December 2005
Monthly Archive
Fri 30 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni [12]

Michuzi sio tu ana ujuzi wa kupiga picha bali pia ni mwimbaji mashuhuri sana hasa akiwa nchi za nje. Katika picha hii Watanzania tuliokuwa katika
mkutano kuhusu utandawizi na demokrasia katika jiji la Helsinki, Ufini mwezi Septemba, tunatumbuiza. Siku hii ilikuwa ndio mwisho wa mkutano. Tukiwa katika tamasha la kuaga wana mkutano, Mama Maria Shaba ghafla alitufuata mimi na Michuzi nje. “Watanzania lazima tuwakilishe.”
Nikamuuliza, “Tuwakilishe vipi?”
Akasema, “Toka tuje wanaoimba na kutumbuiza ni Wafini, kwani sisi hatuna sauti? Lazima tukaimbe.”
Basi akatukusanya Watanzania mmoja mmoja. Hakuna kukataa. Hao jukwaani. Mnajua tuliimba wimbo gani? Buni….tuliimba Malaika. Michuzi akiwa ndio sauti ya nne. Katika picha unamuona Mama Shaba akiwa ameshika kipaza sauti. Pia unaweza kumuona Mama Mwingira wa Tango kushoto kwa Maria Shaba. Mimi nadhani nilikuwa naimba sauti ya 60! Baada ya kumaliza wimbo wa Malaika, tuliaga jukwaa, huku tukishangiliwa kwa nguvu, kwa wimbo wa Bob Marley: Get Up, Stand Up. Wimbo huu ndio wimbo rasmi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.
Ili uione picha kwa uzuri zaidi bonyeza juu ya picha yenyewe (peleka mkono wa kipanya cha tarakilishi yako).
Fri 30 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni

Sio muda mrefu nimemaliza kuonga na
Jeff Msangi ambaye alikuwa akimzungusha mjini Toronto
Boniphace Makene. Katika maongezi yetu tuligusia umuhimu wa kuanza kupanua matumizi ya blogu zetu kwa kuweka picha pale panapofaa na hata kuingilia blogu za sauti na video. Wakati wake utafika.
Baada ya kuongea na Jeff kuhusu picha nikatembelea kamera ya Michuzi nikakuta amewaka picha ambayo imenikumbusha picha ambazo nilisahau kabisa kuziweka kwenye blogu. Bonyeza hapa uone picha aliyotupiga Michuzi nikiwa na mzee mwenyewe Mti Mkubwa (ambaye amebatizwa jina jipya: Mti Mkubwa Mkavu). Basi ndipo nikaanza kuchimba picha nilizonazo toka Helsinki.
Nimeweka picha ya kikosi kamili cha Watanzania wanaoishi Helsinki na wale ambao tulikuwa tuko ziarani hapo. Utamuona Michuzi mwenyewe na Mti Mkubwa Mkavu wakitabasamu. Picha hii ilipigwa na rafiki yangu, Vikii wa jarida la mtandaoni la nchini Malaysia, Malaysiakini. Hapa tulipokuwa ni eneo la kujidai la Watanzania wanaoishi jijini hapo (Fide: klabu ile inaitwa nini tena?).
Ukitaka kuiona picha hii vizuri, peleka mkono wa kipanya chako juu ya picha kisha bonyeza.
**Nyongeza:
Ametokea mtu akaweka majina ya walioko kwenye picha hii kwenye sehemu ya maoni. Pia jina la klabu yenyewe, Chelsea Sports Pub. Majina ya walioko kwenye picha haya hapa:
Pichani kutoka kushoto ni Lwitiko Mwalukasa, Benard Kakengi, Mapinduzi Mwankemwa, Mzee Kimaro, ? , Raymond Mutafungwa, ? , Dennis Londo, Muhidin Issa Michuzi, F MtiMkubwa Tungaraza, Ndesanjo Macha, Magonera Malima, na Kisakisa Kiwara. Picha ilipigwa ndani ya Sports Pub Chelsea. Ukifika Helsinki usiwe na wasiwasi wa kuwapata Watanzania fika Chelsea Sports Pub utawakuta wakinywa na kusogoa masuala mbali mbali ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi.
Fri 30 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Mmoja wa waanzilishi wa
Mradi wa Sauti za Dunia,
Ethan Zuckerman, ameaandaa ka-mtihani kadogo kuhusu Afrika. Jaribu kufanya mtihani huo uone unafuatilia masuala ya Afrika kwa kiasi gani. Nimekosa swali moja kwa ujinga! Tena swali lenyewe linahusu jambo ambalo ninalifuatilia kwa karibu sana, matumizi ya simu za mkono Afrika.
