November 2005
Monthly Archive
Wed 30 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Msanii wa nguvu na rafiki yangu wa karibu, Mrisho Mwana wa Mpoto, wa kundi la
Parapanda, ambaye niliwahi kuandika habari kuhusu harusi yake ambapo “shampeni” ilikuwa ni maji ya madafu (
bonyeza hapa uisome) kaandika ujumbe ambao umenichekesha ingawa aliyosema sio utani. Anasema kuwa Waafrika ni kama kituko vile. Usome. Naubandika hapa chini:
“Mwafrika nikama kituko maana wanaomba Funding kwa wazungu ili wajadili matatizo yao na jinsi ya kujikomboa toka utumwani sasa icho si kituko yaani mtu akupe pesa ili umjadili yeye alafu unachekelea. Huwezi kubisha …..(
hapa Mrisho kataja jina la mtu ambalo nimelitoa)… Maana juzi tu tulikuwa zanzibar kujadili ujinga wetu mbele yao huku wakitulipa pesa na kulala sehemu nzuri huku tukiomba siku ziongezwe hata bila posho.”
All the Best
Mrisho Mpoto
********************
Huyo ni Mrisho Mpoto, wewe unasemaje kuhusu kuomba fedha kwa wazungu ili tujadili jinsi ya kujikwamua toka kwenye makucha yao ya uchumi, fikra, siasa, na utamaduni tegemezi?
Wed 30 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
NYONGEZA!!!!!: Nilipoandika habari hiyo hapo chini mapema leo sikuelezea jambo fulani muhimu sana. Ni kwamba serikali ya Marekani imetoa hela kwa kampuni ya Lincoln Group. Kampuni hii inachukua “habari” zilizoandikwa na wanajeshi wa Marekani kisha inazitafsiri kwa
Kiarabu kisha inalipa magazeti ya Iraki ili iyachapishe kwa majina tofauti na yale ya askari wa Marekani walioandika. Na huu ndio uhuru, na hii ndio demokrasia ambayo Marekani inataka kusambaza duniani!
*******************************
Nina tabia ya kuviita vyombo vya habari, “vyombo vya uongo.” Usidhani kuwa sina sababu za msingi. Sasa huu ni mfano mmoja. Kampuni iitwayo Lincoln Group imekuwa ikilipa wafanyakazi wake ili wajifanye kuwa ni waandishi wa habari na kuandika habari katika magazeti ya nchini Iraki. Habari hizo nia yake ni kuhadaa akili za Wairaki ili waamini kuwa Marekani ni mkombozi wao na sio mwizi wa mali yao ya asili. Yaani wanachofanya hawa jamaa ambao wanalipwa na serikali ya Marekani ni kupandikiza uzushi kwenye magazeti.
Bonyeza hapa usome habari yenyewe.
Wed 30 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kituo cha Kusini kina mradi wa tovuti ya kumbukumbu ya Mwalimu. Baadhi ya hotuba zake zinapatikana kwenye tovuti hiyo. Nimemaliza kuzisoma. Mwalimu alikuwa ana namna yake fulani ya kufikiria…ila katika yote ni ule uwezo wake wa kuona mbele kuleeeeeeeeee….wakati wa-twawala wengi tulionao hata leo hawaioni (sembuse kesho).
Bonyeza hapa uzisome.
Sun 27 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Macharia Gaitho wa Daily Nation la Kenya
anasema kuwa siku moja baada ya kambi ya Ndizi (iliyokuwa ikiunga mkono katiba mpya ya Kenya) na kambi ya Machungwa (iliyokuwa ikiipinga katiba hiyo) kufanya mkutano katika jiji la Nairobi, alipelekewa ujumbe wa maandishi wa simu ukisema kuwa shirika la uongo la CNN lilikuwa na masikitiko makubwa kwani lilikosa habari ya kutangaza kuhusu Kenya. Maana ya ujumbe huu ni kuwa kwakuwa shirika hilo hupenda kutangaza habari za vita na maaa zaidi ya zile za maendeleo na furaha, hakukuwa na habari nzuri maana walidhani kuwa siku kambi hizo mbili zilipofanya mkutano jijini Nairobi, lazima zingepigwa. Wapi.
