Mapumziko yalishaisha ila sikuwa na muda wa kuandika hapa. Bado niko Afrika yetu. Jua la Afrika. Chakula cha Afrika. Hewa ya Afrika. Marashi ya Afrika. Akina dada na kaka wa Afrika. Afrika yetu, Afrika. Mutabaruka ana shairi lake moja anasema “it’s no good to stay in a whiteman country too long.” Ikifika jioni natazama jua linashuka katika anga ya Afrika. Asubuhi jua linachomoza, nalitazama toka dirishani nikiwa nimejilaza kivivuvivu. Naelewa Mutabaruka alikuwa anasema nini. Tuache hayo. Kuna tangazo ambalo nimeona siwezi kuacha kuliweka hapa. Tangazo hili huenda utakuwa umeshaliona. Tafadhali piga kura ili kuiwezesha filamu ya Tanzania kupata tuzo.
(more…)