Inawezekana kuwa wewe ni mtunzi wa riwaya na mashairi kama Boniphace na Maitha au mtunzi wa mashairi kama Rashid na Mwandani. Au pengine wewe ni mtu unayekusanya habari za wanawake muhimu, wanawake wa shoka, kama afanyavyo Da Mija. Au wewe ni mwandishi wa makala kama Jeff. Au pengine wewe ni mchambuzi wa masuala ya uchumi, siasa, na jamii kama Idya. Basi ukafika wakati ukataka kuchapa kazi zako katika kitabu, lakini katika pitapita zako kwa wachapishaji ukakuta kuwa kuna usumbufu, ukiritimba na mauzauza ya kila aina. Inawezekana kuwa kazi zako ni zile zisemazo kuwa “mfalme yu uchi wa mnyama,” wachapishaji wakaogopa kuchapa kazi zako. Wakaogopa kuchezea moto. Inawezekana pia umezuiwa na gharama kubwa za kuchapisha vitabu. (bonyeza hapo chini uendelee kusoma habari hii…). (more…)
July 2006
Wed 19 Jul 2006
Sun 16 Jul 2006
Mjadala Intanetini kuhusu teknolojia na biashara Afrika
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , afrikaToa Maoni [2]
Christine Bowers wa PSD Blog kanitaarifu kuhusu mjadala unaofanyika hivi sasa hadi mwisho wa mwezi huu kuhusu masuala ya teknolojia na biashara Afrika. Mjadala huo ambao unafanyika Intenetini unaratibiwa na jamaa watatu, kama kawaida hakuna aliyetoka Afrika! Bonyeza hapa kama unapenda kushiriki au kusoma mawazo ya wengine ili kupanua mtazamo wako kuhusu masuala ya teknolojia na maendeleo.
Sun 16 Jul 2006
Sijui wewe una mawazo gani kuhusu kazi za Benki ya Dunia (kwa jina jingine, Benki ya Ulaya na Marekani). Kama huna ubaya na hawa jamaa na unapenda kufanya nao kazi, basi kuna nafasi ya kazi. Nafasi yenyewe ni kwa vijana waliotoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Nafasi hii iko chini ya mpango wa benki hii uitwao The Junior Professionals Program for Afro-Descendants (JPPAD). Ili maombi yako yaweze kufikiriwa lazima uwe na miaka 35 au chini ya hapo na pia uwe tayari una digrii mbili. Bonyeza hapa usome mwenyewe kuhusu nafasi hii. Huenda tukijiingiza katika benki hii ya wazungu inayotukopesha Waafrika kwa masharti magumu tutaweza kusaidia juhudi za kubadili sera zake. Au labda ndio tutakuwa tunajiuza kabisa. Sijui. Nkya, sijui una mawazo gani.
Wed 12 Jul 2006
Mwanablogu aachiwa huru + Siku ya Blogu Duniani
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , wanablogu , demokrasiaToa Maoni [3]
Kati ya kampeni kubwa ambayo imewahi kuendeshwa na wanablogu ni ile ya kutaka serikali ya China kumwachilia huru mwanablogu Hao Wu. Hao Wu ni mwanablogu toka China aliyekuwa akiishia Marekani na kisha kurudi China kwa nia ya kutengeneza filamu kuhusu masuala ya dini nchini humo. Blogu yake inaitwa Beijing Or Bust. Februari 22 mwaka huu serikali ya nchi hiyo ikamtia ndani. Hapo kampeni ikaanza. Ikaanzishwa blogu maalum kwa ajili yake, bonyeza hapa. Dada yake naye akaanzisha blogu kwa ajili ya kampeni ya kutaka kaka mtu aachiliwe. Bonyeza hapa uone blogu yake ya Kichina na hapa kwa tafsiri ya kiinglishi.
Sun 9 Jul 2006
Ukurasa wa blogu zetu+blogu mpya + chapati maji
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , wanabloguToa Maoni [1]
Wakati kasi ya blogu za Kiswahili na pia za kiingereza za Watanzania inaongezeka napenda kukumbusha umuhimu wa kuorodhesha blogu hizi katika ukurasa huria (wiki) wa mradi wa Global Voices. Ukurasa huu unaorodhesha blogu kwa kila nchi. Ukitazama ukurasa wa bara la Afrika, bonyeza hapa, utaona kuwa wanablogu wa Tanzania ndio tuko mstari wa mbele katika kuorodhesha blogu zetu. Ni jambo zuri sana iwapo tunaweza kuwa na ukurasa mmoja wenye blogu zetu zote. Faida za kuwa na ukurasa mmoja wenye orodha ya blogu zetu ni nyingi. Kwa mfano, iwapo kuna mtu anafanya utafiti juu ya blogu zetu, badala ya kuhaha huku na kule kuzitafuta anaweza kwenda kwenye ukurasa huo na kuziona zote. Pia kwa wale wanablogu tunaopenda kufuatilia blogu mpya kuna wakati unaweza kupitwa na blogu mpya. Iwapo kila blogu mpya itakuwa inaorodheshwa kwenye ukurasa huu, hofu ya kupitwa na blogu mpya inatoweka.



