December 2006
Monthly Archive
Sun 31 Dec 2006
Habari fupi niliyoandika kuhusu “Person of the Year” nimeitia minofu zaidi na hivyo kuwa makala ndefu ambayo imechapwa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 31, Desemba 2006. Bonyeza hapa uisome. Katika toleo hilo kuna makala kiboko aliyoandika Freddy Macha kuhusu mwanamuziki wa Tanzania, Vitali Vitalis Maembe, na mwanamuziki aliyefariki hivi karibuni, James Brown. Tafadhali soma makala hii. Nimeirudia mara mbili. Isome mwenyewe, utaniambia. Bonyeza hapa. Unaweza pia kusikiliza wimbo wa Vitali Vitalis uitwao Sumu ya Teja katika ukurasa wake wa Myspace. Sikiliza nyuzi anavyozidonoa. Na ngoma zile zikimsindikiza. Pia bonyeza hapa utazame video ya wimbo wake wa Salaam Aleykhum (shukrani Gotta kwa kiungo hiki). Dakika chache zilizopita nilikuwa nasikiliza wimbo wa Kilimanjaro wa Freddy Macha. Midundo yake ilinifanya niwe nacheza huku nikiandaa chai. Bonyeza hapa uusikilize.
**Msomaji Gotta katupatia kiungo chenye maneno ya wimbo wa Vitalis wa Sumu ya Teja. Bonyeza hapa uyasome.
Sun 31 Dec 2006
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
blogu ,
zanaToa Maoni [1]
Kama wewe ni mpiga picha au mwanablogu wa picha, bonyeza hapa usome jinsi utakavyoweza kuuza picha zako. Kwa wale wanaopenda kujenga tovuti zao wenyewe ila hawana ujuzi au muda wa kujifunza toka A hadi Z, bonyeza hapa. Kisha kama wewe ni mwanablogu na unapenda kutumia huduma inayopiga picha tovuti au blogu ambazo umeweka viungo vyake katika mambo unayoandika (kama unavyoona inavyokuwa katika viungo nilivyoweka hapa), bonyeza hapa. Hizi zote ni makala fupi mpya nilizoweka kwenye Mwongozo wa Wanablogu.
Fri 29 Dec 2006
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
afrika ,
mikutano ,
miradiToa Maoni [6]
Nilipokwenda India, ukiacha suala la kusafisha macho, nilihudhuria mikutano miwili. Mikutano hii ni ule wa Global Voices Online na wa pili uliitwa Hibiscus Project. Mkutano wa Global Voices ulifanyika kwa siku mbili. Nilijaribu, ingawa mtandao-usiwaya uliniangusha, kuandika yaliyojadiliwa siku ya kwanza ya mkutano huo. Bonyeza hapa usome niliyoandika toka ndani ya mkutano (jua kuwa niliandika bila kupitia na kuna mambo mengi pia ambayo yalinipita sikuyaandika). Siku ya kwanza ilikuwa wazi kwa mtu yeyote ambaye alikuwa amejiandikisha. Mkutano wa siku ya pili ulikuwa ni wa wahusika wakuu wa mradi huu ambapo masuala ya ndani yalijadiliwa. (more…)
Thu 28 Dec 2006
Nilipokuwa India nilisema kuwa huenda dunia haijapata kuwa na madereva makini (na wanaoendesha kwa fujo wakati huo huo) kama madereva wa India. Huenda ulidhani kuwa ninatania au ninakuongopea. Sasa kuna ushahidi ujionee mwenyewe. Madereva wale sitakaa niwasahau. (more…)
Wed 27 Dec 2006
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
utamaduni ,
afrikaToa Maoni [2]
Kuanzia tarehe 26 Desemba hadi tarehe 1 Januari baadhi ya watu wenye asili ya Afrika Marekani na kwingineko duniani husherehekea sikukuu ya Kwanzaa. Ni kipindi cha kutafakari masuala ya familia, historia, utamaduni, na jumuiya kwa kupitia dhana ya Nguzo Saba. Ni kipindi cha kusalimiana kwa Kiswahili, “habari gani,” “nzuri.” Sitaandika kipya, nitakachofanya ni kuchimba ndani ya blogu yangu na kuibua mambo niliyoandika huko nyuma juu ya siku hii. Hii tabia ya kuanza kuchimba mambo ya nyuma naanza kuipenda (ingawa inaweza kufanya mtu ukawa mvivu wa kuandika mapya. Lakini ina utamu wake, jaribu utaona). Makala ya kwanza kuhusu Kwanzaa inaitwa “Kwanzaa: Meza ya Umoja (na khanga za Mnazi Mmoja).” Bonyeza hapa uisome.
