Haya, siku ya blogu duniani ni leo tarehe 31, Agosti. Kujua zaidi juu ya siku hii soma niliyoandika huko nyuma kwa kubonyeza hapa (hapo utapata pia kiungo cha blogu nilizochagua siku hii mwaka jana) au nenda kwenye blogu maalum ya siku hiyo hapa. Unaweza pia kufuatilia waliyoandika wanablogu siku hii (na blogu walizochagua) kwa kubonyeza hapa. Blogu tano nilizochagua kwa ajili ya kuwapa wasomaji wangu ni hizi (bonyeza hapo chini umalize kusoma niliyoandika):
August 2006
Thu 31 Aug 2006
Blogu nilizochagua kwa Siku ya Blogu Duniani
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , wanabloguToa Maoni [3]
Wed 30 Aug 2006
Fuatilia mjadala uliotokana na habari kuhusu Wikipedia ya Kiswahili
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: wikipediaToa Maoni [4]
Baada ya kutolewa kwa ile habari ya Wikipedia ya Kiswahili kwenye gazeti la the New York Times, kumezuka majadiliano makala sana katika tovuti ya habari za teknolojia, Slashdot. Mjadala huu pamoja na kuwa na mambo mengi ya kujenga na kutupa changamoto una baadhi ya watu ambao wanatoa maoni ya kinazi na kibaguzi. Lakini wakati mwingine ni vyema kusikiliza maoni ya wanaokupinga zaidi ya wale wanaokuunga mkono. Kwahiyo bonyeza hapa ufuatilie mjadala huo. Ukifika hapo, juu kabisa habari yenyewe kwa kifupi, kisha chini yake utakuta msururu wa maoni na mjadala mkali. Unaweza kushiriki ukipenda. Bonyeza hapa usome nilipotangaza kuhusu habari hiyo au some habari yenyewe moja kwa moja kwa kubinya hapa.
Wed 30 Aug 2006
Ile siku ya Blogu Duniani (Blog Day) imewadia. Ni tarehe 31 mwezi wa nane. Huu ni mwaka wa Pili wa kusherehekea siku ya blogu duniani. Ni siku ya kusherehekea haki na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni. Ni siku ya wanablogu kutangazana. Ni siku ya wanablogu kusema kuwa hakuna kitu chochote kinachoweza kuzuia haki na uhuru wa wana dunia kujieleza na kuzungumza. Iwe ni mikono michafu ya ukatili, uongo, ulafi, na damu ya serikali. Iwe ni nguvu ya makampuni makubwa yanayotaka kumiliki nyanja ya habari na kutawala fikra zetu, iwe ni wanasiasa… (bonyeza hapo chini umalize kusoma habari hii).
Sat 26 Aug 2006
Wikipedia ya Kiswahili ndani ya The New York Times
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: kamusi elezo ya kiswahili , lugha , wikipediaToa Maoni [16]
Gazeti la The New York Times limeandika habari (ambayo nami nimehojiwa) kuhusu Kamusi Elezo ya Kiswahili. Mwandishi wa habari hii, Noam Cohen alihudhuria mkutano wa Wikimania kule Boston. Nilikuwa nikimtania sana ndugu huyu wakati wa mkutano huo kwakuwa yeye ni myahudi. Sitaki kusema matani yenyewe. Kwa mtani hunitoi na tena usijaribu! Bonyeza hapa usome makala yenyewe. (***NYONGEZA: makala niliyoizungumzia bado iko kwenye tovuti ya gazeti la the New York Times ila hivi sasa ili uisome unapaswa kulipia! Hivyo ninakupa kiungo kingine ambapo utasoma bure. Bonyeza hapa.
Na kwa wale ambao wamekuwa wakiniuliza juu ya picha yangu (ambayo haiko hapa kwenye blogu), utaona picha yangu hapo kwenye gazeti hilo. Ikitokea ukatakiwa kujiandikisha kabla ya kusoma habari hiyo, fanya hivyo maana ni tendo la dakika chache sana.
Sun 20 Aug 2006
Rais wa Irani, Mahmoud Ahmadinejad ni mwanablogu! Kaanzisha blogu ambayo wengi wetu tutahitaji wakalimani ili kuweza kuisoma. Itazame hapa.