Mashirika haya ya uongo yanapenda sana maafa. Tazama
Liberia. Nchi hii wakati ikiwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, vyombo vya habari vilijaa habari kuhusu nchi hiyo. Lakini hivi majuzi baada ya kufanya uchaguzi ambao ni kati ya chaguzi za amani ya juu kabisa duniani, hakuna vyombo vya habari vinavyotuambia habari hiyo. Katika uchaguzi huo wamemchagua Mama
Ellen Johnson-Sirleaf kuwa Rais. Mwanamama huyu amemshinda mwanasoka wa zamani
George Weah. Ingawa yeye ni rais wa kwanza mwanamke Afrika, yeye sio mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika.
Malkia Zauditu wa Ethiopia aliongoza nchi hiyo toka 1916 hadi 1930. Pia mwanamama
Ruth Perry aliwahi kuwa kiongozi wa nchi (sio rais) wa Liberia baada ya kuangushwa kwa Sajenti Samuel Doe na kufa kwa Rais Amos Sawyer. Perry alikuwa ni mwenyekiti wa Baraza la Taifa toka 1996 hadi 1997 alipomwachia madaraka mwizi na muuaji Charles Taylor baada ya “kushinda” uchaguzi.
Sielewi kwanini nimepitia njia ndefu namna hiyo hadi kufikia kwenye jambo nililotaka kusema. Niliyoandika hapo juu na ninayoandika hapa sasa hivi hayana uhusiano wa moja kwa moja. Nilifungua ukurasa huu ili niandike kuhusu Kibaki lakini mawazo mengine yakanijia. Sasa niko kwa Kibaki.
Nadhani Kibaki alipokuwa mdogo alikuwa ni matata sana kwa matani. Akina Moi nadhani walikuwa hawafungui mdomo kwa matani. Basi wakati wa kampeni zake za kutaka wananchi waunge mkono katiba iliyokuwa imfanye kuwa mfalme, aliwaita wale wanaoipinga kuwa ni wapumbavu. Ila kali kabisa ni pale aliposema kuwa wao ni “mavi ya kuku.” Sijui huwa anatumia mdomo huu huu unaoshusha haya matani kula chakula na pia kusali au ana mdomo mwingine?
Fri 25 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kuna blogu mpya ya ndugu Materu iitwayo Fikra Thabiti. Ili umsome bonyeza hapa. Pia aliyekuwa mwandishi wa gazeti la Daily News kwa muda mrefu, Chemi Che Mponda, kaanzisha blogu ya Kiswahili. Kutokana na shughuli utaona hajaweka mapya kwa muda ila anasema ataivalia njuga karibuni. Che Mponda, zaidi ya kuwa mwandishi wa habari, ni muigizaji wa filamu na michezo ya kuigiza. Ameshiriki kwenye filamu ya Tusamahe na Maangamizi. Bonyeza hapa usome blogu ya Chemi. Bonyeza hapa utembelee tovuti yake yenye habari zaidi kuhusu fiamu na michezo ya kuigiza aliyoshiriki.
Thu 24 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Gazeti la Uingereza la Daily Mirror limetoboa kisa hiki: eti Joji Kichaka alitaka kupiga mabomu kituo cha luninga anachokichukia kupita kiasi cha
Al Jazeera.
Bonyeza hapa usome kisanga chenyewe. Sasa wafanyakazi wa Al Jazeera wameanzisha blogu kumtaka Kichaka asiwapige mabomu. Hata hivyo wamemwambia kuwa hawatishiki.
Bonyeza hapa utembelee blogu yao.