Makala ya pili kuhusu Kwanzaa inaitwa “Somo, Ngoma, na Tambiko la Kwanzaa.” Bonyeza hapa uisome. Tafadhali tafakari kuhusu Nguzo Saba za Kwanzaa.
Tue 26 Dec 2006
Kila mwaka gazeti la Marekani la Time huwa linachagua mtu ambaye huitwa “Person of the Year.” Wakati mwingine huweza kuwa ni mtu zaidi ya mmoja. Kwa mfano, mwaka jana walichaguliwa mwanamuziki Bono, Melinda Gates na mumewe Bill Gates. Huko nyuma walikuwa wakitumia maneno “Man of the Year” wakati ambapo kuna wakati watu waliochaguliwa walikuwa ni wanawake. Basi baadaye wakabadili kuwa “Person of the Year.” (more…)
Sun 24 Dec 2006
Uchovu usio na kifani. India, nitarudi tena. Nitakukumbuka daima. Nipumzike kwanza kabla ya kukupa picha halisi ya safari ya India na pia taarifa zaidi za mkutano wa Global Voices (ambao ndugu Egidio alishiriki na kupewa nafasi ya kuongea kwa Kiswahili mbele ya washiriki wote kwa dakika chache). Wakati napumzika, ningependa kukuacha na tafakari ya huu “mkumbo wa kadamnasi” uitwao Krisimasi. (bonyeza hapo chini umalize kusoma habari hii):
(more…)
Wed 20 Dec 2006
Ndio jibu ninalowapa watu ninapokuwa nakatiza mitaa fulani fulani hapa India ambayo imekaakaa kinamna. Hii ni mitaa ambayo wenyeji wananiambia niwe macho nikipita huko. Basi nikipita mitaa hiyo nikiulizwa nafanya kazi gani mimi huwaambia kuwa ninafundisha Kung-Fu. Mimi eti ni mwalimu wa Kung-Fu. Kisha nawaonyesha mbwembwe kidogo kama za Bruce Lee akiwa kwenye sinema ya Enter the Dragon na kuwauliza kama wanamfahamu. Wengi wanasema wanamjua, basi nawaambia kuwa mimi hufundisha watu kupigana kama Bruce Lee! (more…)
Tue 19 Dec 2006
Ukipewa maji ya kunywa yaliyoko ndani ya chupa ukiwa jijini Delhi, haina maana kuwa hayo maji ni yale “spesho.” Inawezekana kabisa kuwa ni maji yaliyochemshwa kisha yakawekwa ndani ya chupa za maji ya dukani! (more…)
Tue 19 Dec 2006
Bonyeza hapa utazame picha za tarakilishi ya mapajani ya watoto kwa ajili ya nchi zinazoendelea iliyoletwa kwenye mkutano wa Global Voices, jijini New Delhi. Picha hizi kapiga mwanablogu Egidio. (more…)
Sun 17 Dec 2006
Bado ulimi wangu unawaka moto. Pilipili. Acha tu. Basi ukija India mitaa niliyokatiiza ukaniulizia kwa jina la ndesanjo, hutanipata. Baada ya kuona kuwa kwa Wahindi wengi hata neno Tanzania ni gumu kutamka, basi niliamua kuwaambia kuwa naitwa Gandhi! Ukija ulizia kama wanamfahamu yule Gandhi wa Afrika. Watakwambia, “Aah, tunamjua. Alikuwa akipita hapa kijiweni usiku na kutuuliza maswali kibao na kutaka kujifunza kihindi.” Basi ndio mimi huyo. Wanaweza pia kukwambia kuwa mifuko ya suruali yangu ilikuwa imetunatuna. Ila hawajui kuwa mfukoni nilikuwa nimeweka bisibisi, mawe, na zana nyingine za kujilinda!!Nikijitokeza barabarani dakika hiii, utasikia madereva teksi na wachuuzi wakiita, Gandhi, Gandhi, Gandhi! Wananifurhia kiasi ambacho nadhani hadi ukifika wakati wa kuondoka nitakuwa nimeshapewa mungu wangu! Unakumbuka nilikwambia kuwa India ina miungu wanaozidi idadi ya watu hivyo hawataluwa na uchoyo wa kunipa mungu mmoja au wawili. Nami sitakataa. (more…)
Sat 16 Dec 2006
Habari hii, Hii Ndio India, ningependa kuiwekea viungo kadhaa lakini sina subira hata kidogo. Mtandao hauna kasi kabisa. Viungo nitaweka wakati mwingine. Msome Mental Acrobatics na pia Egidio ambao walikuwa kwenye mkutano leo hii hapa Delhi.