Bonyeza hapa ujaribu bahati yako. Kisha
bonyeza hapa usome aliyoandika kuhusu ka-mtihaki hako na maoni ya waliojaribu. Iwapo hutaki “kuibia” nakushauri ufanye mtihani wenyewe kabla ya kusoma maoni ya watu maana pale utapata baadhi ya majibu. Ukifanya hivyo utakuwa unajidanganya mwenyewe. Ukipata F tuambiane!
Huko nyuma niliwahi kutoa jaribio jingine lilloandaliwa na mradi wa SchoolNet. Jaribio lao, kama ambavyo utaona, linakupa nafasi ya kuchagua unataka maswali magumu au mepesimepesi. Kama umetoka Afrika, chagua maswali magumu kabisa. Chini ya ramani utakayoiona ukibonyeza kiungo nitakachokupa ndio kuna sehemu ya kuchagua kama unataka mteremko au la.
Bonyeza hapa ujaribu. Kama umepata sifuri tuambie usifiche!
Thu 29 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Zamani kulikuwa na gazeti Tanzania lililoitwa Baragumu (labda limefufuka tena, sijui). Baragumu ninayozungumzia sio hilo gazeti bali ni blogu mpya ya ndugu yetu ambaye alikuwa mwanablogu hata kabla hajawa na blogu yake mwenyewe kutokana na ushiriki wake kupitia maoni yake katika blogu mbalimbali. Huyu ni ndugu Mwaipopo anayeblogu toka Alabama.
Bonyeza hapa ukamsabahi.
Mon 26 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Jua ndio linachomoza kwenye uwanja wa blogu za Kiswahili (huku tukiwa bado tunatafuta neno muafaka la chombo au uwanja huu…
Da Mija ameweka kiungo cha uwanja wa kuendesha mjadala huu). Napenda kumtangaza mwanablogu mpya, Kaka Pori. Kwa maneno yake mwenyewe anasema kuwa lengo la blogu yake ni:
“Tumetawaliwa kiakili kiasi kwamba tumesahau kabisa sisi ni akina nani. Sasa basi, kwa kupitia blogu hii, tutaamshana, kukumbushana na kupeana hamasa ya kujitambua kwa kupeana habari chanya na mawazo jengevu. Ili tuweze kujenga jamii chanya, tunahitaji umoja, mshikamano, kujielewa na kuelewana, kuhabarishana, n.k. Nipo nanyi nyote na ninaomba kujiunga nanyi.”
Bonyeza hapa umtembelee na kumkaribisha. Utamaduni wa kukaribishana ni mzuri sana na ninaombe tuuendeleze.
Kiungo nilichoongelea hapo juu cha kibanda cha kubunga bongo kuhusu neno muafaka la blogu utakipata
ukibonyeza hapa.
Fri 23 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Majuzi nilikuwa nafanya mahojiano kuhusu blogu zetu za Kiswahili. Jambo moja ambalo nilisema kuwa napenda kuona likitokea ni kuwepo kwa blogu za watu wenye fikra mbalimbali zinazotofautiana. Kujadiliana na watu wanaofikiri kama wewe ni sawa ila unaweza usikue kifikra na pia usipate changamoto ya kuhoji fikra zako mwenyewe na kutafuta maarifa zaidi. Sio vyema tukiwa na blogu za watu wote wanaokubaliana. Kwahiyo nchi kama Irani (ambayo ina blogu zaidi ya laki moja) na Marekani ambapo zipo blogu za wananchi wenye fikra za mrengo wa kushoto, katikati, kulia, n.k. Hapo utakuta mawazo ya watu wanaotetea mfumo na mambo yalivyo hivi sasa na blogu zenye kunyooshea kidole mfumo wa utawala, utamaduni, elimu, n.k. Utakuta pia blogu za vichekesho na kejeli, blogu za fasihi, n.k. Pia unakuta zipo blogu za picha, za video, za sauti (podikasiti), n.k. Unaweza pia kuona kuna blogu nyingine za kufundishia, za kutangazia biashara, za wasafiri, wanamichezo, n.k.
Chemi Che Mponda alipoandika juu ya matako makubwa nikaona kuwa huenda huo ndio mwanzo wa blogu zinazozungumzia masuala ambayo hatupendi kuyazungumzia hadharani.
Bonyeza hapa usome. Ndugu Swai naye alianzisha blogu yake akawa anaandika masuala kwa staili yake na masuala ambayo wanablogu wengine hatuandiki. Lakini amekuwa kimya kwa muda.
Bonyeza hapa uone blogu yake.
