine quick Buy xanax on line How long does xanax stay in the system Importing cialis from canada to us Buy cheap domain onlineatspacecom xanax Phentermine and diet pill

May 2005


Kwanza kabisa nenda hapa kwa undani kuhusu mradi wa Creative Commons. Kisha jua kuwa unaweza kutafuta kazi zinazotolewa kwa modeli ya Creative Commons ndani ya Yahoo! Hapa.
Creative Commons, tofauti na sheria za kibepari zilizopo za hatimiliki, inawapa uwezo zaidi wananchi, watunzi, wasanii, waandishi, wanamuziki, n.k., kuamua kazi zao zitumike vipi na umma. Sheria za hatimiliki zilizopo zimejengwa juu ya mantiki ya kibepari na kibinafsi ya “Haki zote zimehifadhiwa.” Lakini Creative Commons inakuja na mantiki ya kijamaa na kibuntu isemayo “Baadhi ya haki zimehifadhiwa,” au “Hakuna haki zilizohifadhiwa.”
Huu ndio ulikuwa msingi wa mkutano wa Commons-sense. Na haya ndio mapinduzi yanayokuja kutokana na teknolojia mpya za habari na mawasiliano.

Paula LeDieu, aliyewahi kuwa mkurugenzi wa idara ya nyaraka huru za shirika la habari la BBC, aliongea jioni ya tarehe 26 katika mkutano wa Commons-Sense. Alitumia kama dakika ishirini hivi kuzungumzia uamuzi wa shirika hilo kutumia modeli ya hatimiliki ya Creative Commons. Mradi uitwao The Creative Archive unaruhusu wakazi wa Uingereza (kwakuwa kodi yao ndio inaendesha shirika hili) kutumia kwa njia zozote zile (isipokuwa kibiashara) nyaraka zote za shirika hilo. Mradi huu ulianza rasmi mwaka jana.

Kwakuwa BBC ilianzishwa mwaka 1922, rundo la nyaraka ambazo imehifadhi ni kubwa kiasi ambacho inakupasa ukae mbele ya luninga yako ukitazama bila kuzima kwa miaka 68, masaa 24 kwa siku! Utaweza?

Nimewasili Babiloni. Safari nzima nilikuwa najiuliza, “Hivi nitablogu nini na nini nitaacha?” Kwanza hata pa kuanzia sijiu. Nimeamua kuwa nitakuwa nablogu kila siku mambo kadhaa yaliyotokana na mkutano wa Commons-sense; mambo niliyojifunza, watu niliokutana nao, miradi mbalimbali inayotumia zana mpya za mawasiliano Afrika, niliyoona katika jiji la Egoli/Jozi (majina ya jiji la Johannersburg), mapana na marefu ya dhana hii ya “creative commons” (bado natafuta tafsiri yake sahihi ya Kiswahili), n.k.

Ndio nimeamka nataka kunywa chai. Ningependa kwa sasa utazame video hii ya mahojiano niliyofanya na New Media Lab ya chuo kikuu cha Rhodes. Bonyeza hapa uitazame.

Mshikaji wangu, Donald (jamaa nikitaka kumwelezea sijui nitaanzia wapi), ananizungusha katika jiji la Egoli. Tumetoka katika mahakama ya katiba ambayo ilikuwa ni gereza liitwalo Old Fort. Nimepita kwenye mgahawa huu kutazama jambo fulani kwenye mtandao. Picha na yote yanayohusu mkutano wa Commons-Sense ni mpaka nitakapowasilia Babiloni kwa Joji Kichaka mwizi wa kura. Ninaondoka leo usiku.
Uhuru!

Nimefungua barua pepe toka mviringo wa blogu za Kenya (Kenya Unlimited) kuhusu mahojiano wiki ijayo kuhusu blogu za Kenya kupitia redio ya Open Source. Fuatilia.

Mkutano wa Commons- Sense unaendelea. Asubuhi nilichelewa baada ya kulala saa kumi alfajiri. Basi liliniacha ikabidi niende kwa mshikaji mmoja Mkenya akanileta. Ingawa tulipotea njia niliwahi mduara uliokuwa ukijadili blogu (blogging the commons). Mduara huu nadhani ndio bora katika majadiliano yote toka mkutano uanze. Kama nilivyoahidi nitawapa kwa undani yaliyosemwa na yanayofanyika huku Afrika kuhusiana na blogu na zana nyingine za mawasiliano.