——
Hii ndio India. Naambiwa.
Toka niwasili tayari nimekaribia kugongwa na magari mara kadhaa, nimeshikwa shati na ombaomba, na karibu niingizwe “mjini.”
India nchi ya aina yake.
Sanamu za miungu wa Kihindi na mahekalu yamejaa kila kona. Kuna mitaa ya India ina mahekalu madogo (mengine yana ukubwa wa kujaa watu wawili!). Ukifika uwanja wa ndege wa Delhi, kitu cha kwanza unachokutana nacho ni sahamu ya mungu wa Kihindi, Kali. Mungu huyu ni hatari sana, kazi yake ni kuangamiza watu wabaya. Sio tu India ina idadi kubwa ya sanamu za miungu kuliko nchi yoyote duniani, bali pia ina miungu wengi kushinda hata idadi ya wahindi wenyewe! India ina watu wapatao bilioni moja. Idadi hii ni ndogo ukilinganisha na miungu wao. Kila kijiji kina miungu wake! (bonyeza hapo chini umalie kusoma)
(more…)
Sat 16 Dec 2006
Haya ni mambo niliyoandika wakati mkutano wa Global Voices ukiendelea. Nilikuwa niweke hapa kadri mkutano ulivyokuwa ukiendelea ila kutokana na tatizo la mtandao nikashindwa. Kwakuwa nilikuwa nimepanga kupandisha mambo haya bila kusahihisha chochote, na kwakuwa sina muda wa kufanya hivyo, ninapandisha mambo haya hivyo hivyo. Tembelea pia blogu ya Egidio ili upate habari za mkutano huu, bonyeza hapa. Egidio: ilikuwa furaha kubwa kukutana nawe! (bonyeza hapo chini umalize kusoma).
(more…)
Fri 15 Dec 2006
Nyongeza: nimekuwa najaribu kuingia kwenye Intaneti kwa zaidi ya saa moja bila mafanikio. Nilisahau kuweka kiungo ambacho kitakusaidia kuweza kushiriki na hata kutuma maswali kwenye mkutano huu. Bonyeza hapa.
Pia unaweza kufuatilia video ya moja kwa moja toka mkutanoni kwa kubonyeza hapa na kufuata maelezo utakayoyakuta hapa.
——-
Mkutano umeanza. Tatizo la mtandao usiwaya wa Intaneti ambalo limekuwa likitusumbua sana toka tufike hapa India bado linaendelea. Tatizo hili ndio limenifanya nikashindwa kuandika toka nifike hapa. Kila ninapofanikiwa kupata mawasiliano ya Intaneti ninachoweza kufanya ni yale mambo machache.
Hapa mkutanoni napo tatizo linaendelea. Lakini ukiacha tatizo hili nina furaha kubwa kuwa mwanablogu wa Kiswahili Egidio Ndabagoye yuko hapa mkutanoni. Amekaa kona ya kulia, viti kadhaa toka nilipokaa mimi. Na ataongea kwa Kiswahili na wana mkutano hapo baadaye. Wanablogu toka nchi mbalimbali wataongea kwa lugha tofauti katika kuonyesha kuwa “global voices” ziko katika lugha mbalimbali. Basi Egidio ataongea kwa Kiswahili.
Pia hapa ndani kuna mwanablogu toka Kenya, Mental Acrobatics na mwanablogu toka Uganda, Ishna.