Sasa amekuja mwanablogu wa picha ambaye bado sijamuelewa hasa mwelekeo au nia yake. Pia hajaandika jina lake na anasema anaishi “cybercity.” Yaani mji wake uko kwenye mtandao wa kompyuta. Utaona kuwa huyu bwana ni mtu wa utani sana. Hii ni staili nyingine ya blogu (naamini kuwa waliopigwa picha wametoa ruhusu picha zao kutumia. Katika mwongozo mpya wa wanablogu wapya ninaoandika, ninazungumzia masuala ya kisheria kuhusu blogu zetu hizi. Nitagusia kuhusu matumizi ya picha) ya picha tofauti na ile blogu ya kwanza ya picha ya Issa Michuzi.
Itazame hapa.
Huyu bwana nimeanza kuhisi kuwa ni nani. Ila kwakuwa hajapenda kujitangaza jina sio vizuri kumtaja hata kama unamfahamu. Katika mwongozo ninaoandika, ninaongelea pia kuhusu namna ya kublogu kama hutaki ujulikane kuwa wewe ni nani. Kuna mbinu za kiufundi ambazo unatakiwa kutumia maana hata usipotumia jina lako, ni rahisi mtu kujua kompyuta unayotumia na huduma za intaneti unazipata toka kwa nani. Kila kompyuta ina namba ambayo ni rahisi sana kuipata. Njia hii imetumiwa majuzi huko China kumtia jela kwa miaka 10 mwandishi wa habari wa China. Yahoo! iliisaidia serikali ya China kumtambua mwandishi huyu.
Bonyeza hapa usome habari hiyo.
*****************************
Ninasafiri kwa siku mbili tatu hivi kimapumziko. Nitakuwa nachungulia mtandaoni kwa chati. Nadhani jumatatu ndio nitaweza kuandika tena nikiwa nimetulia. Kama nitaandika kabla ya hapo itakuwa ni juujuu au jambo la muhimu sana.
********************************
Wakati huo huo: ninajiandaa kusherehekea sikukuu ya Kwanzaa. Sikukuu hii husherehekewa kwa kukumbuka na kuenzi nguzo saba.
Bonyeza hapa uzione. Zaidi juu ya sikukuu hii baadaye. Kwa sasa
bofya hapa usome kuhusu sikukuu hii.
Wed 21 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Nani alisema kuwa kule Musoma hakuna wanablogu? Acha utani…yupo mwanablogu mpya wa Tafakari ya Maisha toka Musoma. Anauliza ni kitu gani cha muhimu kati ya uhai na kuvaa? Sasa kama kawaida yetu tumkaribishe. Bonyeza hapa umtembelee na kumpa maneno mawili matatu ya kishikaji.
Tue 20 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Mjadala huu huwa unazuka na kutokomea. Jeff ameuanzisha tena. Bonyeza hapa usome aliyoandika. Pia tazama sehemu ya maoni. Soma changamoto ya Mwaipopo (ambaye nasikia ataingia rasmi kwenye blogu hivi karibuni). Da Mija akapokea wito wa Jeff. Anapendekeza neno Ngwanga litumike badala ya neno “blogu” ambalo baadhi wanaona kuwa neno hili tumelichukua kutokana na uvivu tu. Yaani tumechukua neno la Kiingereza “blog” tukaongeza “u.” Bonyeza hapa. Pia tazama maoni yaliyotolewa hapo kwa Da Mija. Unaweza kuchangia hapo kutokana na pendekezo la Da Mija.
Tue 20 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Kama unatazama blogu za Kiswahili kwa karibu, utagundua kuwa kuna jambo moja zuri sana linajitokeza. Blogu zinakuwa sio tu eneo la kujadili masuala ya kisiasa, kiutamaduni, na kijamii bali pia ukumbi wa kutoa kazi za fasihi andishi: riwaya, tamthilia, visa, mashairi, n.k. Hili ni jambo kubwa sana. Nimelizungumzia majuzi kwenye muhtasari niliouandika kwenye blogu ya Sauti za Dunia.
Bonyeza hapa uusome. Katika muhtasari huo nilisema hivi (kwa Kiingereza):
It is a common practice among Swahili poets to challenge each other using various poetry techniques and deep Swahili. For example, one poet writes a poem and another poet responds to that poem through a poem of his/her own. This practice has long been associated with Uhuru, the only Tanzanian newspaper that for many years provided a space for Swahili poets to publish their work. Two poet bloggers, Kasri la Mwanazuo and Fasihi za Ufasaha are moving this practice to cyberspace through their blogs.