Thu 24 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni [5]
Nilisema ninavuta pumzi nizungumze kuhusu utamaduni. Utaona kuna wasomaji wameacha maoni wakishutumu wale tunaopinga tabia ya kudharau utamaduni wetu na kukimbilia wa wengine. Wameuliza eti mbona tunavaa viatu na nguo? Mmoja kasema kama tunatetea utamaduni kwanini tusirudi enzi za kuvaa ngozi? Wasomaji hawa nadhani hawafahamu kuwa jamii mbalimbali Afrika zilikuwa tayari zina viwanda vya nguo wakati weupe wakiwa wanaishi mapangoni na kula nyama za watu! Niliwahi kuandika makala nikizungumzia mada hii ya kuvaa nguo/viatu na kutetea utamaduni. Kichwa chake kilikuwa: Kama Unapenda Utamaduni Mbona Unavaa Nguo? Hapo chini nimeweka vipande kadhaa toka kwenye makala hyo. Ila unaweza kusoma makala nzima kwa
kubonyeza hapa.
*********************************************
Vipande vyenyewe hivi hapa:
“Mara nyingi mtu unapozungumzia utamaduni wa Mtanzania au Mwafrika, inachukuliwa kuwa unazungumzia tu mambo ya kale. Kwa watu wengi utamaduni na ukale ni kitu kimoja. Watu wanaoamini hivyo huchulia kuwa utamaduni ni kitu cha zamani sana. Kitu kikuukuu. Kimezeeka. Kimetoka kwa mababu na mababu. Kwa maana hii watu wa leo tunarithi utamaduni tulioachiwa na mababu ila sisi haturithishi kizazi kijacho utamaduni mpya (unaotokana na kizazi chetu) bali ule tuliopokea toka kwa waliotutangulia.
Ukikutana na watu wanaofikiri kuwa utamaduni ni ukale kuna swali moja linalochekesha sana ambalo lazima wakuulize huku wakikutolea macho kama vile unafanya uhaini kutetea utamaduni wako: Kama unapenda utamaduni wa Mwafrika kwanini unavaa nguo? Kwanini unavaa viatu?”
****************************************
“Ukidhani kuwa ninaposema tupende utamaduni wetu ninamaanisha kuwa tufanye yote yaliyofanywa na mababu zetu utakuwa umefanya kosa kubwa sana. Kwani mababu zetu walikuwa ni miungu? Kwanini tuchukue kila walichofanya kama vile walikuwa hawana mapungufu? Mababu zetu ni binadamu kama sisi. Walikuwa na mazuri na mabaya pia. Je tukubali kukeketa wanawake maana ni urithi wetu? Hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuendelea kukeketa wanawake hata kama tendo hili lilifanywa na mababu zetu.”
**************************************************
“Kuna jambo linalonishangaza ninapokutana na wale wanaoniuliza, “Kama unatetea utamaduni mbona unavaa nguo?” Kwanini wanapozungumzia utamaduni wa watu weupe hawarudi nyuma na kuganda kwenye historia. Wanachukulia kuwa wanayofanya leo hii watu weupe ndio utamaduni wao, ila sisi Waafrika utamaduni wetu ni yale tuliyofanya wakati tukiwa tunatembea uchi. Utamaduni wa watu weupe ni yanayofanywa leo na wa kwetu ni yake ya zamani. Ni kitu gani kinachofanya kuvaa nguo kuwe ni utamaduni wa watu weupe ila sio Waafrika?
Mtazamo huu unaashiria kuwa kuna watu hawategemei Waafrika twende mbele maana itakuwa kinyume na utamaduni wetu! Mtazamo mbovu sana huu. Mbona hata hao watu weupe kuna kipindi katika historia yao ambacho waliishi mapangoni, walitembea uchi, walikula nyama mbichi, walikula nyama za watu, waliua wachawi hadharani, n.k. Watu wengi hawafahamu historia hii maana shuleni tunafundishwa historia yetu toka tukiwa tunatumia zana za mawe, tukiishi na kuchora picha mapangoni ila historia ya watu weupe inaanzia zama za mapinduzi ya viwanda. Kutokana na hili, watu wengi wanaona kuwa utamaduni wa mtu mweupe ni mambo ya kileo.”
