December 2007
Monthly Archive
Mon 31 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
zanaToa Maoni [3]
Kuna teknolojia nyingine unazisikia na kuona kama sio kweli. Hii ni mojawapo. Fikiria: magazeti ya kuuzwa mtaani, kutokana na teknolojia iliyopo, huwa yanakuwa yanafanana. Ina maana kuwa gazeti la Majira au Mwananchi linapochapwa wanunuzi wote watasoma habari hizo hizo. Mnunuzi anayependa zaidi habari za michezo na mwingine anayependa habari za kimataifa wananunua gazeti moja ingawa mapenzi yao ya habari yanatofautiana. Sasa juzi nakuta habari kuwa ipo teknolojia inayowawezesha watoa magazeti kutoa magazeti kuendana na mapenzi ya wasomaji. Sio wote tulazimishwe kusoma habari ambazo moja wakati tuna mapenzi tofauti ya habari. Soma mwenyewe:
A newspaper industry that can better match its content to each individual [print] reader’s unique mix interests will have a more valuable product than today’s ’same-to-all’ editions. Unknown to almost all newspaper people who work with new media (and unknown even to the most newspaper people who work with print), it is now not only possible but economically practical for many newspapers, and soon most, to print a unique edition for each reader. The requirement is that most of today’s newspapers will need to buy new presses.
(more…)
Mon 31 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
hapa na pale ,
safariToa Maoni [6]
Baada ya kujikuta nakuwa kondakta bila kujijua ndani ya basi linalokwenda kitongoji cha Alekzanda pale Jozi (Joburg), safari hii, nilijiambia, nitakuwa makini hapa Dakar. Unajua siku moja niliamka, nikasema hebu ngoja niingie vitongojini. Jiji la Joburg silipendi sana kiasi ambacho huwa nashinda, asubuhi, mchana, jioni, katika mtaa wa Rosebank. Pale ndipo zilipo ofisi za Mail & Guardian ambapo kuna marafiki zangu wanaowasha mwenge wa taaluma ya uandishi wa habari na webu 2.0 barani Afrika. Pia ziko ofisi za iCommons. Pia ndipo zilipo studio za Y FM ambapo rafiki yangu Senzo anafanya kazi kama mtangazaji.
Senzo ni kile kizazi cha vijana wa Afrika Kusini ambao bado wanaamini kuwa siasa za mrengo wa kushoto ndio sahihi kwa Afrika Kusini na wanaamini kuwa Jacob Zuma, mzee wa Umshin Wam (Give me my machine gun….wimbo wa Kizulu ambao amekuwa akiuimba kwenye mikutano ya hadhara) ni jibu muafaka la matatizo ya Afrika Kusini. Humwelezi kitu juu ya Zuma. Tulibishana karibu masaa matano juu ya Zuma na siasa za Afrika. Tukabishana hadi midomo ikakataa kuongea. Akasema, “Twende nyumbani tukale kisha tukatulize kichwa. Nitakupeleka kwenye klabu nzuri sana ya Rege.”
(more…)
Sun 30 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
msetoToa Maoni [1]
“Unajua,” jamaa ananiambia, “tatizo la hiki kitu mnaita “citizen journalism” ni kuwa hawa watu mnawapa cheo cha taaluma ambayo huwa inapatikana kwa kuisomea.”
Namuuliza, “Mwandishi wa habari wa kwanza alisomea wapi? Mwalimu wa kwanza wa uandishi wa habari alifundishwa uandishi na nani?”
===
Sijaelewa kwanini Wasenegali (ambao nimewaona) wanaoendesha magari ya kuvutwa na farasi hawapakii hao farasi. Nimeona farasi wengi na nimepakia mara moja mkokoteni wa kuvutwa na farasi lakini sijaona mtu amempanda farasi. Hata kama mkokoteni utakuwa umejaa mizigo, wataketi juu ya huo mzigo sio juu ya farasi.