This is a particularly interesting moment in the Kiswahili blogosphere. The possibility that blogging can become one of the ways in which Tanzanian writers and poets can bypass problems related to cost of publication and economics of distribution is an exciting one. For example, because of limited distribution, Swahili novels are mostly read in Tanzania and Kenya. If Swahili literary works are available online in digital format, making them globally accessible, Swahili speakers in Oman, India, the US, China, Mexico, South Africa and elsewhere will be able to read them. Utilizing this opportunity, Kasri la Mwanazuo is planning on releasing his first novel on his blog.
Utaona kuwa katika muhtasari huo ninasema kuwa kazi za fasihi andishi hata fasihi simulizi za Kiswahili (tukianza kutumia blogu za sauti [podikasiti]) ambazo kawaida husomwa Afrika Mashariki tu (hasa nchi mbili, Kenya na Tanzania) zinaweza kuanza kusomwa na wasomaji zaidi ya milioni 100 wa Kiswahili ambao wametapakaa sehemu mbalimbali duniani. Kwa kuwa mzungumza Kiswahili anayependa fasihi ya Kiswahili anayeishi India au Oman hawezi kununua vitabu vilivyoko pale TPH, mtaa wa Samora, kazi hizi za fasihi zikipatikana katika mtandao wa Intaneti (kupitia blogu, podikasiti, fasihi pepe, n.k.) mtu huyo ataweza kujisomea. Kwa maana hiyo fasihi ya Kiswahili haitakuwa ni fasihi ya kikanda bali ya dunia. Tunajua kuwa wachapishaji wetu wanakabiliwa na tatizo la mtaji wa kuweza kusambaza kazi za Kiswahili duniani.
Jambo jingine ni kuwa kuna watu wengi ambao ni watunzi wazuri sana wa riwaya, mashairi, au tamthilia lakini kutokana na gharama kubwa za kuchapa vitabu, kazi zao zinabaki kwenye shajara au madafatari yao binafsi. Wanazisoma wenyewe. Teknolojia ya blogu inaweza kusaidia, kwa kiasi fulani, baadhi ya watunzi hawa kwa kuwapa eneo la kuchapa kazi zao kwenye mtandao wa Intaneti. Hata kama mtunzi mwenyewe hana utaalamu wa masuala ya kompyuta anaweza kutumia ndugu au marafiki au wakereketwa ili waweke kazi zake mtandaoni.
Upo pia uwezekano wa kazi za fasihi zilizotolewa mtandaoni kutolewa katika muundo wa vitabu kwa ajili ya wasomaji wasio na mtandao wa Intaneti au wanaotaka kusoma kazi hizo katika vitabu. Kwa mfano, mwablogu Salam Pax wa Iraki amechapisha yaliyoko kwenye blogu yake kwenye kitabu ambacho kimepata umaarufu sana.
Bonyeza hapa uone kitabu chake na
hapa ili usome habari zake.
Kama ulifuatilia tuzo, ambayo niliitangaza hapa, ya blogu duniani utakumbuka kuwa aliyeshinda (ukiacha blogu ya Sauti za Dunia ambayo ilishinda kwa upande wa Kiingereza) kwa blogu za lugha zote zilizoshiriki ni blogu ya kifasihi ya Kihispania ambayo inaelezea maisha ya familia moja. Blogu hiyo inaitwa, Heshima Kidogo, Mimi ni Mama Yako.
Bonyeza hapa uone tangazo la kushinda kwake.
Bonyeza hapa uone blogu yenyewe.
Kwahiyo kama mnafahamu watunzi ambao wanatafuta njia ya kuweka kazi zao mikononi mwa wasomaji ila hawana namna, waelezeni kuwa blogu ni moja ya njia ambazo hazihitaji gharama kubwa. Sio mwanzo na mwisho ila ni moja ya upenyo.
Ninawaombeni pia mufuatilie kazi zilizopo hivi sasa mtandaoni za fasihi. Majuzi nilimtangaza mwanablogu mshairi Ustaadh, Rashid Mkwinda(ngominenga)(Malenga wa Kilwa). Nikamrushia dongo mshairi mwingine, Makene, kuwa akae chonjo.
Bonyeza hapa usome tangazo hilo. Makene, mzee wa Kasri la Mwanzuo, akajibu kwa mashairi mawili ya haraka haraka katika sehemu ya maoni. Nami nikaweka shairi fupi la Ustaadh Mkwinda jibu kwa Makene na mimi.
Bonyeza hapa usome mashairi hayo. Makene hakuishia hapo, akakaa chini na kumkaribisha Mkwinda kwa shairi.
Bofya hapa usome shairi hilo. Mkwinda naye akamwandikia Makene.
Bofya hapa na pia tazama sehemu ya maoni kwa mashairi la Makene. Mkwinda akaandika pia shairi jingine kwa Makene na mimi.
Bofya hapa. Nadhani nitamjibu Mkwinda kwa Kichagga!