***************************************
“Hakuna jamii yoyote isiyokua, isiyobadilika, isiyochukua mapya, isiyotupa ya zamani, na isiyohifadhi yale ya zamani yanayofaa. Nipe mfano wa jamii kama hiyo. Hoja hii ndio ambayo inawapa tabu wanaotetea ukeketaji wa wanawake kwa madai kuwa ni utamaduni. Kwa uelewa wa zama zile za mababu, tendo hili lilionekana kuwa ni sahihi. Ila kwa uelewa wa mazingira tunayoishi leo tendo hili linaonekana kuwa sio sahihi.”
Wed 23 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kama kuna siku mabata hapa duniani yanapata ni hapo kesho. Kama kuna siku bata wanaliwa kwa wingi hapa duniani ni hapo kesho Wamarekani wanaposherehekea sikukuu ya “thanksgiving.” Kesho ni siku ya kula bata kama vile sijui nini…nchi nzima itakula bata kwa mlo wa mchana. Bonyeza hapa usome kuhusu sikukuu hiyo.
**************************************************
Halafu: Navuta pumzi kisha niongelee mambo kadhaa ambayo wasomaji waliotoa maoni wamezungumzia hasa suala la utamaduni na kuiga.
Wed 23 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Waliopiga kura kuitakaa katiba iliyokuwa imfanye rais wa Kenya kuwa kama mfalume wameshinda. Ila Rais wa Kenya, Mzee Mwai Kibaki amesema kuwa Wakenya wanapaswa kujua kuwa Kenya tayari ina katiba ambayo imekuwa ikitumika siku zote!
Umeelewa undani wa kauli yake hiyo?
Mon 21 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Wapiga kura wa upande wa machunga ambao unakataa katiba mpya inayomlimbikizia Rais madaraka wanaongoza. Wanaounga mkono katiba hiyo (wanaotumia alama ya ndizi) wanaongozwa na Rais Kibaki ambaye wakati akiwa nje ya madaraka alitaka Kenya iwe na katiba ambayo haitampa mtu mmoja madaraka makubwa. Lakini alipoingia madarakani…au kwenye utamu kama mnavyojua…anataka alimbikiziwe madaraka kama vile yeye ni Mungu. Wanaosema “Hapana” wanaongoza kwa asilimia 56.
Mon 21 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Ule mchuano wa blogu bora katika katika vigezo na lugha mbalimbali (Kiswahili hakimo!) umemalizika. Na kwa upande wa blogu za kiinglishi (kiingereza) blogu ya Mradi wa Sauti za Dunia imeshinda. Shukrani zinakwenda kwa waliopiga kura.
Bonyeza hapa uone tangazo la ushindi huo.
Bonyeza hapa uone blogu zote zilizoshinda.
Sun 20 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni [12]
Mjadala kuhusu muziki wa “kizazi kipya” umepamba moto.
Jeff na
Ramadhani wameuanzisha. Na wasomaji wao wameudaka. Maswali kadhaa bado yanaelea hewani. Hivi “kizazi kipya” ndio akina nani? Na Bongo Flava ndio nini hasa?
Ukitazama kizazi tunachokiita kipya. Ukaangalia tabia, mwenendo, fikra, na njozi zake utakubaliana nami (kama huwa unapenda kuita beleshi kuwa ni beleshi) kuwa jina sahihi la “kizazi kipya” ni “watumwa wapya.”
