January 2007
Monthly Archive
Tue 30 Jan 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
webu 2.0Toa Maoni [1]
SHIRIKI: kama wewe ni mwanablogu au unatarajia kuwa mwanablogu au ungependa kushirikiana na wanablogu, tafadhali shiriki. Fungua hapa.
————
Mwezi wa nane mwaka jana niliandika habari niliyoiita: Webu 2.0: Awamu ya pili ya mapinduzi…. Katika habari ile nilizungumzia juu ya faida ya programu, teknolojia, au zana zilizojikita webuni. Zana ambazo mtumiaji hana haja ya kuzihifadhi kwenye kompyuta ili aweze kuzitumia. Nikasema kuwa zana hizi zina faida kubwa kwa watumiaji wa teknolojia walioko katika nchi zinazoitwa masikini. (more…)
Tue 30 Jan 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
blogu ,
wanablogu ,
TuzoToa Maoni [2]
Shindano la saba la kila mwaka la tuzo za blogu: 2007 Bloggies Award ndio hilo. Unajua mshindi atapewa nini? Atapata senti za Kimarekani 2007!:
Because of the large amount of categories, I won’t personally give a award to every winner, but the final four categories, including Weblog of the Year, will receive 2,007 US cents (US$20.07).
Ukifika kwenye tovuti ya tuzo hii, ukishuka chini utaona blogu zilizo kwenye shindano hilo. Hebu tazama blogu za ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati. Kwanza sielewi kwanini wamechanganya maeneo haya mawili. Bonyeza hapa.
Mon 29 Jan 2007
Kumbe blogu zaweza kuwa chanzo cha mahaba na hata ndoa! Mmh….Bonyeza hapa upate habari nzima.
Michuzi katukumbusha kuwa tamasha la muziki liitwalo Sauti za Busara la mwaka huu litafanyika mwezi ujao. Bonyeza hapa uende kwenye tovuti ya tamasha hili. Michuzi alihudhuria tamasha la mwaka jana. Ukibonyeza hapa utaona picha alizotuletea an habari alizoandika toka Zanzibar kwenye tamasha hilo (kwenye kiungo hicho tazama aliyoandika mwaka jana).
Mon 29 Jan 2007
Unaweza kusoma sehemu ya pili ya ule ushauri wa bure kwa vyombo vya habari Tanzania, Wanahabari, Karibuni Ndani. Makala hizi mbili zimetoka kwenye safu ya Gumzo la Wiki kwenye gazeti la Mwananchi. Sehemu hii ya pili imetoka jumapili iliyopita. Kabla ya kukupa kiungo cha makala, ngoja nikupe mistari kadhaa toka kwenye makala hii:
(more…)
Sat 27 Jan 2007
John Githongo kaanzisha blogu. Githongo alikuwa akiongoza mashambulizi ya kufunua uozo wa rushwa nchini Kenya. Hivi sasa yuko ukimbizini nchini Uingereza. Katika blogu ameweka mambo aliyorekodi kwa kaseti wakati wa uchunguzi wa kashfa ya Anglo Leasing. Blogu yake imetembelewa na watu wengi hadi ikazimia!
(more…)
Thu 25 Jan 2007
Majuzi niliandika makala kwa ajili ya gazeti la Mwananchi katika safu yangu ya Gumzo La Wiki iitwayo, Wanahabari, Karibuni Ndani. Katika makala hii nilionyesha jinsi ambavyo vyombo vya habari Tanzania (nilizungumzia magazeti) vinahitaji kubadili mwelekeo wake kutokana na mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari, elimu, na mawasiliano. Ningependa mwana Jikomboe uisome.
(more…)
Thu 25 Jan 2007
Wakati tukiendelea na demokrasia-shiriki ya kujenga Jumuiya ya Wanablogu Tanzania, soma habari kuhusu chama cha wanablogu wa Chile, Chilean Bloggers Association. Bonyeza hapa uisome. Bonyeza hapa uone tovuti yao.
Tafadhali shiriki kwenye ujenzi wa jumuiya yetu. Hivi sasa tunajadili muundo wa uongozi. Bonyeza hapa.
(more…)
Sun 21 Jan 2007
Hayawi hayawi. Jumuiya inayoundwa na wanablogu wa Tanzania ina jina rasmi. Muda wa kupendekeza umemalizika, na kamati ya muda imetangaza jina. Jumuiya hii itaitwa: JUMUIYA YA WANABLOGU TANZANIA (tukifupisha tutakuwa na jina sawa na bendi ile ya Juwata!).
(more…)
Sun 21 Jan 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
blogu ,
afrika ,
kenya ,
mikutanoToa Maoni [2]
**Nyongeza: Nilisahau kumweka mwanablogu wa Kiswahili, Ndugu Mjengwa, ambaye naye anahudhuria mkutano wa Jukwaa la Kijamii Duniani (au mkutano wa wakimbiza wezi wakuu duniani). Bonyeza hapa uone picha na maelezo toka Nairobi, Kenya.