Kwenye hotuba za Ali Mazrui, ambazo zimekusanywa kwenye kitabu cha The African Condition (mwenye kitabu changu hiki anajijua, utanirudishia lini? Usifikiri nimesahau!) kuna mahali Mazrui anasema kuwa ukilitazama bara la Afrika ni sawa na kujiangalia kwenye kioo. Niliwahi kuzungumzia hili huko nyuma. Narudia tena maana kuna ukweli fulani kuhusu kauli yake hiyo. Anasema ukijiangalia kwenye kioo, mkono wa kushoto unakuwa wa kulia na wa kulia unakuwa wa kushoto.
(more…)
Thu 20 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
safariToa Maoni [9]
Je unafahamu kuwa niliingia Senegal bila pasipoti? Usimwambie mtu. Haya, sio kuwa sikuja na pasipoti. Nilikuja nayo ila nikaiacha uhamiaji uwanja wa ndege nikaingia zangu mjini. Kila niliyemwambia aliacha mdomo wazi, “Umeacha pasipoti yako uwanja wa ndege?”
“Ndio.”
“Jina la uliyemwachia unalijua?”
“Hapana, ila najua sura yake.”
“Utaichuikua lini?”
“Siku nikiondoka.”
“Sasa hotelini si lazima uonyeshe pasipoti?”
“Nina pasipoti nyingine!”
Hapo ndio mtu anakuwa haelewi kabisa. Nawe hutaelewa. Kuna wakati fulani huwa nafanya vitu vya kuthubutu baadaye nikikaa na kufikiri najilaumu. Kisa hiki nitakisimulia siku moja. Labda.
Thu 20 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
blogu ,
wanabloguToa Maoni [12]
Kati ya hoja za waandishi na pia watu wengine dhidi ya blogu ni kuwa kuna wanablogu wasiotumia majina yao. Tutaaminije kitu kilichoandikwa na mtu tusiyemjua? Mtu asiyetumia jina lake? Kwanini kama mtu unasema ukweli ujifiche? Nilijadili kirefu wakati wa chai na waandishi wa habari wa Afrika Magharibi hapa Senegal kuhusu suala hili. Mmoja aliongea kwa msisitizo mkubwa kuwa wanablogu wakatazwe kabisa kisheria kuandika bila kujitambulisha.
Nikamuuliza, “Wewe ni mkristo?” Akajibu ndio, yeye ni mkristo. Nikamuuliza, “Unaamini kitabu cha Mhubiri kilichoko kwenye Biblia?” Akasema anakiamini. Nikamuuliza, “Jina la aliyekiandika hicho kitabu unalijua na kama hulijui mbona unaamini yaliyoandikwa?” Akasema, “Sijui jina lake. Hapo naona umenipata. Ngoja nifikirie hoja zangu kwa undani zaidi.” Nikamuuliza swali la mwisho, “Mbona kwenye magazeti yenu huwa mnatupa habari zilizoandikwa na ‘Mwandishi Wetu’? Je unataka tusiziamini habari hizo?” Akasema basi mjadala uishe. Hakuwa amefikiria kwa undani hoja zake dhidi ya wanablogu wasiotumia majina yao.
(more…)
Wed 19 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
mseto ,
bloguToa Maoni [1]
Ni miaka kumi iliyopita Jon Berger alitumia neno “weblog” lililokuja kufupishwa na kuwa “blog” (blogu). Bonyeza hapa usome ushauri anaotoa kwa wanablogu wapya.
Wed 19 Dec 2007
Wakati tukijadili kuhusu uandishi wa raia kwenye warsha na waandishi wa Afrika Magharibi hapa Dakar, Senegal, mmoja wa washiriki alisema kuwa hakuna haja ya kubishana. Jambo muhimu ni kutazama ni jinsi gani mifumo hii miwili ya nyanja ya habari inaweza kusaidiana. Alisema sawa. Hata mimi nakubali kuwa sio suala la kuchagua uandishi wa jadi au uandishi wa raia, kila moja ina nafasi yake kwenye jamii.