Wanafunzi 15 na walimu wawili wa maabara ya uandishi wa zana mpya za habari katika idara ya uandishi wa habari ya chuo kikuu cha Rhodes hapa Afrika Kusini wanablogu moja kwa moja toka mkutanoni. Nenda hapa ufuatilie kila kinachotendeka kila dakika!

Nimewasili hapa jana baada ya safari ya masaa 17 hivi. Nadhani nilitakiwa kuoga na magadi kabla ya kuondoka ili kuondoa kisirani kwani begi langu la nguo halikufika! Litafika leo usiku na nitalipokea kesho! Niende nikanunue nguo mpya? Nisubiri
Kwa wale wasiofahamu, ninahudhuria mkutano unaoitwa Commons-Sense ulioandaliwa na chuo kikuu cha Wits, Creative Commons (Afrika Kusini), na Links. Mkutano huo unafanyika hapa katika jiji la Egoli ( jina la Kizulu la jiji la Johannersburg). Shughuli rasmi zitaanza leo jioni kwa tafrija ya mkia wa jogoo (kwa kiingereza wanaita “cock tail”). Tayari nimekutana na watu wawili ambao nao wanahudhuria mkutano huu. Dada mmoja toka Kenya na mwingine toka Marekani.
Nenda hapa kwa taarifa zaidi juu ya mkutano huu.
Jana usiku, ingawa nilikuwa nimechoka, sikujisikia kulala. Nilishuka chini (ninakaa hapa) kwenda kuongea na waswahili wenzangu ambao kazi zao ni ulinzi, ufagizi, kufungua milango, n,k. Tsedu ni mlinzi wa usiku hotelini hapa. Anaishi kitongoji cha Alexandra. Tsedu ni rasta: anamuenzi Mfalme wa Wafalme, Simba wa kabila la Yuda Haile Selassie I, Jah! Rastafari!
Tsedu alinivunja mbavu. Baada ya kuniambia kuwa yeye ni rasta na anapenda sana kusikiliza muziki wa hisia na mafunzo, Rege, nilimuuliza kama anampenda Lucky Dube. Akanitazama kwa mshangao na kusema, “Dube hapigi rege. Ile sio rege!” Tsedu anawasikiliza wanamuziki kama Culture, Burning Spear, Bob Marley, Mutabaruka (yule mshairi anayetembea pekupeku), Luciano, n.k. “Rege ni mafunzo, ni tenzi za rohoni, ni mashairi ya kiroho…” Tsedu ananiambia.
Karibu kila wimbo niliomtajia wa wanamuziki anaowasikiliza, alikuwa amekariri maneno yake na hata ufafanuzi wa jinsi ujumbe wa nyimbo hizo unavyoendana na hali ya kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni duniani hivi sasa. Nilipomtajia wimbo wa Burning Spear uitwao “Days of slavery.” Alitabasamu huku akitikisa kichwa. Kisha akaanza kuuimba. “Watu wengi wanaposikiliza huu wimbo wanafikiria mambo yaliyotokea miaka mingi iliyopita. Hapa Afrika Kusini utumwa anaozungumzia Burning Spear upo hadi leo.”
Tulipiga gumzo na Tsedu kwa masaa kadhaa…nadhani nilienda kulala saa tisa. Nilipomtaja Steve Bantu Biko, Tsedu alitazama chini, uso wake ukajaa huzuni. Alikaa kimya kwa muda kisha akasema, “Black consciousness.” Black Consciousness ni jina la falsafa na itikadi aliyokuwa akihubiri mwanamapinduzi Biko. Baada ya muda kidogo alinieleza kwa kina jinsi Biko alivyouawa kinyama. Alivyoburuzwa akiwa amening’inizwa nyuma ya gari katika barabara ya kokoto. Uchi wa myama. Alipomaliza kunieleza kwa undani na hisia kali niligundua kuwa sikuwa ninafahamu kwa kina yaliyotokea siku za mwisho wa uhai wake. Maelezo yake yalinitia hasira na huzuni kwa wakati mmoja. Hadi sasa bado kuna donge limekwama kooni.
Nilipomuuliza Tsedu juu ya kitongoji anachoishi, visa alinieleza visa ambavyo vimenijaza huzuni kubwa. Anasema kuwa maisha wanayoishi Waafrika katika vitongoji mbalimbali nchini humu hayana thamani yoyote. Vifo kutokana na ukimwi, ujambazi wa kutumia silaha vimekuwa ni kitu cha kawaida. “Nikiwa nyumbani nikasikia mlio wa risasi huwa ninaendelea na shughuli zangu. Hata watoto wangu wamezoea. Kila mtu kazoea. Hakuna anayeshtuka. Tumekuwa sugu. Tumekuwa viziwi. Tumekuwa vipofu. Hii ndio njia pekee ya kuendelea kuwa na akili timamu. Bila hivyo utarukwa na akili au utakata tamaa na kujiua. Anasema majambazi katika vitongoji vya weusi wamefika hatua ambayo hakuna kinachowazuia kupora mtu yeyote na saa yeyote. “Majambazi wanampora mtu pembeni yako, unatazama na kuendelea na shughuli zako.” Ananiambia.
Anasema kuwa siku moja aliporwa simu ya mkono. Kawaida akiwa vitongojini hapendi kutumia simu yake. Siku hiyo alisahau kuizima. Akiwa anapita mtaani, simu ikalia. Jamaa watatu wakamfuata, mmoja wao akamwambia, “Pokea hiyo simu. Ukishamaliza kuongea tupe simu yetu.” Wakati wanamwambia hivyo mmoja wao alikuwa amechomoa bastola.
Nitakutana na Tsedu leo usiku baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano na tafrija ya mkia wa jogoo. Usisahau kutembelea tovuti ya mkutano huu. Nitakuwa ninawapa taarifa mbalimbali kadri mkutano unavyoendelea. Ninakwenda kutembea mjini hadi jioni. Sijui nikanunue bastola…maana nataka kwenda ile mitaa ninayoambiwa kuwa nisithubutu kupeleka unyayo. Huko ndio ninataka kwenda. Niombeeni!!!!
Sobonana futhi (tutaonana baadaye kwa Kizulu).