——
Kila mwaka wezi wakuu duniani wanapofanya mkutano wao kule Geneva, Uswisi, World Economic Forum, wakimbiza wezi nao hufanya mkutano wao, World Social Forum (Jukwaa la Kijamii Duniani). Mwaka huu Jukwaa la Kijamii Duniani liko kule Kenya.
(more…)
Sat 20 Jan 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
blogu ,
sheria ,
mikutanoToa Maoni [7]
Moja ya matatizo ya taaluma ya uandishi wa habari ni kuwa waandishi katika nchi mbalimbali huwa wanajifunza taaluma moja: uandishi wa habari. Lakini kutokana na kazi zao huwa wanajikuta wanaandika habari za taaluma mbalimbali ambazo hawazifahamu kwa kina. Wako wanaoamini kuwa njia bora ya kuondoa tatizo hili ni kuweka mfumo ambao utawafanya wanaotaka kusomea uandishi wa habari kuwa na taaluma nyingine kwanza kabla ya kusomea uandishi wa habari. Au wawe na mafunzo ya kutosha kuhusu taaluma ambayo watakuwa wakiandika habari zake.
(more…)
Mon 15 Jan 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
siasa ,
dini ,
demokrasiaToa Maoni [12]
Mwaka 1988, aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo, Ronald Reagan (ndio, Reagan aliyekuwa rais wa Marekani, unaweza usiamini) alitia saini sheria ya kufanya kila jumatatu ya tatu ya mwezi Januari kuwa ni siku ya kukumbuka maisha, harakati, na falsafa za Dr. Martin Luther King, JR (MLK). Hii ndio sikukuu pekee inayoazimishwa kwa ajili ya mtu mweusi hapa ndani ya tumbo la Jitu (Nadhani unafahamu kwanini Malcolm X hana sikukuu ya kitaifa.)
(more…)
Sun 14 Jan 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
wanablogu ,
tanzaniaToa Maoni [13]
Mwishoni mwa mwaka jana wanablogu wa Tanzania, kwa kutumia teknolojia za dijitali, tuliweza kufanya mkutano kwenye mtandao wa Intaneti. Tukajadili mambo kadhaa na pia kutangaza kuwa kila tarehe 18 Novemba ni Siku ya Blogu Tanzania. Katika mkutano ule baadhi ya mambo hayakuweza kuamuliwa kwani kulihitajika muda zaidi wa kujadili na pia ushiriki wa wanablogu na wapenzi wa blogu wengi zaidi. Iwapo ndugu msomaji huelewi ninazungumzia nini, basi fuata viungo hivi ili uweze kuelewa. Soma kuhusu mkutano huo kwa kubonyeza hapa. Bonyeza hapa utazame ukurasa wa wiki wa mkutano. Hapa kuna makala iliyotoka katika gazeti la Mwananchi kuhusu mkutano huo.
(more…)
Fri 12 Jan 2007
World Press Institute ina mpango wa “fellowship” wa miezi minne kila mwaka kwa waandishi wa habari toka nchi mbalimbali duniani kutembelea Marekani. Mpango huu unawapa waandishi waliochaguliwa nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali Marekani kwa muda wa miezi mitatu (karibu nusu ya majimbo yote), kuhudhuria mikutano, kufanya mahojiano, na kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo nyanja ya habari na mengineyo. (more…)
Tue 9 Jan 2007
Michezo mingi ya kwenye kompyuta (computer games) huwa haina mafunzo yoyote ya msingi zaidi ya burudani (burudani?) kupitia mikasa inayohusisha umwagaji damu, ubomoaji wa majengo kwa mabomu, kuendesha magari mbio na kugonga wapita njia bila huruma, kubeba “changudoa” mitaani, n.k. Kuna fani mpya katika michezo hii ya kwenye kompyuta au michezo digitali ambayo inajaribu kuchanganya teknolojia na harakati. Wenye kujihusisha na fani hii waniita michezo yao “Games for Social Change.” Tunaelezwa kuwa fani hii ni tawi toka kwenye fani nyingine ya “Serious Games” ambayo hutumiwa kwenye nyanja mbalimbali kama za jeshi, utabibu, diplomasia, n.k. (more…)
Sun 7 Jan 2007
Kipindi cha BBC cha Newsnight kina filamu kuhusu mapinduzi ya simu za mkono nchini Kenya, Kenya’s Mobile Revolution. Filamu hii inaongozwa na Paul Mason.
Hivi ndivyo Newsnight isemavyo:
Mobile phones in Africa are helping to provide better services, economic growth and even democratic rights. Paul Mason reports from Kenya on how technology has stepped in where governments and aid agencies have failed.
(more…)
Fri 5 Jan 2007
Niliwahi kuandika huko nyuma kuhusu zana zinazokuwezesha kuiuliza dunia nzima maswali kuhusu jambo lolote. Zana hizi zinatuwezesha kufanya mambo mapya ambayo huko nyuma hatukuweza kufanya. Ubongo wa dunia nzima unasubiri swali lako. Zana hizi sio tu zinakuwezesha kuuliza maswali bali pia kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa na watu wengine. Nimekuwa natembelea tovuti za zana hizi na kuelimika sana. Kama hukusoma niliyoandika au unataka kusoma tena bonyeza hapa. (more…)