Mradi wa Knight News Challenge una dola milioni tano za kutoa bure! Kila mtu ana sifa za kuomba na pia kupata. Ili mradi uwe na wazo linalohitaji kufanyiwa kazi, wazo hilo liwe la kipekee, liwe linahusisha teknolojia ya habari na mawasiliano, liwe lina malengo ya kujenga jumuiya…kama una wazo la namna hii na unajikuna kichwa jinsi ya kupata fedha za kulitekeleza, nafasi ndio hii. Haijali mwombaji anatoka nchi gani. Bonyeza hapa ufuatilie changamoto hii. Usije ukasema sikukwambia. Lakini…sio mtu mmoja atajichukulia dola milioni tano. Hapana. Huyu dola elfu 20, huyu elfu tano, yule elfu 7, n.k. hadi milioni tano iishe.
August 2007
Tue 28 Aug 2007
Knight News Challenge: Dola Milioni 5 Zinakusubiri
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , miradiToa Maoni [6]
Mon 27 Aug 2007
Hii Ndio Hoja Aliyoizua Zitto Kabwe…Na Tutajadili!
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: siasa , tanzania , demokrasiaToa Maoni [10]
Katika mambo yote yanayotokea kuhusu suala la Zitto, tamko la Katibu wa Bunge la kutaka wananchi wasijadili hili suala la sivyo watachukuliwa hatua ni la kupingwa vikali kabisa. Toka lini kazi ya Bunge ikawa ni kutuambia wananchi mambo gani tujadili na mambo gani tusijadili? Hakuna chombo chochote kina uwezo wa kutukataza kujadilia masuala yanayohusu nchi yetu wakati ambapo mjadala huo hauvunji sheria yoyote bali ni utekelezaji wa moja ya kanuni za demokrasia na haki zetu za kikatiba. TUTAJADILI, ndugu Katibu wa bunge (anaitwa nani tena huyu jamaa?). Haya, bonyeza hapa usome hoja yenyewe iliyoleta mgogoro huu wa kisiasa na kidemokrasia Tanzania.
Sun 26 Aug 2007
Ucheke una mwanya? Ucheke unatumia Blogger? Watumiaji wa Blogger wamewezeshwa. Jinsi ilivyo rahisi kuweka picha kwenye Blogger, hivi sasa ni rahisi pia kuweka video zako mwenyewe kwa urahisi kabisa. Kama wewe unatumia Blogger/Blogspot na unapenda kujua jinsi ya kuweka video kwenye blogu yako, bonyeza hapa.
Sun 26 Aug 2007
Naona mzimu wa Wikipeda umeniingia. Nimeandika habari za Wikipedia mfululizo. Mizimu hii huwa inakuja na kuondoka. Kuna jambo moja linalonifurahisha sana kwenye jumuiya ya wana Wikipedia. Jambo lenyewe ni kuwa, mtu anaweza kushiriki kwenye ujenzi wa Wikipedia ya lugha fulani hata kama hajui lugha hiyo! Teknolojia nyingine huwa nazitazama na kucheka tu. Kwa mfano, kwenye Wikipedia ya Kiswahili tuna wajenzi/wachangiaji ambao hawajui Kiswahili hata kidogo.
(more…)
Sat 25 Aug 2007
Ukiona vinara wa mapinduzi ya mtu mweusi na muungano wa Afrika wanaanza kutumia zana mpya za mawasiliano, maarifa, na habari, basi ujue yule aliyesema, “…the revolution will be digitized” hakuwa amekosea. Horace Campbell ni mtu ambaye unamweka kwenye kundi la akina Walter Rodney. Wanazuoni wanaharakati wa utu na maendeleo ya watu weusi ulimwenguni kote. Yeye ni mwandishi wa kitabu (ambacho unaweza kukipata kwenye maduka nchini Tanzania) kiitwacho, Rasta and Resistance: From Marcus Garvey to Walter Rodney, ambacho alikichapisha wakati akiishi Tanzania. Aliandika pia kitabu kiitwacho, Bob Marley Lives, mara baada ya kufariki kwake. Hiki pia alikichapisha nchini Tanzania.
(more…)
Fri 24 Aug 2007
WikiScanner: CIA, Vatican, Labour Party, Amnesty International…wanaona haya hao!