Sun 20 Aug 2006
“Mhariri Mkuu” Anaitwa Nani Vile?/ (soma nyongeza mwishoni)
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , Uandishi wa Raia , vyombo vya habari/uongo , zanaToa Maoni [3]
Mwanamuziki Prince aliwahi kubadili jina lake huko nyuma (mwaka 1993 – 2000). Badala ya kuwa na jina lenye herufi, alichukua jina ambalo ni alama. Alama hii
ikawa ndio jina lake. Basi ikabidi watu wawe wanamwita “the artist formerly known as Prince” (msanii aliyekuwa akiitwa Prince). (Bonyeza hapo chini umaliza kusoma habari hii).
Sat 19 Aug 2006
Unapenda kuendeleza lugha za Afrika?: Jiunge na AfrophoneWikis
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , lugha , wikipediaToa Maoni [2]
Kama wewe ni mtaalamu au unajishughulisha na masuala ya lugha za Afrika au unajali maendeleo ya lugha zetu, unaweza kushiriki kwenye mijadala ya kundi liiitwalo AfrophoneWikis. AfrophoneWikis ni kundi la majadiliano kuhusu masuala ya kuendeleza Kamusi Elezo Huru (Wikipedia) za lugha za Kiafrika. Kundi hili limeundwa hivi majuzi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wikimania uliofanyika kule Boston. Washiriki ni watu ambao wanajihusisha na miradi kadhaa ya kuendeleza lugha za Afrika. Kwa mfano, ndugu Martin Benjamín wa Kamusi Hai ya Kiswahili Kwenye Mtandaoni na ndugu Don Osborn wa mradi wa Bisharat. (bonyeza hapo chini umalize kusoma habari hii):
Sat 12 Aug 2006
Digital Citizen Indaba: Skolashipu kwa Wanablogu…Fanya Hima!
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: skolashipu , mikutanoToa Maoni [8]
Taarifa hii kama inakuhusu inakupasa uchukue hatua haraka sana. Kama haikuhusu basi unaweza kutoa taarifa hizi kwa yeyote unayemjua ambaye inamhusu. Septemba 14 na 15 mwaka huu kutakuwa na mkutano wa kila mwaka nchini Afrika Kusini uitwao Highway Africa. Mkutano huu huwa unafanyika katika chuo kikuu cha Rhodes. Katika mkutano wa mwaka huu kutakuwa na mjadala uliopewa jina la Digital Citizen Indaba. “Indaba” ni neno la Kizulu. Digital Citizen Indaba ni mjadala kuhusu masuala ya blogu, podikasiti, videoblogu, uandishi wa raia, n.k.
Fri 11 Aug 2006
Wakati tunaingia katika awamu ya pili ya teknolojia za mawasiliano na habari, yaani Webu 2.0 (au kama wanavyoita: Web 2.0), kuna faida ambazo ni nzuri sana kwa wale tunaotokea katika nchi za Kusini, tukiwemo wale wa bara la Afrika. Hivi sasa kuna teknolojia na zana ambazo mtumiaji anaweza kuzitumia bila kupakua progamu yoyote kwenye tarakilishi/kompyuta. Programu hizi ni zile zilizojikita webuni.
Wed 9 Aug 2006
Wikimania: watu niliokutana nao - 1
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , wikipedia , zanaToa Maoni [12]
Wakati wa mkutano wa Wikimania, sikuhudhuria mada zote zilizokuwa zikijadiliwa. Zipo mada ambazo zilikuwa zikijadiliwa na watu ambao nimewasikiliza na kuwaona kwenye mikutano mingi. Watu hawa nawajua watakayoyasema. Hivyo nilitumia muda huu kujuana na watu, kujua wanashughulika na miradi gani, na pia nafasi yao katika vuguvugu zima la Wikipedia. Mmoja wa watu niliokutana nao ni Kevin Flaherty. Kevin anaishi Seattle katika jimbo la Washington. Mke wake anatoka nchini Kenya.