Watumwa wa zamani walidakwa kifikra, kitamaduni, na kiroho katika wimbi la ukoloni, safari za “wavumbuzi,” na kazi za wasambaza “ustaarabu” (wamisionari). Leo hii wimbi linalokumba kizazi kipya cha watumwa wapya ni wimbi la utandawizi. Utandawizi ndio ukoloni mpya. Wimbi hili linasukumwa na falsafa na itikadi za soko na ulaji. Soko lenyewe sio soko kama la Kariakoo au Kiboriloni. Nitamwachia Nkya wa
Pambazuko achambue zaidi juu ya hii dhana ya soko. Kwa kifupi dhana ya soko katika ubepari haina maana mahali pa kuuza na kununua. Na ninaposema ulaji simaanishi ulaji kama ule wa kula ugali na kisamvu. Kwa kilugha chao wanaita “consumerism.” Katiba ubepari dubwana hili ulaji (consumerism) ndio ibada.
Zamani zile waliotutangulia walitekwa kwa njia mbalimbali, baadhi zikiwa za kinyama (viboko, bundiki, vifungo), nyingine vitisho (utakwenda motoni usipoamini dini yetu), elimu, n.k. Leo hii mabwana wa utumwa wala hawana haja ya kuja na viboko na au kutuma watu wao na biblia na kurani kutuhadaa tukatae tamaduni zetu. Mazingira yamebadilika na mbinu zimebadilika. Lakini pia ziko nyingine zimebaki vile vile au kubadilika kidogo. Vitukuu wa wale waliotia minyororo fikra za mababu zetu ndio hivi sasa wanakaza pingu katika akili za hawa tunaowaita “kizazi kipya.” Wanatumia tamaduni maarufu (kilugha chao wanaita pop culture) na vyombo vya uongo kama MTV. Wanatumia picha za wanamuziki wakiwa wamevaa nguo za aina fulani kuwafanya watumwa wapya wadhani kuwa ili wawe wanamuziki wakubwa wanapaswa kuvaa nguo kama hizo, mikufu, na pia kuwa na majina kama Crazy G na hata kubadili namna ya kutembea. Wanatumia majarida. Wanatumia filamu na muziki. Wanatumia redio za FM na Ma-DJ ambao ndio vinara wa utumwa mpya. Wanatumia vipindi vya luninga kama Big Brother. Wanatumia mashindano kama Miss Tanzania. Wanatumia mikufu ya dhahabu (mingine ikiwa ni ya msalaba). Wanatumia mapicha makubwa ya ukutani ya watu kama akina 50 Cent.
Unajua wengi tunaona utamaduni kuwa ni kitu cha mchezo mchezo. Hasa tunapodhani kuwa utamaduni ni ngoma za kukata kiuno, vinyago vya wamakonde, ngonjera, na nguo za batiki. Utamaduni ni rasilimali. Watu wakizimikia utamaduni wako watazimikia pia na bidhaa zako (hadi bendera ya nchi yako wataivaa). Unakuta kuna nchi zinatambua hili na zinafanya kila liwezekanalo kulinda utamaduni wao. Wanatumia sera, sheria, elimu, n.k. kutimiza azma hiyo. Nchi kama Ufaransa zina idadi maalumu ya sinema za Marekani zinazoruhusiwa kuonyeshwa katika majumba ya sinema nchini humo. Nia yake ni kulinda soko la watengeneza sinema wa ndani. Sheria ya mambo ya Intaneti Ufaransa inasema kuwa tovuti yoyote ile ya Ufaransa lazima iwe na lugha ya Kifaransa. Inaweza kuwa kwa Kiingereza au Kijerumani lakini lazima kuwe na toleo la Kifaransa.
Lakini pia utamaduni unaweza kuwa mpambano. Ni mpambano wa mitazamo. Mfano mzuri wa hili ni ugaidi. Ugaidi una sura nyingi. Upande mmoja wa sura ya ugaidi ni utamaduni. Unaweza kutazama ugaidi kama mgongano wa mitazamo ya kitamaduni kuhusu demokrasia, wema, ubaya, historia, n.k.
