Nimeibuka. Nimeibukia wapi? Tazama picha hii ambayo nimeipiga muda mfupi uliopita, nje ya ofisi nilipo hivi sasa. Nimekuja hapa kwa ajli gani? Bonyeza hapa (kama Kifaransa kinakupiga chenga, nilipe nitakusaidia kutafsiri!).
Unakumbuka nilipokuja nchi hii mwaka jana nikaacha pasipoti kule uwanja wa ndege? Bonyeza hapa usome kisa hicho na mambo mengine mepesi mepesi kuhusu nchi hii. Hivi safari hii nimekutana na yule ofisa? Na je pasipoti nimeiacha pale?
Nitapiga picha zaidi na kuziweka kwenye ukurasa wangu wa Flickr (bonyeza hapa uende kwenye ukurasa huo).
Ni nchi gani hii?…nimekaribishwa kwenye futari kwenye nyumba tatu tayari!