Mkwinda kaandika shairi, baada ya mchezo wa kuigiza wa uchaguzi Tanzania, akiuliza kama ulikuwa ni uchaguzi au uchakuzi.
Lisome hapa. Makene kabla
hajaondoka kwenye Kanada aliandika shairi la salamu kwa wanablogu wa Kiswahili.
Bofya hapa ulione. Kinachotokea katika mashairi haya ya nipe nikupe ni sawa na hali ambayo imekuwepo kwa miaka mingi katika ukurasa wa mashairi wa gazeti la CCM, Uhuru.
Bonyeza hapa uone ukurasa huo, Uga wa Malenga.
Huko nyuma
Mwandani aliwahi kuandika mshairi kadhaa (ninatafuta viungo vyake…Tunga unavyo haraka haraka unipatie?). Ukiacha mashairi kuna kazi nyingine za kusisimua kama aliyoandika Jeff hivi karibuni. Kazi yake hii: Nyerere Yuko Wapi?, nimeipenda sana. Isome kwa
kubonyeza hapa. Makene naye ana kazi yake iitwayo Safari ya Mashua.
Bonyeza hapa kwa sehemu ya kwanza na
hapa kwa sehemu ya pili. Jana ameandika kisa kilichomtokea ndotoni.
Bofya hapa. Kasri la Mwanazuo tuliongea siku si nyingi juu ya kufungua ukurasa wa Fasihi Pepe za Kiswahili (Makene, sijasahau nilichokuahidi!).
Kwangu mimi mambo haya ni kile kitu ninachopenda kuita, “ishara ndogo za mambo makubwa.” Hizi ni ishara ndogo za mambo makubwa yanayokuja mbeleni. Ninatazama mambo haya ninatabasamu. Tunafanya jambo moja kubwa sana bila wenyewe kujua. Au pengine tunajua…
Sat 17 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni

Samaki jamani lazima umkunje mapema mapema. Ndio anavyokunjwa mwanamapinduzi wa kesho, Ukweli Ndesanjo, kama unavyomuona hapo kwenye picha ya juu. Hiyo ilikuwa ni Oktoba mwaka huu wakati wa maandamano ya Vuguvugu la Mamilioni na Zaidi. Hapo anamtazana na kumshangilia mwanamuziki aliyehamia Marekani toka Haiti, Jean Wycleaf. Picha ya chini yakea ndio Wycleaf mwenyewe anaonekana kwenye luninga (iliyokuwa ikirusha matangazo kwa walioko mbali na jukwaa kuu). Ingawa anamshangilia Wycleaf kwa furaha, Ukweli anawapenda zaidi Fela Kuti na Bob Marley. Masikini, hatakaa awaone wakitumbuiza hadharani.
Sat 17 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni

Naendelea kuweka picha zaidi nilizopiga wakati wa maandamano ya
Vuguvugu la Watu Milioni na Zaidi kule Washington, DC, Oktoba mwaka huu. Hawa ni wanachama wa kundi la New Black Panther Party (tofauti na lile kundi la wazee wengine wa shoka la Black Panther). Hapa unaona mwenyewe wanaume wa shoka wako tayari tayari kwa lolote lile. Joji Kichaka, we endelea kuleta za kuleta…
Picha hiyo hapo chini ndio kiongozi wao, Malik Zulu Shabazz. Huyu bwana analindwa na utitiri wa wanaume wa shoka sijapata kuona.
Bonyeza hapa usome kwa kifupi juu yao.
Fri 16 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni

Wanaume hawa wa shoka ni akina nani? Hawa ni walinzi wa kiongozi wa kundi la New Black Panther Party, Malik Zulu Shabazz. Malik ambaye ni mwanasheria ni machachari sana kwa siasa zake kali ziilizojengwa juu ya falsafa za akina Malcolm X, Marcus Garvey, Kwame Toure, n.k. Malik Zulu Shabazz ndiye aliyeko mbele katika picha hii. Picha hii niliipiga siku ya maandamano ya Vuguvugu la Watu Zaidi ya Milioni, Washington, DC.
Fri 16 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni

Hii picha niliipiga wakati wa maandamano ya Vuguvugu la Mamilioni na Zaidi kule Washington, DC. Kama unakumbuka, mwimbaji Kanye West alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha kwa ajili ya waliathirika na Katrina alisema kuwa Joji Kichaka hana habari na watu weusi. Swali kwenye picha hiyo linatokana na kauli hiyo ya Kanye West.