Nilikosea kiungo cha mviringo wa blogu za Kiswahili. Mviringo huu hapa.

Kwanza nilitangaza blogu ya Kishona. Hapa. Kisha nikatangaza blogu ya Kichagga. Hapa. Sasa rafiki yangu, Mokhtar, toka Morocco ameanza kublogu kwa lugha ya Kiberber, Tamazeight. Mokthar ni anafundisha Kiarabu katika chuo hiki. Blogu yake hapa. Nina mambo mengi ya kuandika na kutundika lakini muda umekuwa mdogo. Jumamosi ndio siku ninaongea katika mkutano wa Afrogeeks kuhusu blogu za Kiswahili na jumatatu ninaondoka kwenda Afrika Kusini kwenye mkutano wa Commons-Sense.

Baada ya kuanza kufumuka blogu za Kiswahili, mwanadada toka kule kwa Mangi Horombo, chini ya mlima wa Ruwa (Kilimanjaro), amekuja na blogu kwa lugha ya Kichagga. Mtembelee Mtafiti na blogu yake hapa. Mtafiti hivi sasa yuko masomoni nchini Marekani ila anaendelea kuenzi utamaduni wake.

Shukrani za dhati zinamwendea ndugu yetu Maitha. Ametupatia mviringo wa blogu za Kiswahili. Tembelkea mviringo huo hapa.

Dakika hii ninavyoandika ninasubiri dakika chache kabla ya kufanya mahojiano kuhusu blogu na redio ya Open Source. Nenda hapa.

Idya wa blogu ya Pambazuko kanipa msamiati mpya: Mkumbokrasia. Mkumbokrasia ndicho kimekuwa chakula, maji, na chai ya Watanzania hasa baada ya kuchaguliwa Jakaya Kikwete. Nimekaa kimya, nimesoma yanayotokea Tanzania, nimechambua hoja za wananchi, vijana kwa wazee. Nimeulizwa niseme ninamwonaje Kikwete. Sasa Idya kanipa msukumo wa kukaa chini na kuandika mawazo na mtazamo wangu. Nitatumia msamiati huu wa “mkumbokrasia” kujenga hoja zangu za msingi. Kaa tayari kumeza au kutema vidonge…hiyo itakuwa ni shauri yako. Soma makala mpya za Padri Karugendo na blogu nyingine za Kiswahili wakati ninaandaa jibu kuhusu ninamwonaje Kikwete.

Haya. Kuna makala nne kabambe za Padri Karugendo. Zinaitwa: Tuacheni Tutetee Matumizi ya Kondomu, Tumwogope Mungu kwa Matendo Yetu Yote Kila Siku na Kila Wakati, Papa Benedikto ni Rafiki wa Tanzania, na Elimu, Vijana, na Uchumi. Bonyeza juu ya makala unayotaka kuisoma. Kumbuka makala zake za nyuma ziko katika kona yake, Kalamu ya Padri Karugendo chini ya makala zangu naFreddy Macha.

