March 2007
Monthly Archive
Wed 28 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
afrika ,
historiaToa Maoni [12]
Soma mawazo ya baadhi ya wanablogu wa Afrika kuhusu utumwa, fidia, na msamaha. Habari hii nimeiandika kwa ajili ya tovuti ya Global Voices Online. Mmoja wa wanablogu hao, Chixta anasema:
……If you watch the movie Roots, Kunta Kinte was not kidnapped by white guys, he was kidnapped by niggers…..
If there is anyone who should apologise, it is those of us that come from Africa now. We should apologise to those that can’t trace their roots, and have no ‘true sense’ of identity, afterall we sold them.
(more…)
Wed 28 Mar 2007
Mjadala bado unaendelea. Je wanablogu ni waandishi wa habari? Bunge la Lituania limekataa kutoa kibali kwa mwanablogu wa nchi hiyo, Liutauras Ulevicius, kuhudhuria na kuripoti vikao vya bunge kama mwanablogu. Mwanablogu huyo anasema kuwa atakwenda mahakamani. Soma habari hiyo hapa. Tukiacha habari hiyo, kuna habari ya kutishiwa kuuawa kwa mwanablogu Kathy Sierra. (more…)
Mon 26 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
afrika ,
historiaToa Maoni [4]
Kumbe! Ala…
Kanisa la Anglikana lilikuwa na watumwa. Pengine sio ajabu maana kitabu chao kimejaa utumwa katika kurasa mbalimbali na hata mmoja wa watume wake wanawaambia watumwa wawaheshimu mabwana zao (na sio kudai haki zao). Sasa kanisa linaelekea kutaka kulipa fidia. Lakini swali kubwa ni: je fidia hiyo iende kwa nani? Soma zaidi hapa.
Sun 25 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
afrika ,
kenya ,
uchumiToa Maoni
White African amehudhuria mkutano wa Wakenya ulioitwa “The Role of the Kenyan Diaspora in Kenya’s Development.” Soma nukuu hizi alizoandika toka kwenye mkutano huo: (more…)
Sun 25 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
afrika ,
historiaToa Maoni [7]
Wakati dunia inakumbuka kupitishwa kwa sheria ya kupiga marufuku biashara ya utumwa na bunge la Uingereza miaka 200 iliyopita, ningependa utazame video ya Rasta Babu Burning Spear akikuuliza, “Do you remember the days of slavery?” kwenye wimbo wake wa Slavery Days.
And how they beat us
And how they worked us so hard
And how they used us
Till they refuse us
Do you remember the days of slav’ry?
(more…)
Sun 25 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
msetoToa Maoni
Sat 24 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
afrikaToa Maoni [4]
Unajua kuna watu ambao wanadhani kuwa sisi Waafrika hatuwezi. Utawasikia wakisema, “wazungu achaneni nao.” Kumbe suala sio rangi. Ni mazingira, sera, na kuwezeshwa kwa wanafunzi, wanazuoni, na wananchi kwa ujumla. Blogu ya Afrigadget inasaidia kuondoa hisia potofu kuwa sisi Waafrika hatuwezi. Sio wanasayansi. Sio wabunifu. Sio wavumbuzi. Uwe ukiitembelea blogu hii kupata habari mbalimbali kuhusu wanasayansi wetu ambao hakuna anayewajali. Hata zile wizara zinazoitwa “wizara za sayansi” (na utumbo) hazina hata majina yao. Afrigadget inatupa habari na picha ya baiskeli yenye injini kama pikipiki iliyotengenezwa Mombasa, Kenya.
Fri 23 Mar 2007
Blogu ya Kenya ya African Affairs ina makala ya sehemu nne inayoelezea tofauti za kitamaduni kati ya Wakenya na Watanzania. Katika makala ya kwanza anatoa mfano huu:
Picture this:
A.
In a restaurant in Nairobi, a Kenyan is asking to be served a cup of tea.
Kenyan: Hello, we leta chai ninachelewa. Harakisha basi!
In a restaurant in Dar es Salaam, a Tanzanian is asking to be served a cup of tea.
Tanzanian: Habari za saa hizi. Naomba kikombe cha chai ya rangi.
B.
In a mathree (matatu) in Nairobi, a conductor is asking for fare from the passengers.