Lakini ukweli ni kuwa mabishano yapo na yataendelea. Sasa majuzi hapa mwalimu mmoja wa uandishi, David Hazinski, kazuka na kusema hiki kitu kinachoitwa uandishi wa raia ni hatari sana. Ameandika makala akatoa hoja za hapa na pale. Dan Gilmor, mmoja wa watu wanaosukuma gurudumu hili la uandishi wa raia akamjibu. Ningependa usome makala hizo. Sioni ubaya wowote wa kuwa na mjadala huu. Ni vizuri. Wale tunaoona faida wa uandishi wa raia tutaendelea kuelimisha na kuelimisha, wale wanaopinga, wajitokeze tujadiliane. David katika makala yake anasema:
Supporters of “citizen journalism” argue it provides independent, accurate, reliable information that the traditional media don’t provide. While it has its place, the reality is it really isn’t journalism at all, and it opens up information flow to the strong probability of fraud and abuse. The news industry should find some way to monitor and regulate this new trend.
Dan Gilmor anamjibu:
It is false, of course, that anyone who’s serious about this field argues that it’s entirely accurate or reliable (though it is often independent, and often covers what traditional media can’t or won’t spend time on). In fact, as many of us have been noting for years, accuracy and reliability are key areas for improvement.
(more…)
Wed 19 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
mseto ,
teknolojia ,
safariToa Maoni [3]
Teknolojia mpya za habari na mawasiliano zinarahisisha sana kazi za waandishi. Zinatuwezesha kufanya mambo ambayo huko nyuma tulikuwa hatuwezi kufanya au tulikuwa tunafanya kwa tabu sana. Lakini kuna watu inawawia vigumu sana kuelewa. Tena wengine ni maprofesa wa uandishi. Jana nilikwenda chuo kikuu cha Cheikh Anta Diop. Nikaongea na walimu na wanafunzi wa idara ya sayansi na teknolojia ya mawasiliano. Nikaambiwa na mkuu wa idara kuwa walimu wazee huwa wanafanya kila mbinu ili kuwaondoa walimu vijana maana wanakuja na uelewa wa teknolojia mpya na hivyo kutia kazi wao mashakani. Badala wafurahi na kujifunza toka kwa hawa damu mbichi (ambao huitwa digital natives) wanataka kubaki na elimu yao ya zamani na matumizi ya zana ambazo mahali pake ni majumba ya makumbusho.
(more…)
Sun 16 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
blogu ,
mikutano ,
safariToa Maoni [7]
Wakati naingia mjini toka uwanja wa ndege niliona kitu kimoja kikanikumbusha India. India kule kumejaa ng’ombe barabarani. Hapa nilikuta kondoo wamejazana mjini. Nikauliza kulikoni? Kumbe sikukuu ya Tabaski inakuja. Siku hii lazima kila familia ichinje kondoo. Ni sikukuu ya kukumbuka ile hadithi ya Ibrahimu alivyotaka kumchinja mwanaye kama sadaka. Usipochinja kondoo watu wanakusema. Na watu wengi wasio na uwezo hudiriki hata kuiba ili wapate fedha wa kondoo wa Tabaski. Hapa kwenye warsha fedha zilikuwa kwenye begi la mmoja wa waandaaji zikaibiwa. Nikaambiwa kuwa huenda mtu alikuwa akitafuta fedha za kondoo!
(more…)
Fri 14 Dec 2007
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
mikutano ,
webu 2.0Toa Maoni [8]
Salamu za masiku toka Dakar, Senegal. Niko hapa kushiriki kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Afrika Magharibi kuhusu Webu 2.0 na Uandishi wa Habari. Tembelea ukurasa huu kwa habari zaidi toka kwa waandaaji wa warsha hii. Unaweza pia kutazama hii picha hii nikiwa ninawakaripia waandishi wa habari kuwa nyuma kiteknolojia kisha wanalalamika kuwa wanablogu wanaingilia taaluma yao bila mafunzo.
Wakati nikielekea uwanja wa ndege kuja hapa Dakar niligundua mambo kadhaa. Kwa mfano, nimegundua kuwa Intaneti imekuwa kama madawa ya kulevya kwangu. Nikiwa nje ya mtandao ninakuwa kama mgonjwa. Lakini wakati huo huo nimegundua kuwa siku hizi nachukia sana mjini. Hasa miji mikubwa. Nilipowasili Dakar nikakumbuka kosa moja nililolifanya miaka mingi sana iliyopita. (more…)