Tunampokea kwa shangwe, nderemo, vifijo, nyimbo, vigelegele, na ngoma za ukae mwanablogu mwingine mpya wa Kiswahili. Huyu ni dada yetu Da Mija anayeblogu toka Amsterdam, Uholanzi. Sasa tuna dada zetu wanne wanaoblogu kwa Kiswahili. Tuwakaribishe na kuwatia moyo. Kila blogu ya Kiswahili inapojitokeza ninapata furaha isiyoelezeka. Kongoli hapa umsome.

Nipe Aya! ni moja ya makala mbili mpya ambazo nimepandisha hapa ndani. Kaba ya kusoma makala hizi ni vyema ukasoma kwanza makala ya Wazee Afrika ni Vyuo Vikuu ambayo iko katika kona ya makala zangu, chini ya picha yangu. Makala ya kwanza leo inaitwa: Soma Anga, Mawingu, na Nyota Kama Kitabu. Bonyeza hapa. Ya pili ndio hii ya Nipe Aya! Bonyeza hapa.

Kama wewe ni mzungumzaji wa Kiswahili, unaipeda lugha hii na una muda, tafadhali shiriki katika kujenga kamusi elezo ya kiswahili iliyoko katika mfumo wa wiki. Teknolojia ya wiki inawezesha mtu yeyote kushiriki katika kuhariri na kuandika kamusi hii. Ninatafsiri orodha ya mambo ya msingi yanayopswa kuwemo katika kamusi hii. Nenda hapa. Ukiwa na swali lolote kuhusu hili unaweza kuniandikia. Lakini kwa ujumla teknolojia ya wiki ni rahisi sana kwa mtu yeyote yule kuitumia.

Niliutaja huu mkutano siku za nyuma. Usiache kuufuatilia. Ni ule mkutano wa Commons-Sense huko Afrika Kusini. Nenda hapa. Pia kama ni mwanablogu au mtafiti wa masuala ya zana mpya za mawasiliano na habari unaweza kupewa skolashipu. Fanya hima. Nenda hapa kuna fomu fulani ya kujaza.

Tanga kunani? Kuna wimbo ule wanasema kuwa Tanga watu huoga na maji yenye viungo kama mdalasini na iliki! Na Dokta Remmy, katika kibao cha Mariamu anasema, “Waja leo, warudi leo, Tanga mbali…” Sasa kaingia binti kutoka Tanga katika ulimwengu wa blogu za Kiswahili. Blogu yake inaitwa Wanawake na Maendeleo. Nenda hapa umsome na kumkaribisha.

Kuna wakati unasoma jambo, linakuingia hasa hadi unaamua kuacha kusoma na kwenda kunywa maji, kujisaidia, kujinyoosha, kutengeneza chai, kisha unarudi tena kusoma. Ndio imenitokea leo nilipotembelea blogu ya Mwandani. Nimekwenda hapo nikakuta amemnukuu shujaa Marcus Mosiah Garvey. Nimechukua nukuu hiyo. Hii hapa:

Ni wachache tu kati yetu, ambao wanaelewa ni kitu gani kinachomfanya mtu awe mtu!Namaanisha -Mtu asiyeweza kufa moyo; mtu asiyeweza kukata tamaa;
Mtu asiyetegemea wengine wamfanyie yale anayoweza kuyafanya yeye mwenyewe;
Mtu asiyemlaumu Mungu, asiyelaumu mazingira;
mtu asiyelaumu ‘bahati mbaya’ kwa hali yake kimaisha;
Bali yule mtu awezaye kutoka na kujitengenezea mazingira yanayomwezesha kuishi.
Kweli nawaambia, ikiwa sisi watu weusi milioni mia nne tungekuwa tunajitambua,
Na tungetambua kwamba ndani yetu tunao uwezo na haki,
Na kwamba tunayo mamlaka kamili,
Ama kwa hakika nawaambieni, mnamo masaa ishirini na nne tu yajayo tungekuwa na taifa jipya,
Tungekuwa na dola iliyosimama kisawasawa,
Si kutokana na matakwa ya watu wengine wowote ya kutaka kutuona tunatengenekewa,
Bali kutokana na moyo wetu dhabiti wa kutakaka kujiinua,bila kujali watu wengine humu duniani wanatufikiriaje.
-Marcus Mosiah Garvey

Next Page »