Conductor: Leta pesa yako na ufanye fasta (bring the fare and be fast at that). Fare ni mbao (twenty shillings) sitaki mtu ambaye anajifanya hajui fare ni chapa ngapi!
In a Daladala in Dar es Salaam, a conductor is asking for fare from the passengers.
Conductor: Naomba nauli yako. Nauli ni mia mbili hamsini (approximately Ksh 14).
(more…)
Thu 22 Mar 2007
Afrika Kusini wanaelewa somo. Somo la Teknohama (teknolojia za habari na mawasiliano). Majuzi tulisikia kuhusu Gargoyle. Sasa gazeti la Mail & Guardian wamekuja na Amatomu. Amatomu ni kama Technorati. “Technorati” ya Afrika Kusini. Technorati imekuwa ikilaumiwa kwakuwa teknolojia yake ina upendeleo fulani kwa wanablogu wa nchi za Magharibi. Soma lawama hizo toka kwa Africa Media, Blacklooks, na mchango wa Grandiose Parlor. Katika mazingira kama haya, ujio wa Amatomu tunaushangilia.
Kuhusu Technorati, wikipedia inasema:
Technorati is an Internet search engine for searching blogs, competing with Google, Yahoo and IceRocket. As of December 2006, Technorati indexes over 55 million weblogs.
(more…)
Tue 20 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
siasa ,
tanzania ,
makalaToa Maoni [6]
Msangi Mdogo amekuwa akituelimisha juu ya aya za kidikteta zilizoandikwa na genge linalojiita serikali na wawakilishi nchini Tanzania. Aya hizi nimeziita kuwa ni kifo cha uwazi na ukweli. Wiki iliyopita nilikaa chini nikaandika makala ambayo nitakupa uisome. Niliiandika kama vile nilikuwa nimekula jani. Makala hii niliiandika kwa ajili ya gazeti la Mwananchi. Iliitwa: Mapambano Dhidi ya Kifo cha Uwazi na Ukweli. Kuna ile makala nyingine ambayo nilipomaliza kuiandika nilipiga ngumi ukutani, nikajiumiza mwenyewe. Safari hii sikufanya hivyo. Nilipomaliza nilikwenda kutembea bustanini. Kutafakari. Kutazama maua, ndege, na vipepeo.
(more…)
Tue 20 Mar 2007
White African kachapa habari toka Pambazuka. Habari hii Rasta Luihamu lazima aisome. Inaanza hivi:
Rural farmers in central Kenya have been piloting a project, called DrumNet, that provides marketing, financial services and information to them using their mobile phones. The project’s premise is that information on the market is one of the key elements that keeps farmers from getting the full market value for their products. This lack of information also keeps the farmers in a disadvantageous financial position, so that it is difficult to get the financing and resources they need to grow their business.
(more…)
Sat 17 Mar 2007
Aliyekuwa mwizi wa Malawi, Bakili Muluzi, ameshindwa kuishi maisha ya wastaafu. Amekumbuka utamu wa madaraka. Anataka tena kurudi jikoni. Ikulu. Kamaliza vipindi vyake viwili sasa anadai kuwa wananchi wamemtaka awe rais wao tena. Kwa kuwa ana rohoo njema sana, amekubali. Atagombea urais mwaka 2009. Wakimlilia na kumtaka awe rais wa maisha sidhani kama atakuwa na roho mbaya. Atakubali. Ndio siasa hizi za bara letu. Zimbabwe wala usiseme kitu. Weka sikio ardhini, sikiliza. Itazame Zimbabwe. Baada ya Bakili kutangaza hivyo, mwananchi mmoja wa Malawi akaamua kutumia blogu kama moja ya silaha ya mapambano dhidi ya nia chafu ya Bakili Muluzi. (more…)
Fri 16 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
afrika ,
historiaToa Maoni [12]
Mwidimi ni mmoja wa washiriki wakubwa katika mijadala ndani ya blogu zetu. Ninaheshimu sana wasomaji kama hawa ambao wanashiriki na kuanzisha mijadala juu ya habari tunazoandika. Hawa ndio wasomaji wa zama hizi ambao wanataka kupata habari kwa mfumo ambao utawaruhusu nao kuchangia, kusahihisha, kufafanua, kuuliza maswali na kadhalika. Hawa ndio wale ambao Jay Rosen anawaita, “The People Formerly Known as the Audience.”