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: wikipediaToa Maoni [3]
Virgil ana miaka 24. Ni mwanafunzi wa masuala ya kompyuta. Ni mmoja wa wale wanaoitwa “hackers.” Majuzi ametuletea zana ambayo imetia aibu makampuni makubwa, serikali, na hata CIA na Vatican. Zana hiyo inaitwa WikiScanner. Kwa kutumia WikiScanner unaweza kuona ni akina nani wanaohariri Wikipedia. Kwakuwa kila kompyuta huwa na anuani yake (IP), zana hii imewezesha watu kuona jinsi ambavyo wanasiasa, makampuni, CIA na hata Vatican wamekuwa wakihariri Wikipedia (kujipendelea au kuandika mabaya kuhusu wenzao). Moja ya habari kuhusu kijana huyu inasema:
One American student sent major corporations, governments and even the Vatican on the defensive after coming up with Wikipedia Scanner, a software program that reveals who changed Wikipedia entries.
Fri 24 Aug 2007
Bonyeza hapa usome sehemu ya kwanza ya Wikipediolojia.
Wachangiaji kwenye Wikipedia ya Kiswahili wameongezeka kwa ghafla. Sijui kimetokea nini. Ila ni furaha kubwa. Katika makala ya kwanza ambayo nilitoa maelekezo kwa kifupi ya jinsi ya kuhariri Wikipedia, nilizungumzia suala la kuandika makala bila ushabiki. Ndio maana nikasema huwa sio jambo zuri mtu kuandika makala juu yake. Makala za kwenye Wikipedia zinapaswa kuandikwa kwa uangalifu. Hata hivyo, sio lazima washiriki wote wawe na ufundi wa lugha. Kwakuwa kazi hii tunafanya kijamaa na kiharambeeharambee, tunasaidiana kusahihishana.
Tue 21 Aug 2007
Ni furaha kubwa kuona wahariri wapya kadhaa wa Wikipedia ya Kiswahili wamejitokeza siku za karibuni. Wengi wao naona wametoka kwenye nyanja ya muziki na filamu nchini Tanzania. Tena ni vijana. Furaha ilioje. Kuingia kwao kumenisukuma kufanya jambo ambalo nilipaswa kulifanya siku nyingi sana: kuandika mwongozo wa jinsi ya kuhariri Wikipedia. Kabla hujasoma mwongozo huo, kama hujui hasa Wikipedia ni nini, bonyeza hapa usome kwanza makala itakayokupa picha kwa ufupi kuhusu Wikipedia. Kama unajua Wikipedia ni nini, endelea kusoma makala hii.
(more…)
Fri 17 Aug 2007
Marufuku Kuanzisha Blogu! Geti Limefungwa!
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , wanabloguToa Maoni [10]
Mtu niliyekuwa nikimsubiri kwa miaka na miaka ili aingie kwenye masuala ya blogu sasa kaingia. Nilikuwa najua iko siku. Uzoefu wake huku bloguni tunauhitaji. Sasa kaingia. Na kwasababu hiyo geti limefungwa. Hakuna kuanzisha blogu mpya tena. Marufuku. Zimetosha….kama hujui kuwa natania, kanywe chai. Natania.
Ila sitanii kuhusu kuingia kwa mwanablogu mpya. Huyu ni mwanablogu ambaye amechochea wengi wetu kupenda masuala ya fasihi toka tukiwa watoto. Huyu ni mwandishi wa siku nyingi, mwanamuziki, mwalimu wa michezo ya kujilinda toka Ujapani, Uchina, na Brazili. Mtunzi wa kitabu cha Twen’zetu Ulaya, Remi Ongala, Mpe Maneno Yake (hiki kiko madukani Tanzania hivi sasa), Papers! Papers! Papers! (cha mashairi ya kiingereza na kijerumani) na kuendelea. Pia ni mwandishi wa makala kila jumapili katika gazeti la Mwananchi. Ni mwandishi wa makala za zamani kwenye gazeti la Sunday News za “Cultural Images.” Ukumbini, namuingia mwanablogu mpya, ndugu yangu….Freddy Macha! Bonyeza hapa. Halafu soma makala yake hapo iitwayo, “Let’s talk about textmessaging.”
Fri 17 Aug 2007
Hivi unadhani unajua majina ya ndege, wewe? Ukiacha kunguru, korongo na bata maji, majina gani mengine unayajua? Basi ongeza elimu yako ya majina ya Kiswahili ya ndege. Bonyeza hapa uone mwenyewe.
Thu 16 Aug 2007
Mugabe Atangaza “Cyberwarfare”
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , sheria , demokrasia , global voicesToa Maoni [13]
Kwa kiingereza wanaita “cyberwarfare.” Ndio aina ya vita alivyotangaza dikteta Mugabe baada ya kuamua kufungia tovuti za habari na blogu ikiwemo tovuti ya Global Voices Online. Amefungia pia tovuti ya ubalozi wa Marekani, ambayo amesema kuwa inaendesha vita vya mtandaoni dhidi ya serikali yake. Bonyeza hapa usome habari hiyo.
Wed 15 Aug 2007
Highway Africa: Language and the Blogosphere: the KiSwahili -Tanzania Experience.