Nirudi kwenye hoja ya msingi. Wakati tunapotazama kundi tunaloliita “kizazi kipya,” mimi ninachoona ni kizazi cha watumwa wapya. Tena watumwa kwa maana mbili. Kwanza, watumwa wa kifikra na kitamaduni. Pili, watumwa kiuchumi, kwa maana ya kuwa katika nchi yao bila uwezo wa kumiliki njia kuu za uchumi au kuwa na uwezo wa kutoa maamuzi makuu kuhusu uendeshwaji wa nchi.
Wa-twawala wanapenda sana kizazi hiki kinapotumia muda mwingi “kujirusha” na Bongo Flava au kuketi mbele ya luninga wakitazama Big Brother wakati nchi keki ya nchi inamalizwa. Kwa akili za kizazi hiki cha watumwa wapya, kitendo cha kuwa na luninga zinazoonyesha Big Brother, redio za FM za kupiga miziki yao, luninga za kuonyesha video zao, na majengo marefu marefu yanayojengwa mjini ambayo wanayatumia katika kutengeneza video zao za muziki, bila kusahau hoteli za kifahari ambazo nazo wanazitumia kutengeneza video hizo…mambo haya kwao ni alama ya maendeleo makubwa ya nchi. Na nchi kwao huwa ni mjini.
Sat 19 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kama kuna mtu ana mpango wa kujilipua ndani ya treni au mabasi pale London kwa Malikia Lizabeti, namshauri asithubutu kufanya hivyo mwezi ujao. Mwezi ujao nitakuwa yaliyo makao makuu ya shirika la habari la
Reuters, Canary Wharf, London. Nitakuwa hapo kwenye mkutano wa pili wa kila mwaka wa Mradi wa Sauti za Dunia.
Mradi wa Sauti za dunia uko chini ya
Kituo cha Berkman cha Intaneti na Jamii katika chuo kikuu cha Harvard. Habari zaidi kuhusu mradi wa Sauti za Dunia ulivyoanza na pia kuhusu mkutano wa London mwezi ujao na watu wanaohudhuria,
bonyeza hapa. Utaona kuwa kati ya wanaohudhuria ni wanablogu wawili mahiri wa Kenya,
Kenyan Pundit na
Mshairi. Mshairi huandika habari kuhusu wanablogu wanawake wa Afrika kila jumatatu katika blogu ya Sauti za Dunia.
Kwahiyo wasomaji wangu, ndugu, na marafiki wa Uingereza, tuwasiliane ili tuweze kunywa chai na kupiga gumzo (Masawe, Maruma, Kibwana, Mgosi, Theodore, Freddy, Neema (JALO!!!) …mpo?).
Sat 19 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Ndugu Chris Bwalya yuko Arusha. Anablogu kwa Kiswahili na Kiingereza.
Bonyeza hapa umsome. Blogu yake haipokei maoni. Nadhani atabadili ili kuruhusu watu kutoa maoni. Nadhani kutakuwa na mijadala mikali kutokana na masuala ambayo anazungumzia. Anaandika, pamoja na mambo mengine, kuhusu ukristo, biblia, yesu, n.k.
Sat 19 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Hebu bonyeza hapa uende kwa Ndugu Msangi umsome. Kisha soma maoni motomoto ya wasomaji na pia ongeza yako.
****************************************************
Wakati huo huo….
Mapema leo wakati nikiipitia blogu mpya ya ndugu
Nyembo nilikutana na hoja yake ya agano jipya na la kale. Agano la Kale ndio lile ambalo tumeambiwa kuwa hakuna anayejua liko wapi…yaani mkataba wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Nimependa aliposema haya, “Kuipaka rangi Manowari si njia sahihi ya kuzuia maji kupenya…”
Sat 19 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Tarehe 20 mwezi huu ndio mwisho wa kupigia kura blogu bora kwa ajili ya Tuzo ya Blogu Bora.