*Kwakuwa naandika haraka huku nikishiriki kwenye mkutano, naweza kukosea herufi na pia naweza nisiwe na nafasi ya kuweka viungo na mambo kama hayo. Nitasahihisha baadaye.
Tue 12 Dec 2006
Sahihisho: wanablogu wa Kiswahili watakaohudhuria mkutano huu huenda bado wakawa wawili, ingawa Nambiza hatakuwepo. Mwanablogu Egidio wa Pilikapilika Vyuo Vikuu kuna uwezekano mkubwa naye akawepo.
——
Ninasikitika sana kuwa ndugu Nambiza Tungaraza hataweza kuhudhuria mkutano wa Global Voices Online kule New Delhi, India kutokana na sababu fulani fulani za kibinafsi. Tulikuwa tuwe na wawakilishi wawili wa blogu za Kiswahili kwenye mkutano huu. Ingekuwa poa sana kukutana nawe Tunga. Mara ya mwisho mwaka gani vile?…miaka ya tisini nadhani. Ilikuwa pale nyumbani kwenu, kisha ufukweni na ndugu Kibope na lile gitaa kavu. Kuna wimbo ule mlikuwa mmeutunga, nimeusahau jina. Miaka imepita. (bonyeza hapo chini umalize kusoma).
(more…)
Sun 10 Dec 2006
Nyongeza: sura za wana Global Voices watakaokuwa New Delhi, bonyeza hapa.
———
Jumanne wiki hii ninasafiri kwenda New Delhi, nchini India kushiriki kwenye mkutano wa kila mwaka wa mradi wa Global Voices Online:
Global Voices Online is an award-winning online portal and guide to international blogs beyond North America and Western Europe. It has also become the hub of a growing community of international bloggers who want to build a better global conversation.
(bonyeza hapo chini umalize kusoma habari hii)
(more…)
Sat 9 Dec 2006
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
siasa ,
tanzaniaToa Maoni [2]
Zawadi ya miaka 45 ya “uhuru” wa Tanganyika toka kwa mwanablogu wa katuni, Musa Ngarango. Bonyeza hapa upokee zawadi hii.
Thu 7 Dec 2006
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
mseto ,
siasa ,
tanzaniaToa Maoni [11]
Waziri Mkuu ndugu Lowassa hebu acha utani.
Nimepitia la The Guardian nikakuta habari ina kichwa hiki: Lowassa Calls a Spade a Spade. Nikadhani ni habari moto na nzito hasa. Namaliza kuisoma nikitikisa kichwa. Maswali anayouliza Waziri Mkuu huyu ni maswali ambayo sisi wapiga kura tungepaswa kumuuliza. Pengine kwakuwa hatumuulizi basi akaamua kujiuliza mwenyewe. (bonyeza hapo chini umalize kusoma).
(more…)
Thu 7 Dec 2006
Nilikuwa napitia mambo niliyokuwa naandika wakati nilipoanza kublogu. Nadhani ni jambo zuri ukishablogu kwa muda kupitia mambo ya nyuma. Sasa nimekuta habari mbili nilizoandika mwaka 2004, zote ni fupi fupi. Ya kwanza nilikuwa nikiongelea suala la hofu tuliyonayo ya kuhoji mambo: Hoji, Usiogope. Bonyeza hapa uisome. Nyingine ni visa vya jiji la Dasalama kwa Kaka Dito! Bonyeza hapa usome, Oya, Shika Mchuma!
Sun 3 Dec 2006
Sultan Tamba kumbe mtu wa matani namna hii. Sikujua. Ukiacha kamera, ndugu Tamba ni mchoraji mahiri kama utakavyoona katika katuni aliyochora kuonyesha masahibu yaliyowakumba wajumbe walioshindwa kuingia ndani ya ukumbi wa mkutano wetu. Bonyeza hapa uitazame. Kwakuwa nimemtaja Sultan Tamba ambaye ni mtengeneza filamu, ngoja nikuulize kama unafahamu kuhusu Bongowood. Kama jinsi ambavyo kuna Hollywood, na baadaye ikaja Bollywood, ikafuatia Nollywood, sasa kuna Bongowood. Bonyeza hapa.
— Next Page »