Doug Clark ni mwandishi wa gazeti la News and Record. Gazeti hili liko mbele sana katika masuala ya blogu na uandishi wa umma. Mtoto wa Doug Clark anaishi Mwanza, Tanzania. Hivi majuzi Doug alimtembelea mwanae. Soma aliyoandika kuhusu Mwanza na hasa kuhusu utendaji wa kazi wa polisi jijini Mwanza. Bofya hapa.
June 2006
Thu 29 Jun 2006
Tanzania kupitia jicho la mwanablogu Mmarekani
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: wanablogu , MengineyoToa Maoni [14]
Thu 29 Jun 2006
Nimemaliza kutembelea blogu mpya ya ndugu Simba wa kampuni ya vitabu ya Mkuki na Nyota. Msabahi kwa kubonyeza hapa. Simba alikunwa na mfululizo wa makala kuhusu blogu nilizoandika katika gazeti la Mwananchi. Dakika hii ninasikiliza kibao murua kabisa cha Mlimani Park Marquis Orijino, enzi hizo wakiwa na mtindo wa Zembwela. Kibao hicho ni kile cha Karubandika (ambaye inasemekana anaombaomba fegi na unywaji baa). Kibao hicho nimekifuma toka kwa Maitha wa Mawazo na Mawaidha, ambaye naye amekifuma toka kwa Ntwiga. Kisikilize hapa. Enzi zile kuna watu walikuwa wanapanga sauti kwenye ile safu ya waimbaji kama vile wamechanjiwa. Halafu magitaa yalikuwa yakipigwa kwa utamu wa aina yake. Sikiliza mwenyewe uniambie. Iwapo wewe ni mpenzi wa Disco Chakakacha, nimekuta Maitha kaweka kiungo ambacho ukikifuata unaweza kuwasikiliza Mombasa Roots. Bofya hapa.
Wakati huo huo unaambiwa kuwa pamoja na timu ya Brazili kuendelea kuzoa ushindi kwenye kombe la dunia, wapenzi wa soka Brazili (inamaanisha Wabrazili wote!) hawafurahishwi na uchezaji wa timu hiyo iliyotutia huzuni Waafrika baada ya kutuchabanga mabao matatu. Hata hivyo chenga tuliwala. Ghana ilimiliki mpira asilimia 53 na ilivurumisha makombora 17 golini wakati Brazili ilivurumisha makombora 10. Soma habari kamili hapa.
Wed 28 Jun 2006
Wataalamu na blogu zao + luninga ya Tanzania kwenye Intaneti
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , tanzaniaToa Maoni [1]
Hizi ni habari njema. Mwanablogu mpya Alexander Mwalyoyo, ambaye tayari ametangazwa na John Mwaipopo, anaendeleza njia iliyoanzishwa na mwanablogu Hector. Njia hii ni ile ya wanablogu wanaoblogu masuala yanayohusu fani au utaalamu wao. Tofauti na wanablogu ambao tunaandika juu ya chochote kinachoingia katika anga zetu (siasa, michezo, teknolojia, utamaduni, fasihi, n.k.) Alexander ameamua kutumia blogu yake kutuelimisha kuhusu mazingira. Naamini kuwa tutaelimika kiasi cha kupanua uelewa wetu wa mazingira ambao mara nyingi huwa unaanzia na kuishia kwenye kupanda miti. Hector Mongi yeye anaandika kuhusu masuala ya kilimo. Bonyeza hapa umtazame Alexander na hapa umsome Hector. Wakati huo huo: unaweza kutazama televisheni ya kituo cha Star TV ya Tanzania kupitia kwenye Intaneti. Bonyeza hapa.
Sun 25 Jun 2006
Mexico: “Viwanja vya Jangwani” vimehamia kwenye Intaneti
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , demokrasiaToa Maoni
Uchaguzi wa urasi ulipofanyika nchini Mexico miaka sita iliyopita, kulikuwa na wakazi milioni tatu wa nchi hiyo wanaotumia Intaneti. Hivi sasa wakazi milioni 20 wanatumia Intaneti. Kutokana na ukweli huo na uelewa wa mahusiano ya teknolojia mpya na jamii, kampeni za urais mwaka huu zimeongeza eneo la harakati. “Viwanja vya Jangwani” vya Mexico sio vile tu vilivyopo katika dunia ya udongo na mawe bali pia vile vilivyopo kwenye Intaneti. Sio vile tunavyovitembelea kwa miguu na magari bali vile tunavyovitembelea kwa vidole kwa kutumia baobonye (keyboard) na puku/kipanya (mouse) kwa kubonyeza/kubofya na kurambaza(surf)). Bonyeza hapa usome kwa undani mabadiliko haya ya mbinu za kupiga kampeni yanayoletwa na teknolojia mpya za habari na mawasiliano.
Sun 25 Jun 2006
Wikimania 2006 na skolashipu
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: wikipedia , skolashipu , mikutanoToa Maoni [6]
Tarehe 4-6 mwezi wa nane kutakuwa na mkutano wa pili wa kila mwaka wa wana jumuiya wa Wikipedia na miradi mingine iliyo chini ya Wikimedia Foundation, Wikimania 2006. Mkutano wa kwanza ulifanyika nchini Ujerumani mwaka jana, Wikimania 2005. Wikimania 2006 utafanyika katika chuo kikuu cha Harvard.