Mradi wa Sauti za Dunia (Global Voices) ni miongoni mwa blogu zilizo katika mchuano huo kwa upande wa lugha ya Kiingereza.
Bonyeza hapa uwapigie kura. Ukifika hapo tafuta lilipo kundi la blogu za kiingereza. Piga kura yako.
Mradi wa Sauti za Dunia umetoa nafasi kila wiki kwa ajili ya muhtasari wa blogu za Kiswahili. Kulikuwa na uwezekano wa kuweka eneo ambalo wanablogu wa Kiswahili wangekuwa na ukurasa wao katika blogu ya mradi huo ila kukawa na hoja kuwa ukifanya hivyo itabidi utoe ukurasa kwa kila lugha. Kwa kifupi, mradi huu unaheshimu mno kazi zinazofanywa na wanablogu wa Kiswahili. Na kazi hiyo ni kuondoa ukoloni mamboleo mtandaoni na kupanua wigo wa lugha zinatotumika katika mijadala kwenye Intaneti. Sababu hii ndio inanifanya kuwataka mupige kura zenu kwa ajili ya Sauti za Dunia.
Basi bonyeza hapa. Kura inachukua nusu dakika.
Fri 18 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Bwana Nyembo kajiuliza kwanini naye asiamue kuwa na blogu yake ili kutoa mawazo yake mtandaoni? Huyu ni mwabablogu mpya wa Kiswahili. Kanifurahisha mahali fulani ambapo kabadili msemo wa Kiswahili usemao “Asiyekubali kushindwa sio mshindani.” Yeye anasema kuwa kule Zanzibar, “Asiyekubali kushindwa ni shujaa!” Bonyeza hapa usome blogu yake na kumkaribisha.
Wed 16 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kundi moja linalojiita vuguvugu la Njano lilikwenda mahakamani likitaka zoezi la kupiga kura ya maoni ya “ndiyo” au “hapana” kuhusu katiba mpya nchini Kenya lisimamishwe. Kundi hili lilidai kuwa bunge lilipounda sheria ya kutengeneza katiba mpya lilijichukulia mamlaka ambayo yako mikononi mwa wananchi. Pia likadai kuwa tume ya uchaguzi ya Kenya haina haki kisheria kusimamia zoezi hilo maana tume hii imepewa wajibu wa kusimamia uchaguzi wa wabunge na rais na sio kura ya maoni kuhusu katiba. Wanasheria wa kundi hili walidai kuwa kesi hii pengine ni kesi ya pili kwa ukubwa nchini Kenya ukiachilia mbali ile ya shujaa
Dedan Kimathi. Jana Mahakama Kuu nchini Kenya imeamua kuwa zoezi hilo litaendelea.
Bonyeza hapa usome habari hiyo.
Wakati huo huo jamaa wa
Kenya National Commission of Human Rights ambao wanafuatilia kwa karibu kampeni za kura hii ya maoni, wana “orodha ya aibu” katika tovuti yao. Orodha hii inaonyesha matumizi mabovu ya mali ya umma na kauli za uchochezi toka kwa waongo na wezi wanaojiita wanasiasa nchini humo.
Bonyeza hapa utazame orodha hiyo.
Mon 14 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanya kampeni kwa kutumia barua pepe. Nimefurahi kujua hili maana haya ndio kati ya mambo ninayotazama kwa karibu (kwasababu za kitaaluma). Ninaamanisha matumizi ya zana mpya za mawasiliano katika kampeni za urais na ubunge.
Kuna mistari ambayo iko katika barua pepe yao ambayo nimeona niwagawieni kidogo (iwapo hujapata barua pepe hiyo). Nabandika hapo chini mistari hiyo:
Maendeleo ya Kweli
hayawezi kuletwana
Mafisadi wale wale
wa Chama kile kile
chenye Uoza ule ule
Wakiendeleza yale yale
eti kwa Kasi mpya,
Nguvu mpya
na Ari mpya.