Wed 14 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Mark Msaki ni mwanafunzi wa udakitari katika chuo kikuu cha Kwa Zulu Natal kule Afrika Kusini. Amesema kuwa ingawa yeye sio mwandishi wa habari, ana nasaha na maoni ambayo anapenda kuyatoa hadharani. Na chombo ambacho anamependa kukitumia kufanya hilo ni blogu. Kaanzisha blogu yake ambayo ameiita Kurunzi.
Bonyeza hapa usome na kumkaribisha.
Tue 13 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Majuzi niliandika kuhusu Tuzo ya Haki za Binadamu ya Majimaji aliyopewa Jaji James Mwalusanya. Kama hukusoma niliyoandika,
bonyeza hapa usome. Tuzo hiyo ilitolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Niliwapongeza kwa kumpa Jaji Mwalusanya tuzo hiyo kutokana na mchango wake katika ujenzi wa demokrasia Tanzania kupitia maandiko yake na hukumu mbalimbali ambazo amewahi kutoa.
Lakini nikawanyooshea kidole wanaharakati hawa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kosa ambalo linatokana na ugonjwa ambao inaelekea ni mbaya kuliko ambavyo wengi tunadhani. Ugonjwa huu ni ule unaotufanya kutumia lugha ya kiingereza hata pale ambapo walengwa wetu lugha yao kuu ni Kiswahili. Tazama majina ya mashirika yasio ya kiserikali, vyama vya upinzani, kampuni za kibiashara, maduka, baa, bendi, na hata vikundi vya utamaduni. Utakuta majina ya kiingereza ndio yanaonekana kuwa ni bora zaidi.
Achilia mbali majina, tuje kwenye tovuti. Nimeongelea kwa muda mrefu kuhusu tovuti ya ikulu, waziri mkuu, bunge, tume ya uchaguzi, mwanablogu mmoja (sijui alikuwa ni Nkya au Egidio) akatukumbusha pia tovuti ya Makumbusho ya Taifa, n.k zina taarifa muhimu kwa Watanzania kwa lugha ya kiingereza. Niliwahi kusema kuwa iwapo Rais akiongea na Watanzania anatumia kiingereza basi sitalalamika iwapo tovuti ya ikulu ni ya kiingereza. Iwapo wabunge ni wawakilishi wa wananchi ambao lugha wanayotumia asubuhi, mchana, na jioni ni Kiswahili, kwanini tovuti ya bunge lao na miswada ya sheria iwe ni ya kiingereza? Kama huu sio ugonjwa ni nini?
Sasa nilipokuwa naongelea kuhusu Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, nikauliza: kuna sababu gani ya tovuti ya kituo hiki kuwa ya kiingereza wakati ambapo wanatuambia kuwa lengo lao kuu ni kuwawezesha Watanzania wasiojiweza kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, na kiroho kwa kuwapa mafunzo ya haki za binadamu na kuwapatia msaada wa kisheria? Kama nia ya kituo hiki ni kuwasaidia hao Watanzania, kwanini watumie lugha ya watu wengine na sio lugha wanayotumia Watanzania masaa 24?
Soma mwenye lengo kuu la kituo hiki (kwa kiingereza). Nimetoa kwenye tovuti yao (wino mzito nimeuweka mwenyewe):
The primary task of the Legal and Human Rights Centre is to create legal and human rights empowerment amongst the socially, economically, culturally and spiritually disadvantaged and marginalized groups within the Tanzania society through legal and human rights training, provision of legal aid, information generation and dissemination through publications and radio programmes, research on legal and human rights issues and networking and alliance building with other institutions which share this mission.
Nilipoandika kuhusu hili,
mwanablogu Jeff, akatoa maoni yake akitaka kujua kama “binadamu” wanaozungumziwa na kituo hiki ni pamoja na babu na bibi yake kule Kilimanjaro. Alisema, “Huenda wanadamu wanaoongelewa hapa sio babu yangu na bibi yangu kule Kilimanjaro.”Wanadamu” hawa nadhani ni wale ambao tayari wanazijua baadhi ya haki zao za msingi.Kituo kinafanya kuwakumbusha tu pale wanapoonekana kuzisahau.”
Mwanablogu
Da Mija akatoa wazo: “Mimi naona tuanze kuwaandikia moja kwa moja kuwauliza kwanini wanatumia kiingereza kuwaandikia waswahili, je wanajua madhara yake?”