Sun 6 Aug 2006
Wikimania: teknolojia mpya na watu weusi
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , wikipedia , afrika , mikutanoToa Maoni [6]
Kuna jambo moja ambalo huwa naliona kwenye mikutano ya masuala ya teknolojia ninayohudhuria. Watu weusi hatuko kabisa. Jana nilikuwa naongea na Ethan Zuckerman. Tukawa tunajiuliza, “Hivi Wamarekani weusi wako wapi?” Mkutano wa Wikimania unafanyika Marekani katika jiji la Boston ambapo kuna Wamarekani weusi wengi. Mbona hakuna hata mmoja? Wako wapi? Kwa upande wa Waafrika tunaweza kusema kuwa pengine gharama za kuhudhuria mkutano huu ni kubwa. Afrika ni mbali. Lakini ndugu zetu walioko Marekani kwanini hawajihusishi (au labda tuulize, kutegemea na mtazamo wako: kwanini hawahusishwi?) na masuala haya ambayo ndio msingi wa uchumi, siasa, elimu, na jamii kwa vizazi vijavyo?
Sat 5 Aug 2006
Kwanza kabisa kama hufahamu kwa undani kuhusu mradi wa Wikipedia na faida zake kwetu Watanzania na Waafrika, soma niliyoandika mwezi wa tatu mwaka huu kuhusu mradi huo. Bonyeza hapa. Wakati nilipoandika makala hiyo tulikuwa na makala 292 katika Wikipedia ya Kiswahili. Sasa tuna makala 1,024! Ni lugha kama 100 tu hivi sasa duniani zenye Wikipedia zenye makala 1000 na ushee. (Bonyeza hapo chini umalize kusoma makala hii)
Fri 4 Aug 2006
Wikimania + Makala Elfu na Ushee katika Wikipedia ya Kiswahili
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: wikipedia , mikutanoToa Maoni
Moja ya habari inayosisimua watu wengi katika mkutano huu wa Wikimania ni habari kuwa Kamusi Elezo ya Kiswahili imekuwa kamusi ya kwanza ya lugha ya Kiafrika kuwa na makala zaidi ya 1000! Dakika chache zilizopita kulikuwa na idadi ya makala 1,022. Lugha nyingine za Afrika zilizo na matoleo yake ya Wikipedia unaweza kuziona kwa kubonyeza hapa (wakati unatazama orodha hiyo kumbuka kuwa kuna tofauti kati ya lugha za Kiafrika na lugha zinazozungumzwa Afrika. Orodha hii inajumuisha lugha zilizoko Afrika ingawa sio za Kiafrika). Bonyeza hapa utembelee Wikipedia ya Kiswahili utaona idadi ya makala katika ukurasa wa kwanza. Kumbuka kuwa hata wewe unaweza kushiriki kuandika makala au kusahihisha makala ambazo zimeshaandikwa. Unaweza kuandika makala kuhusu jambo lolote lile. Utaona kuwa kuna makala za vitu kama ugali, pombe za mbege na mnazi (kwenye zile kamusi elezo wanazodai kuwa zimeandikwa na “wasomi” huwezi kukuta habari za mnazi, utakuta habari za vinywaji toka katika tamaduni zao), chama cha Hezbollah, Sheng, Leonard Mbotela wa “Je Huu ni Ungwana?,” bendera, n.k.
Halafu: tazama blogu ya Wikimania kwa kubinya hapa.
Thu 3 Aug 2006
Wakati naelekea kwenye mkutano wa jumuiya ya wana Wikipedia, Wikimania (bonyeza hapa usome nilipouzungumzia mkutano huo huko nyuma [hivi kuna aliyeomba zile skolashipu?]), tunaambiwa kuwa mwanablogu wa video mwenye umri wa miaka 24 katiwa lupango kwa kukataa kutoa mikanda ya video. Soma habari hiyo katika viungo vifuatavyo: hapa, hapa, na hapa.
Kati ya watu watakaotoa mada katika mkutano huo ni ndugu Martin Benjamin, mwanzilishi wa kamusi huria ya mtandaoni, Internet Living Swahili Dictionary. Mada yake inasema: Huru na Bure: Swahili Collaboration and the Future of African Languages on the Web. Kama unakereketwa na masuala ya programu huria, kamusi huria, kamusi elezo huria, n.k.. Fuatilia habari za Wikimania hapa.



