April 2008
Monthly Archive
Mon 21 Apr 2008
Mwezi uliopita nilishiriki kwenye mahojiano ya dokumentari kuhusu Wikipedia na dhana ya ukweli pale kwenye chuo kikuu cha Western Cape, Cape Town. Dokumentari yenyewe imetolewa hivi sasa na inapatikana YouTube. Inaitwa The Truth According To Wikipedia. Inajadili mahusiano ya dhana ya ukweli na kamusi elezo ya mtandaoni, Wikipedia ambayo kila mtu anaweza kushiriki kuiandika. Walioiandaa ni Televisheni ya Uholanzi, VPRO Backlight.
Jamaa wa The Next Web wanaandika hivi kuhusu dokumentari hii na majina ya waliohojiwa:
On The Next Web we’ll show the premiere of a documentary that takes a better look at Wikipedia. Backlight plunges into the story behind Wikipedia. Is it a revolution, or pure hype?…Van Veelen managed to get some interesting and authoritative people for his camera. Of course the before mentioned Jimmy Wales, Larry Sanger (the since-fired co-founder of Wikipedia, now head of Wiki spin-off Citizendium), the infamous Andrew Keen (author of The Cult of the Amateur: How Today’s Internet Is Killing Our Culture and Assaulting Our Economy), Phoebe Ayers (a Wikipedian in California), Ndesanjo Macha (Swahili Wikipedia, digital activist), Tim O’Reilly (CEO of O’Reilly Media, the “inventor” of Web 2.0), Charles Leadbeater (philosopher and author of We Think, about crowdsourcing), and Robert McHenry (former editor-in-chief of Encyclopedia Britannica).
Soma hapa.
Bonyeza hapa utazame dokumentari hii.
Sun 20 Apr 2008
Zimbabwe ni nchi ambayo kwa miaka ya karibuni imekuwa ikiweka historia duniani. Ni nchi ya kwanza duniani kuwa na noti ambazo zina tarehe ya mwisho kutumika (expiration date)! Ukiwa na hela zako tarehe ikapita, umeingia hasara. Mfumuko wa bei ni mkubwa zaidi ya nchi ambazo ziko kwenye vita (leo hii Paundi 1 ya Uingereza ni sawa na dola milioni 200 za Zimbabwe). Pia imeweka historia kwa kuwa na uchaguzi ambao matokeo yake hayajatangazwa kwa karibu wiki tatu na huenda, usije ukashangaa, yasitangazwe kabisa! Kutokana na uchafu unaondelea hapo Zim, watu wengi wamekuwa wakifuatilia blogu za Zimbabwe. Katika kufuatilia huko, nimekutana na blogu ya Comrade Fatso. Huyu bwana ninachomsifu ni umahiri wake wa kuandika na kuelezea hali ya nchi hiyo kwa ufundi ule wa waandishi wa riwaya. Zaidi ya kuwa mwanablogu, Comrade Fatso ni mwanamuziki na mshairi. Albamu yake ya House of Hunger. Sikiliza shairi lake la Bread and Roses.
Katika blogu yake anaandika, Bread, Milk and Toilet Paper:
The parallel realities we live in have become the only reality now. The other one is paralysed. So bread is now hustled on street corners for two US dollars. Like an illegal drug. Milk has also joined the list of ‘goods’ that are sold in our parallel economy. Not in the shops but on the streets. And if you’re looking for toliet paper then just drive to the nearest ‘Give Way’ sign, a Zimbabwean ‘Stop’ sign.
In our country survival was criminalised a long time ago. We don’t know what is upside-down or downside-up. Normal means no electricity and a drop of water from the tap. Yet our rulers fill the news with talk of the need for a re-count before Zimbabweans know the-count. Filling the news like cramming empty shop shelves with toilet paper. A disgusting illusion. A lie.
(more…)
Thu 10 Apr 2008
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
tanzania ,
zana ,
webu 2.0 ,
pichaToa Maoni
1186240346
Jiunge na FotoBraza. Lakini FotoBraza ni nini?:
Fotobaraza ni jamii ya wapenda picha na wapenda soga, wazungumzao Kiswahili, waliosambaa ulimwenguni mwote. Jamii inaunganishwa na tovuti ya fotobaraza. Tafadhali jiunge nasi kwa kubofya SIGN UP pale kulia. Kama wewe ni member tayari bofya SING IN.