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: mseto , blogu , lugha , mikutanoToa Maoni [3]
Nimefurahi kuona kuwa mkutano wa Highway Africa wa mwaka huu umetambua mchango wa wanablogu wanaotumia lugha ya Kiafrika, Kiswahili. Hii ni hatua nzuri inayotupa moyo na kuona kuwa ili kazi na juhudi zetu zitambuliwe, sio lazima tutumie lugha za kuja. Kwa wale wasiojua Highway Africa ni nini:
Highway Africa is an annual ICT conference hosted by Rhodes University which is situated in Grahamstown, South Africa.
Each year, more than 500 delegates from across the globe attend the conference to discuss issues relating to Internet governance, ICT policy and media for democracy.
Basi katika mkutano wa mwaka huu, ambao utafanyika Septemba 10 - 12 huko Grahamstown, Afrika Kusini, kutakuwa na mjadala ambao wazungumzaji wakuu watakuwa ni wanablogu wa Kiswahili.
(more…)
Sun 12 Aug 2007
Kazi Global Voices Online: Mhariri wa Video
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: nafasi za kazi , global voicesToa Maoni [2]
Kama unafahamu masuala ya blogu na video, omba kazi ya uhariri wa video Global Voices Online. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 24 mwezi huu. Kama masuala haya huyafahamu, usipoteze muda wa kuomba:
Our ideal candidate has an international outlook and solid experience in blogging and online citizens’ media with a special emphasis on online video. Solid English-language writing editing skills are a must, but a strong familiarity with the current tools, web sites and trends in online video worldwide is important. S/he has the ability to work independently and responsibly with only remote supervision.
Mon 6 Aug 2007
Toka Kwenye Wikimania 2007 Hadi Taipei 101
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: mikutano , safariToa Maoni [2]
Mkutano wa Wikimania 2007 umemalizika jana. Kilichobaki sasa ni kusafisha macho. Baada ya kutoka kwenye masuala ya kamusi elezo huria duniani, nikimaliza kuandika ninachoandika hapa nitaelekea kwenye jengo refu kuliko yote duniani lililoko hapa Taipei (ingawa linakaribia kidogo kupitwa. Sijui itabidi waongeze paa?). Jengo hili linaitwa Taipei 101. Tarakimu 101 zinatokana na idadi ya gorofa zilizoko kwenye jengo hili.
Pale kwenye tovuti ya Anothr kuna habari zaidi toka kwa wanablogu waliohudhuria mkutano huu.
Mon 6 Aug 2007
Mahaba ya Enzi Hizo: Dada Jeni na Michael Wake
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: hapa na paleToa Maoni [6]
Stela kule Himo atakuwa anapiga chafya sana siku hizi kwa kutajwatajwa. Dada Jeni alituuliza hivi karibu, “Mbona Stela tu? Je Michael?” Basi akaahidi kutusimulia ukifika wakati wake. Hapo chini ni kisa cha dada Jennifer Mhando na “Michael” wake (kama vile Sankofa na “Stela” wake. Au Simon na nani hii na nani hii…). Msome dada Jeni kwa maneno yake mwenyewe:
Nilikutana na Michael katika tamasha la wanafunzi mkoani morogoro, yeye akiwa ni mwanafunzi wa kidato cha nne seminary mojawapo morogoro nami katika shule ya sekondari hapo morogoro, michael alikuwa kijana mzuri kweli, anajua kuimba vizuri na ni mcheshi. Mimi napenda sana kucheka mara kwa mara. Alipenda kunitania kuwa tutaunganisha sauti zetu na kuunda bendi, mie hoi kwa vicheko. Nami ni mwimbaji mzuri wakati ho sina uhakika na sasa.
(more…)
Sun 5 Aug 2007
Toka niwasilia hapa Taipei na kujikuta kila nikitaka kuuliza kitu mjini inanipasa kuzunguka huku na kule kutafuta mtu anayezungumza kiingereza, nimekuwa nikifikiria sana masuala ya lugha na maendeleo. Katika kufikiria huko nikasoma makala niliyokuwa nimeihifadhi ili niisome baadaye iitwayo Language, Liberation and Development iliyoko pale Pambazuka. Kipande kidogo cha makala hiyo hiki hapa:
Statistics frequently account for the African population of a country by simply considering them as speakers of the former colonial language. Nigeria, with its 470 African languages thus becomes an anglophone country. The two Congos with the 221 languages of the DRC and the 60 languages of Congo Brazzaville become francophone countries.