Sun 18 Jun 2006
Blogu zilipoingia kwenye ulimwengu wa teknolojia watu wengi walidhani kuwa ujio wake si chochote na blogu hazitaleta mabadiliko yoyote katika nyanja ya habari na hata siasa na utamaduni. Wakadhani kuwa blogu ni upepo unaokuja na utapita. Waliokuwa wanadhani hivi wameshatambua kuwa walikosea. Walishindwa kujua thamani na nguvu za teknolojia hii na jinsi ambavyo raia kama mimi na wewe tutakata shauri na kuanza kuitumia kama zana ya mapambano.
Sun 18 Jun 2006
Siasa ndio hivyo tena…si hasa! Uchumi nao…tumeamua kuwarudishia wakoloni baada ya kuwabatiza jina jipya. Amani iliota miguu toka zamani. Elimu…sifuri. Afya…sifuri. Tazama aibu hii kwenye kombe la dunia. Wakati nchi zinaweka rekodi muhimu kama vile kutofungwa katika mechi za kimataifa, kuwa na wafungaji bora duniani, n.k. sisi tunakaribia kuweka rekodi ambayo itakuwa ndio mara ya kwanza katika miaka 76 ya kombe la dunia. Bonyeza hapa. Kabla ya hapo kulikuwa na kasheshe hii hapa.
Sat 17 Jun 2006
Toka juu ya miti hadi kublogu, Africa Unite, na kadhalika
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: Mengineyo , video , sokaToa Maoni [7]
Inaelekea kama nimetupa mkono blogu hii. Unajua wakati kombe la dunia linachezwa kule Ujeremani, hapa wengine tuko kazini. Hivyo, unapotoka kazini unakwenda kutazama mechi zilizorekodiwa. Hivyo ninajitahidi sana kukaa mbali na chombo chochote cha habari kinachoweza kunitaarifu matokeo hivyo kuharibu ladha ya kutazama mechi zenyewe.
Wakati najiandaa kutazama mechi ya Ghana na Czech (matokeo ya Ivory Coast yamenitia huzuni kubwa) nimeona nikupe mambo mawili. Jambo la kwanza ni picha inayoonyesha jinsi ambavyo binadamu tulivyotokea kuishi mitini, tukiwa na mkia hadi tumefikia hatua ya kuwa wanablogu! Bonyeza hapa.
Jambo la pili linahusu muungano wa Afrika. Sijui kama muungano wa Afrika utabaki kuwa ni ndoto tu. Tazama ujumbe ulioko kwenye video utakayoipata kwa kubonyeza hapa.
Sat 10 Jun 2006
Sio siri. Wamenifurahisha. Walivyowakaba koo Waswidi na spidi na chenga zao. Ila heshima zote ni kwa golikipa Shaka Hislop. Unadhani mtu anapokuwa na jina “Shaka” atakuwa mtu wa kuchezea? Acha tu. Ninawazungumzia Trinidad na Tobago. Mtazame Shaka mwenyewe akiwa kazini. Kipenga cha mwisho kinalia matokeo ndio haya…Waswidi vichwa chini.
Tue 6 Jun 2006
Utabiri wa tarakilishi na ule wa wazee wa Bwagamoyo upi mkali?
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: sokaToa Maoni [2]
Unadhani kuwa Brazili itachukua kombe la dunia? Jamaa wa Electronic Arts wanakwambia kuwa umepotea njia. Jamaa hawa wa Electronic Arts, wakitumia uchawi wa kompyuta, wanakwambia kuwa timu itakayochukua ubingwa ni…bonyeza hapa.
Sun 4 Jun 2006
Nini cha kufanya kuondoa ufisadi?
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: Wapi tunakwenda? , tanzania , videoToa Maoni [3]
(bonyeza juu ya picha hapo juu utazame video)
Video hii nimeiweka hapa kutokana na makala kali iliyoko katika Kasri la Mwanazuo kuhusu wizi wa mchana wa mali za umma unaofanywa na watu wanaoitwa “viongozi” nchini Tanzania. Baada ya kusoma makala hiyo unatakiwa kufanya jambo moja kama raia wa Tanzania na binadamu. Kwahiyo jambo la kwanza soma makala hiyo kwa kubonyeza hapa. Unachotakiwa kufanya kipo katika video niliyoiweka hapa. Bonyeza juu ya picha hapo juu ili uitazame video yenyewe. Au unaweza pia kubonyeza hapa. Ujumbe ulioko katika video hiyo usiuchukulie kwa mzaha.
Sun 4 Jun 2006
Duniani kuna mambo. Tazama video hii hapa kisha uniambie mwenyewe (bonyeza hapa). Utabaki mdomo wazi. Halafu kuna video (ni ndefu kidogo na utamu wake na utamu wake hauko mwanzoni bali baada ya dakika kadhaa) inayosisitiza madai kuwa yaliyotokea Septemba 11, 2001 nchini Marekani ni hujuma kali inayohusisha sirikali ya Joji Kichaka na wenzie. Bonyeza hapa utazame video yenyewe.