Suala hili la lugha wengine wanaweza kuona kuwa ni jambo dogo sana. Hapana. Kama ambavyo tovuti ya shirika lisilo la kiserikali Uingereza haitakuwa ya Kiswahili maana hawatumii lugha hii ndivyo hivyo tunaamini kuwa tovuti ambayo inatoa taarifa, elimu, na maarifa kwa Watanzania haina haja ya kuwa ya kiingereza. Hili ni suala la kujikwamua. Kama tovuti hizi zinatengenezwa kwa ajili ya wafadhili, tuambiwe. Ila kama zinatengezwa kwa ajili ya kutoa taarifa na elimu kwa Watanzania, basi hakuna sababu ya kukopa lugha ambayo wengi tunaielewa kijuujuu. Ukitaka kujua lugha gani uitumie unapotaka kutawanya habari, taarifa, elimu, n.k. kwa Watanzania, nenda kwenye vituo vya mabasi, uwanja wa mpira, baa, saluni, vijiwe vya kahawa, mashambani, kampeni za kisiasa, n.k., tazama Watanzania wanatumia lugha gani sehemu hizo.
Kama Da Mija alivyosema, tunapaswa kuwaambia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kuwa ni busara na heshima kwa taifa na utamaduni kujenga tovuti yao kwa Kiswahili. Haki za binadamu wanazotetea zinajumuisha pia haki za kitamaduni. Haki za kuwa na utamaduni wako, kuujua, na kuuheshimu.
Bonyeza hapa uone tovuti yao. Anuani yao ya barua pepe ni hii: lhrc@humanrights.or.tz
Na simu yao ni hii: 2773038, 277 3048
Bonyeza hapa usome moja ya makala zilizowahi kuandika kuhusu suala la kimombo kwenye tovuti za umma.
Tue 13 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Mkutano wenyewe ulifanyika tarehe 10 Desemba. Wanablogu toka pande mbalimbali za dunia walikutana katika makao makuu ya shirika la habari la Reuters (wakiwemo Paul Kihwelo wa kitivo cha sheria
Chuo Kikuu Huria Tanzania, ambaye blogu yake itakuwa hewani karibuni na
Fatma Karama). Mambo kadhaa yalijitokeza ambayo yanatuhusu wanablogu wa Kiswahili. Mawili makuu: 1. Jinsi gani ya kuongeza idadi ya blogu? 2. Je
mradi wa Sauti za Dunia ufanye nini kuhusu blogu ambazo sio za kiingereza?
Ningependa tutazame hayo masuala mawili na kujadiliana kitu/mambo gani tunaweza kufanya. Tayari nimejadiliana kwa kifupi na Jeff na Paul. Mawazo yetu wote yanahitajika. Jambo mojawapo ambalo Jeff nami tumeligusia ni kuwa tunaweza kupeana changamoto: kila mwanablogu alete wanablogu wawili wapya…wawili tu…kwenye blogu za Kiswahili. Paul Kihwelo amezungumzia umuhimu wa sisi kukutana. Alizungumzia jambo hili kwa kirefu alipokutana na
Ethan Zuckerman, mmoja wa waanzilishi wa Sauti za Dunia. Na anaporudi Tanzania atalifanyia kazi.
Wakati huo huo kuna “wiki” ambayo imeundwa kwa ajili ya kubunga bongo na kukusanya mawazo kuhusu nini cha kufanya ili kuimarisha mradi wa Sauti za Dunia na kupanua wigo wa blogu duniani. Unaweza kuchangia mawazo yako. Kuhusu suala la lugha na tafsiri
bonyeza hapa. Kuhusu suala la kuongeza na kuvutia watu zaidi katika ulimwengu wa blogu,
bonyeza hapa. Ukitaka kuona “wiki” nzima
bonyeza hapa.
**Wiki: wiki ni aina ya teknolojia ambayo inaruhusu ukurasa wa kwenye tovuti kuhaririwa au kuandikwa na mtu yeyote bila haja ya kuwa na neno la siri au ufahamu wa lugha ya kompyuta kama “html.” Teknolojia hii ndio tunayotumia katika kutengeneza kamusi elezo ya Kiswahili.
Ukibonyeza hapa utaiona kamusi hiyo na unaweza kushiriki kuiandika. Pia kwa wale ambao nimewahi kuwagusia kuhusu mradi ule ninaosimamia wa kuandika katiba kwa kutumia “wiki,” basi teknolojia yenyewe ni kama hii.
Rebecca MacKinnon, mmoja wa waanzilishi wa mradi wa Sauti za Dunia, ameandika muhtasari mzuri sana wa mkutano huo wa wanablogu. Tafadhali ukiwa na muda usome ili tusije kupitwa na mazungumzo yanayoendelea duniani kuhusu blogu.
Bofya hapa usome muhtasari huo.
Tue 13 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni

Na huyu ndiye mwanablogu Ory wa blogu ya
Kenyan Pundit akiwa kwenye mkutano wa wanablogu uliomalizika mwishoni mwa wiki nchini Uingereza. Ory ni kati ya wanablogu ambao kupitia blogu zao wanilitia hamasa ya kuanza kublogu. Moja ya kazi kubwa ambayo ameifanya karibuni kupitia blogu yake ni kuripoti zoezi la
kura ya maoni ya katiba mpya nchini
Kenya.