Sun 13 Nov 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Naendeleza mjadala nilioandika jana ulioitwa: Tatizo ni Wa-twawala au Watawaliwa? Kama hukuusoma
bonyeza hapa uusome kisha urudi hapa ndipo uendelee.
*********************************
Kenya itazameni. Kuna masomo chungu nzima pale. Unaona tunavyoonyeshwa kuwa kuna uwezekano kuwa wapinzani na wa-twawala hawana tofauti zaidi ya kuwa upande mmoja uko madarakani na upande mwingine unataka kuyachukua. Wapinzani watapinga mambo yote yanayofanywa na walioko madarakani. Lakini wakiingia madarakani watayafanya yote waliyokuwa wakiyapinga na hata mabaya zaidi. Na wale waliokuwa madarakani wataanza kupinga mambo ambayo nao walipokuwa madarakani waliyafanya. Kumbuka Kaunda alivyotiwa ndani na sheria ambayo alikuwa yeye mwenyewe akiitumia. Akadai kuwa sheria ya kutia watu kizuizini ni kinyume na haki za binadamu. Yaani haki hizo anaziona pale yeye ndiye anapokuwa anakandamizwa.
Pale Kenya waliokuwa wakiiunga mkono katiba wakati wakiwa wapinzani, wameikataa walipoingia madarakani. Waliokuwa wakiikataa wakati wakiwa madarakani sasa wanaikubali. Yote hii ni mchezo wa kuhadaa wananchi kwa nia ya kushika madaraka. Midomo ya wanasiasa ni bomba la uongo. Jana niligusia suala la wanasiasa wanaohama vyama vyao baada ya kutochaguliwa kugombea uongozi wakidai kuwa vyama hivyo havifai. Vyama wanavyohamia vikija kuacha kuwapa nafasi za kugombea uongozi wataondoka wakidai kuwa navyo havifai. Wewe mtu umekuwa kwenye chama toka ukiwa kijana, leo hii umezeeka unakuja kudai eti chama hicho hakifai kuongoza. Na unasema hayo mara tu baada ya kuchujwa kwenye kura ya maoni.
Au tazama kiongozi wa chama fulani anayelalamika juu ya viongozi wasiotaka kuachia madaraka au marais wanaobadili katiba ili waendelee kuwa madarakani wakati yeye mwenyewe hayo madaraka ndani ya chama chake hajayaachia. Ni nini kinakufanya wewe uwe na haki ya kuwa mwenyekiti wa kudumu wa chama chako (au cheo kingine cha “maisha” ndani ya chama chako) na wakati mwingine mgombea urais wa maisha, lakini mpinzani wako hana haki ya kung’ang’ania madaraka?
Jana nilisema kuwa tabaka la wa-twawala limefanikiwa kutufanya tuamini kuwa huu mfumo wa ulaji na ukandamizaji wanaouita “demokrasia” ndio njia pekee ambayo binadamu wanaweza kutumia kujenga taifa. Tazama bunge la Kenya kwa dakika chache. Bunge hili ni upenyo wa kujitajirisha na kuipora nchi. Mwezi uliopita bunge nchini Kenya kwa dakika 30 liliruhusu wizara 18 kuchukua zaidi ya shilingi za Kenya bilioni 100 toka kwenye mfuko maalum. Kwa nusu saa shilingi bilioni 100 za nchi masikini kama Kenya zimeyeyuka. Kura hiyo ilipitishwa na wabunge wangapi unajua? 22!
Sisi wananchi wa kawaida, tabaka la waliwao, tuna uwezo wa kukataa kunyonywa na kudanganywa. Tuna wajibu wa kikatiba na hata kiroho (kama unaamini kuna kitu kama roho) kukataa kuwa chini ya hili tabaka dogo la wezi na wauza nchi. Kuna sababu za kutotimiza wajibu huu?
— Next Page »