FotoBraza imetengenezwa kwa kutumia huduma ya Ning ambayo inawezesha watu kutengeneza “facebook” zao! Neno Ning kwa Kichina ni amani. Jina zuri sio?
Ning is the only online service where you can create, customize, and share your own Social Network for free in seconds.
Wed 9 Apr 2008
Lazima ucheke. Vichekesho na kebehi vimekuwa vikitumiwa kwa miaka mingi duniani kama moja ya harakati za kisiasa. Tembelea ukurasa huu wa Mwai Kibaki wa Twitter. Kama hufahamu Twitter, bonyeza hapa usome niliyoandika huko nyuma kuhusu teknolojia hii. Kwenye ukurasa huo, Kibaki anasema:
Hakuna cabinet. Kazi iendelee.
about 2 hours ago from web
Hawa Njaruo wanataka nini? Raila amepata kiti ya waziri mkuu. Wacheni vita. Hapana. Sisi tuko hapa hapa. about 22 hours ago from web
Time to take a nap. This reminds me, I should have a bedroom built at Harambee house. 03:03 PM April 08, 2008 from web
Kama ODM hapana taka ministers, kazi iendelee. 07:54 PM April 07, 2008 from web
Wapi huyu Alfred Mutua? Pumbavu yeye. Anarega rega kama kihii. Tell him to issue another press statement. 04:38 PM April 07, 2008 from web
Umuthi utiri silly games. I am the duly elected president of Kenya. Raila ni mtu bure kabisa. 07:07 AM April 07, 2008 from web
Mon 7 Apr 2008
Kila mwaka huwa kunakuwa na mkutano uitwao Wikimania, ambao unahusu miradi mbalimbali iliyo chini ya Wikimedia Foundation. Mkutano wa kwanza ulifanyika Ujerumani mwaka 2005. Wa pili ulikuwa Cambridge, Marekani mwaka jana. Mwaka jana, Wikimania 2007, ilifanyika kule Taiwan. Mwaka huu Wikimania 2008 itakuwa Alexandria, Misri.
Habari kubwa ni kuwa kuna skolashipu. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi za skolashipu hizo. Ukipata utanikuta nikinywa kahawa pembeni ya piramidi!
Bonyeza hapa usome habari za mikutano ya Wikimania niliyohudhuria.
Sat 5 Apr 2008
Je unafahamu mtu yeyote mwenye lori nchini Zimbabwe?
Vichekesho vya kisiasa vimetawala simu za mkono nchini Zimbabwe kama ilivyotokea Tanzania baada ya waziri mkuu wa zamani kugundulika kuwa alikuwa akituibia. Vichekesho hivi vya kisiasa husambazwa kama virusi.
Anyone know someone with a truck? There’s a guy wanting to move all his stuff from State House to Zvimba. The jokes spread as text messages refer to our aged dictator relocating to his rural home.
Soma hapa.
Halafu inasemekana kuwa kuna kampuni ya Israeli imehusika na wizi wa kura Zimbabwe:
On Friday, March 28th, an online newspaper called “Zimbabwe Online” published an article accusing Cogniview, an Israeli startup company, of helping Robert Mugabe rig the Zimbabwean elections.
Soma hapa.
Tue 1 Apr 2008
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
msetoToa Maoni
Ukiwa na wasaa, shiriki kwenye mkutano wa Kamusi Project utakaofanyika mtandaoni. Bonyeza hapa usome jinsi ya kushiriki. Ni kesho.
Wanasema:
We are pleased to announce that we are about to begin work on PALDO: the Pan-African Living Dictionary Online. PALDO will build on the Kamusi Project architecture to create an interlinked multilingual dictionary for African languages, creating a powerful communications tool that will be useful throughout the African continent.
The first step for PALDO will be to program the database, multilingual tools, and enhanced user interface. This work will begin on April 2 with our partners at Kasahorow (kasahorow.org), at a meeting in Accra, Ghana. This meeting will be simulcast LIVE ONLINE, and the transcript will also be posted on this page (www.kamusiproject.org/paldo)
WE INVITE YOU TO PARTICIPATE IN THE MEETING by logging into the live chat session or commenting on the blog, beginning at 9 a.m. on April 2. The timezone for Accra is GMT.