Ukitaka picha hiyo iwe kubwa zaidi, bonyeza juu yake.
Tue 13 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Fide alituma ujumbe wa barua pepe kwa watu kadhaa hivi karibuni akihoji mantiki ya kumtaka Mola awabariki viongozi wa Afrika. Nilipenda sana ujumbe wake ule nikaufanya kuwa ni sehemu ya makala yangu ya jumapili iliyopita katika gazeti la Mwananchi, nchini Tanzania. Katika makala ile nilijadili kwa kifupi sana jambo ambalo msomaji na rafiki yangu, Frank Massawe, ameuliza hapa kwenye blogu. Katika makala hiyo nimegusia pia tukio tulilofanya jeshini (mwanablogu Nkya akiwemo) la kuchora mstari ardhini na kutamka afande mmoja pale Ruvu aruke huo mstari kama ni mwanaume!
Ninaiweka makala hiyo hapa na pia katika kona ya makala zangu, upande wa kuume wa blogu hii, chini ya picha yangu. Bonyeza hapa uisome.
Tue 13 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni
Majuzi nilitangaza kuwa kuna mwanablogu mpya aliyekuja kwa nguvu na kutishia wale wote wanaotaka kujichukulia cheo cha u-malenga. Nikampiga dongo
Kasri La Mwanazuo. Kama hukusoma tangazo hilo lisome kwa
kubofya hapa.
Basi Kasri hakusita, akarudisha dongo kwangu na
Mkwinda kwa shairi hili hapo chini:
Ndesanjo acha udhia, kidole ninyooshea
Gange umemgusia, vitisho kumtupia
Kasri limechimbia, mizizi imarishia
Itakuwa songombingo, kutaka libomolea.
Wazo la kulijengea, asili mbali anzia
Nikali bado tambua, Baba Mama ungania
Pumzi ilinambia, Kasri kwenda jengea,
Itakuwa songombingo, kutaka libomolea.
Mkwinda mwana fikia, Kasirini jifunzia
Fikira kutafunia, Fasihi kufahasia
Kisha weledi jazia, gange bora patilia
Itakuwa songombingo, Kasri libomolea.
Ndesanjo nanyamazia, karatasi kushikia
Kesho napaswa ketia, mtihani kufanyia
Nikisha kumalizia, Mkwinda ntamchapia
Kasri jumba la ghali, kicheko kubomolea!
*********************************************
Hakuishia hapo. Baada ya kuona Mkwinda kawa kimya akafyatua shairi jingine:
Sina ajizi fyatua, bomu nilolizindua
Awali nilidhania, muda bado kufikia
Kumbe mwanichungulia, kwa lengo kunilipua
Nataja hali hatari, Kasri kulilindia.
Ugaidi sikujua, waweza kunifikia
Hima sipendi jutia, tahadhali naanzia
Ijapo sitasemea, Walinzi naandalia
Hii ni hali hatari, Kasirini sogelea.
Nilisema nakimbia, kurasa kutazamia
Bado sijamalizia, ni mbili zilobakia
Moja itashika tama, leo napoifutia
Nikirudi hadithia, Kasri mtazamia.
Mkwinda u wapi kaka, utata umezulia
Umechupa kwa haraka, kisa watu nitishia
Tambua sijatishika, cheche ninakutemea
Kama wataka ingia, balaghashia vulia.
********************************************************
Mkwinda akasema isiwe tabu. Akaandika shairi fupi akitutisha kwa kalamu yake (mimi na Makene). Hili hapa:
Ya mja ada unene, nimepata makene,
Katu si vyema ujivune,kauli pasi mapene,
Kalamu iwe ni nene,andiko lionekane,
Ndesanjo nawe makene, kalamu vyema tumieni.
******************************
Sat 10 Dec 2005
Na , Maudhui: Uncategorized
Toa Maoni [7]
Kasri la Mwanazuo kaa chonjo. Rashidi Mkwinda ni mwanablogu mpya wa Kiswahili ambaye anapenda sana lugha ya Kiswahili. Na pia ni mshairi anayependa kujibu wasomaji wake kwa mashairi. Tazama shairi lake hili:
Kilo chako ndicho, hicho sitarijie kisicho,
Katu sikodoe macho,ukadhani ndicho hicho,
Kwa macho utamanicho, kitakutoboa macho,
Epuka njia za chocho,si maisha pochopocho.
Blogu ya Mkwinda inaitwa Fasihi za Ufasaha. Bofya hapa umtembelee na pia kumkaribisha uwanjani.
— Next Page »