Mwidimi kaandika makala fupi inayorusha mishale ya moto. Moto wa maarifa, historia, na elimu ya utu. Anasema kuwa utumwa unaosemekana kuwa ulimalizika miaka 200 iliyopita unaendelea kwa kasi. Tena majumbani mwetu. Bonyeza hapo chini usome makala hiyo. Utaniambia mwenyewe.
(more…)
Fri 16 Mar 2007
Toka mwaka 2005 wanablogu wa Afrika Kusini wamekuwa wakitoa tuzo kwa blogu bora katika makundi mbalimbali. Tuzo za mwaka huu zimekuja na yake mengi. Mabishano, majadiliano, maswali, majibu, na kila kitu ndani yake. Ninaona kuna mambo ambayo nasi wanablogu wa Tanzania tunaweza kujifunza toka kwa wenzetu Afrika Kusini ili kuhakikisha kuwa tuzo hizo zinaheshimika na kuondoa kabisa au kupunguza lawama na hisia mbaya. Sasa ili ujue undani wa mabishano na majadiliano haya kuhusu “The South African Blog Awards - 2007″ soma muhtasari wake niliouandika kwenye blogu ya Global Voices Online. Kichwa chake ni: South Africa: Blog Awards Mashup: Blogging Is Dead, Where Art Thou Stormhoek?, Conflict Of Interest, and Elite Bloggers.
Ili uisome bonyeza hapa.
Wed 14 Mar 2007
Kila mwaka Project For Excellence in Journalism hutoa ripoti kuhusu vyombo vya habari, The State of News Media. Ripoti ya mwaka huu, The State of News Media - 2007, imetoka. Ripoti hii inaonyesha jinsi ambavyo nyanja ya habari inabadilika kwa kasi wakati ambapo vyombo vya habari vya jadi vikibadilika kwa mwendo wa kinyonga. Mradi wa Global Voices Online umeonekana kuwa mfano bora wa mabadiliko katika nyanja hii. (more…)
Sun 11 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
zanaToa Maoni [5]
Je Tumblelog ni mtoto wa blogu? Labda.
Tumblelog ni nini? Ni aina ya blogu ila sio blogu. Wajamaa wa Tumblelog wenyewe wanaielezea hivi:
What’s a tumblelog? To make a simple analogy: If blogs are journals, tumblelogs are scrapbooks. You can also look at tumblelogs as slightly more structured blogs that make it easier, faster, and more fun to post and share stuff you find or create.
(more…)
Sat 10 Mar 2007
Katika mkutano wa Global Voices Online kule New Delhi, India, siku ya pili tulijadili mambo mbalimbali likiwemo suala la uhamasishaji na mafunzo kwa wanablogu wapya/wachanga au wale ambao sio wanablogu ila wanaweza kufaidika na teknolojia hii. Bonyeza hapa usome baadhi ya mambo yaliyojadiliwa siku hiyo. Kutokana na umuhimu wa shughuli ya uhamasishaji, Global Voices Online imetangaza nafasi ya kazi: Outreach Director (Mkurugenzi wa Uhamasishaji). (more…)
Sat 10 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
siasa ,
blogu ,
tanzania ,
sokaToa Maoni [3]
Vijana/wapenzi wa Jangwani wana blogu. Simba je?
Viongozi wa Chadema wana blogu (ingawa bado hazina uhai). Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi je?
Sat 10 Mar 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
blogu ,
afrika ,
zanaToa Maoni
Ndio, najua hii ni blogu ya Kiswahili. Lakini nimeona nisiumize kichwa nikitaka kutafsiri kichwa cha habari. Maneno hayo hapo juu ndio kichwa cha habari niliyoandika jana kwenye ukurasa wa Global Voices Online kuhusu “blog search engine” ya blogu za Afrika iitwayo, Gargoyle. Soma habari hii utaelewa umuhimu wa injini hii katika suala zima la mapinduzi ya teknolojia na maendeleo ya Afrika. Bonyeza hapa uisome.
Sat 10 Mar 2007
Kitu Kizuri. Kama binti wa Afrika.
Kitu Kizuri ni jarida la wanawake wa Afrika. Inaonyesha kuwa waanzilishi wa gazeti hili wanaheshimu lugha ya Kiswahili (na sio ajabu hawakifahamu). Bonyeza hapa utazame Kitu Kizuri. (more…)
— Next Page »