Sun 5 Aug 2007
Wikimania 2007: “Sharing Economy” + Wikipedia Academy
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: wikipedia , afrika , mikutanoToa Maoni [1]
Wikimania 2007 imemalizika jana. Jana niliandika kuhusu mada ya “The Sharing Economy” ya Joi Ito ambayo imegusa wengi, mimi nikiwa mmojawapo. Rebecca MacKinnon ameandika kifupi kuhusu mada hiyo. Mada hii imenifikirisha sana na itaendelea kunifikirisha na kuniongoza kwa muda mrefu katika mahusiano yangu na vuguvugu la utamaduni huru, programu huria, programu huru, uandishi wa raia, n.k. Rebecca ameandika:
People who work on any of the Wikimedia projects are certainly not motivated by money: Nobody who creates any of the content gets paid a cent. (The funds raised are spent on computer server space, administrative and technical staff needed to keep things running, legal counsel, etc.) The Wikipedians I’ve been hanging out with over the past several days derive happiness and feelings of self-worth and belonging by being active participants in a global community.
Sat 4 Aug 2007
Picha zinaendelea kupigwa kila sekunde. Picha hii hapa niko na Mtaiwan, Joy Tang, anayesema kuwa yeye ni Mwafrika. Watu wakimshangaa anauliza, “Kwani watu wote si tumetokea Afrika?” Joy Tang ni Rais wa Taasisi ya Kijiji Kimoja (oneVillage Foundation) ambayo inajihusisha na masuala ya maendeleo, uchumi, na teknolojia Afrika. Nyingine hii hapa tunaongelea masuala hayo ya teknolojia na maendeleo.
Picha hii hapa sikumbuki nilikuwa ninashangaashangaa nini. Na hii hapa nikisaini “autografu” kutokana na kuwa na nywele ambazo huwa wanaziona tu kwenye picha za Bob “Malya” na pia viatu ambavyo hawajawahi kuviona toka wazaliwe (yaani “makamteria” au “maraiyo”)! Autografu…natania au sitanii? Ajabu ni kuwa huyu bwana hizi picha badala ya kuweka jina langu ameweka jina la Babukadja (Sankofa wa Mwenye Macho).
Bonyeza hapa utazame picha nyingine nyingi toka mkutanoni.
Sat 4 Aug 2007
Wikimania 2007: Joi Ito na “The Sharing Economy” + Waafrika Walipwe Kwenye Wikipedia?
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: wikipedia , mikutanoToa Maoni [1]
Kati ya mada (kwenye mkutano wa Wikimania 2007) ambayo imegusa watu wengi ni ile ya “The Sharing Economy” ambayo imetolewa na Joi Ito, ambaye amezungumzia masuala ya teknolojia na utamaduni huru akitumia falsafa za Kibudha. Amechambua tofauti kati ya furaha na raha akisema kuwa watu wanaoitwa “professionals” huwa wanafanya kazi wakitazama jinsi gani watapata fedha nyingi zaidi, wakati ambapo watu wanaoitwa “amateurs” huwa wanatazama jinsi gani kazi zao zitawapa furaha zaidi (ingawa hawalipwi). Joi Ito ni wale watu ambao ukikutana nao, jinsi wanavyojiweka kama watu wa kawaida, ukiambiwa yeye ni nani unaweza usiamini. Bonyeza hapa usome yeye ni nani na anajihusisha na masuala gani na hii hapa ndio blogu yake.
(more…)
Sat 4 Aug 2007
Wikimania 2007: Fuatilia Mkutano Kwenye Anothr
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: wikipedia , mikutanoToa Maoni [1]
Siku ya pili ya mkutano wa Wikimania 2007 imemalizika. Fuatilia blogu zenye habari kuhusu mkutano huu kwenye tovuti ya Anothr (huduma ya hawa jamaa nimeipenda sana. Itazame) ambayo inadaka kila habari inayoandikwa. Bonyeza hapa. Nimesikitika sana “kalamu” yangu (tarakilishi) imeniangusha. Sasa tunaelekea kwenye tafrija\ na tamasha la filamu.
Ni furaha kukutana na watu ambao unashirikiana nao kuzalisha maarifa bila kujuana. Basi mnakutana na kuongea kama vile mnafahamiana siku nyingi. Na kwenye tafrija ndio raha zaidi maana unajua tena watu wakishamimina maji kidogo…
Swali kubwa ninaloulizwa, “Waafrika wako wapi? Mbona hawajihusishi na Wikipedia?” Jamaa mwingine akaniambia, “Wikipedia is going to define human knowledge, if you people don’t participate in the process of creating knowledge for humanity…I don’t know.” Akakomea hapo. Akaacha tujaze wenyewe. Yaani mkutano mzima “nyani” niko mwenyewe! (nimejitukana? kwani binadamu si tumetokea kwa nyani au shule tulidanganywa?).



