Majuzi, mwanablogu Kareem Sulaiman wa Misri alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela kutokana na kuandika mawazo yake kwenye blogu yake. Bonyeza hapa uone blogu yake. Pia unaweza kufuatilia habari zake kwenye tovuti ya kampeni ya “Free Kareem.” Hii sio mara ya kwanza kwa wanablogu nchini Misri kupata misukosuko toka serikalini. Soma hapa yaliyotokea mwaka jana. Bonyeza hapa usome zaidi kuhusu kisa cha Kareem toka Global Voices Online. (more…)
February 2007
Wed 28 Feb 2007
Mwachilie Huru Kareem Sulaiman! + Tuzo Za Blogu Bora Uganda
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , sheria , Tuzo , harakati dijitaliToa Maoni [10]
Mon 26 Feb 2007
“YouTube” za Africa: Jambo Video, Kenyamoto, Mooziko, SwahiliRemix, n.k.
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , afrika , tanzania , kenya , videoToa Maoni [7]
Tukizungumzia mapinduzi ya zana mpya za habari na mawasiliano, hatuwezi kuacha kuitaja YouTube (Broadcast Yourself). YouTube ndio mapinduzi yenyewe tunayozungumzia. Sitaki kuongelea YouTube bali tovuti mbalimbali za Afrika au zinazohusu Afrika ambazo nimeamua, ingawa zina tofauti kadhaa na YouTube, kuziita YouTube za Afrika. Tunaanza na Jambo Video ya Tanzania. Bonyeza hapa uitazame. (more…)
Sun 18 Feb 2007
Nilipomaliza Kuandika Makala Hii Nilipiga Ngumi Ukutani!
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: siasa , tanzania , demokrasia , makalaToa Maoni [19]
Nilipopiga ngumi ukutani, nilijiumiza mwenyewe…soma makala ambayo imetoka jumapili ya wiki hii katika safu yangu ya Gumzo La Wiki kwenye gazeti la Mwananchi. Makala hiyo ina kichwa hikii: KABLA YA KUBADILI NCHI, BADILI MTAANI KWENU. Ni makala inayokutana inayokutaka kuanza kujifunza mbinu rahisi za kuleta mabadiliko ya kudumu nchini. Kati ya mambo niliyosema katika makala hiyo ni: (more…)
Sun 18 Feb 2007
Miriam na “Anti HTML-table Zone” + Image Chef
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: mseto , teknolojia , zanaToa Maoni [6]
Kama wewe unapenda kujifunza masuala ya ujenzi wa tovuti, basi soma mwongozo ulioandikwa na mwanablogu mwenzetu, Miriam, wa Mirecipe. Jumuiya yetu nikiitazama inanifurahisha sana. Tukitazama kila mmoja wetu ujuzi wake na maarifa aliyonayo, utagundua kuwa tunachofanya sio tu kujenga jumuiya ya wanablogu, bali pia kisima cha wana maarifa. Mwongozo wake kauita, Anti HTML- table Zone. (more…)
Sat 17 Feb 2007
Simu Za Mkono Na Mabadiliko Chanya Ya Jamii
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , afrika , harakati dijitaliToa Maoni [7]
Huenda wewe ni mwanaharakati. Huenda unajihusisha kwa njia moja au nyingine katika harakati za kuleta mabadiliko chanya ya jamii. Je ni vipi unaweza kutumia simu ya mkono ili kuleta mabadiliko? Watembelee MobileActive ujifunze mbinu mbalimbali na usome habari zinazohusu simu za mkono na mabadiliko chanya ya kijamii. Bonyeza hapa. Kwa upande wa siasa, unaweza kusoma ripoti inayohusu matumizi ya simu za mkono kwenye uchaguzi mwaka jana nchini Marekani. Bonyeza hapa. Ingawa ripoti hii inahusu Marekani, utaona kuwa zipo mbinu mbalimbali ambazo hata vyama vya siasa vya nchi kama Tanzania wanaweza kuzitumia.
SMS Ilivyotumiwa Kupindua Serikali:
Mwaka 2001 matumizi ya kisiasa ya ujumbe wa maandishi wa simu za mkono (SMS) yalichangia kumuondoa madarakani rais wa Ufilipino, Joseph Estrada. (more…)
Sat 17 Feb 2007
Reuters Na Blogu Za Afrika
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , wanablogu , afrika , tanzaniaToa Maoni [2]
Kama ambavyo mashirika mengi ya habari yanatambua umuhimu wa kazi za wanablogu, jamaa wa Reuters nao hawajabaki nyuma. Reuters ina mkataba wa ushirikiano na mradi wa wanablogu wa Global Voices Online. Kutokana na mkataba huu, Reuters imefungua kikusanya habari (aggregator) cha habari ambacho pamoja na kuwa na habari toka kwenye vyombo vingine vya habari, kuna habari toka kwa wanablogu. Ukifika katika tovuti yao unaweza kuchagua nchi ambayo unataka habari zake, utapata ramani ya nchi hiyo na upande wa kulia wa kisanduku cha kuchagua nchi, utaona kona ya habari zilizoandikwa na wanablogu wa nchi hiyo. Bonyeza hapa uone kikusanya habari hicho (nimechagua Tanzania, hivyo kiungo hicho kitakupeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wa Tanzania). Blogu utakazoziona hapa ni zile ambazo habari zake zimeandikwa kwenye ukurasa wa Global Voices Online.
Fri 16 Feb 2007
Samahani sana kwa kutokuwepo hapa kwa siku kadhaa. Nitarudi rasmi leo hii. Jikomboe!
Nimesharudi.
Sun 4 Feb 2007
Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania: Huu ndio muundo wa uongozi
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , wanablogu , tanzaniaToa Maoni [13]
Polepole ndio mwendo. Wanablogu wa Tanzania mwaka jana tulianza na mkutano mtandaoni, tukaja na kuchagua jina (ambalo ni Jumuiya ya Wanablogu Tanzania - JUWATA), halafu wiki mbili zilizopita tukashauriana na kutoa mapendekezo yetu kuhusu muundo wa uongozi na kamati. Matokeo yametoka. Bonyeza hapa uone muundo wa uongozi uliopita. Shukrani kwa wote walioshiriki na hata wale ambao hawakushiriki ila wanaunga mkono jitihada hizi.
Thu 1 Feb 2007
Thu 1 Feb 2007
Baada ya Skype kujipatia umaarufu kwenye teknolojia za simu za mtandaoni (kundi la teknolojia hii huitwa VoiP - Voice Over Internet Protocal), jamaa wa Gizmo Project wameingia kwenye uwanja huu kwa mara ya pili na Gizmocall. Mara ya kwanza ilikuwa ni Gizmo Project. Nakumbuka niliandika juu ya Skype mwaka 2004 (tazama hapa). Toka wakati huo nimeitumia Skype. Mahojiano yangu na Deus Gunza wa Radio Butiama tuliyafanya kwa kutumia Skype. Lakini Gizmocall inaelekea kunivutia. Bado sina sababu za msingi. Ni hisia zangu tu maana nimeitazama kijuujuu tu. (more…)



