May 2009
Monthly Archive
Tue 26 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
blogu ,
lugha ,
global voicesToa Maoni
Mwanablogu wa Kiswahili, Bwaya, ametafsiri makala yake ya kwanza kwenye ukurasa wa Kiswahili wa mradi wa kutafsiri wa Global Voices Lingua. Kichwa cha makala yake hiyo ni: Saudi Arabia: Je, mafua ya nguruwe yatatishia Hija?:
Kila mwaka mamilioni ya Waislamu husafiri kwenda Maka kuhiji, moja ya nguzo tano za Uislamu. Je, msimu wa hija ya mwaka huu utatishiwa na homa ya mafua ya nguruwe? Wanablogu wanayo maoni ya kusema.
Bonyeza hapa usome makala nzima.
Juu ya GV Lingua, bonyeza hapa:
Project Lingua seeks to amplify Global Voices in languages other than English with the help of volunteer translators. It will open lines of communication with non-english speaking bloggers and readers of GV by translating main GV site content into other languages.
Mon 25 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
mseto ,
afrikaToa Maoni
Kupitia ukurasa wa Twitter wa Firoze Manji wa Pambazuka na Fahamu tumepata habari za kifo cha Dk. Tajudeen Abdul-Raheem. Huyu ni Tajudeen wa Justice Africa na Global Pan-African Movement. Dk. Tajudeen anajulikana Tanzania kwa makala zake kwenye gazeti la The Citizen. Amekuwa pia akiandika Pan-African Postcard kwenye tovuti ya Pambazuka.
Tajudeen Abdul Raheem tragically died in car accident this morning in Nairobi. We mourn the loss of this Pan African activist.
Tue 19 May 2009
Kuna kesi kubwa itakayosikilizwa kuanzia kesho nchini Zambia kuhusu ukimwi na ajira. Utaweza kufuatilia kesi hiyo ambayo inaweza kuwa ni kesi ya kwanza Afrika ambayo wanablogu watakuwa wakiripoti moja kwa moja toka mahakamani. Juu ya kesi hiyo na pia kufuatilia ripoti hizo za moja kwa moja toka mahakamani, bonyeza hapa.
Juu ya kesi kwa ufupi (toka kwa Priti Patel anayefanya kazi Southern Africa Litigation Centre iliyoko Johannesburg, Afrika Kusini):
On Wednesday, 20 May, the Livingstone High Court will hear a ground-breaking case determining whether mandatory testing for HIV and discrimination solely on the basis of HIV status is constitutional in Zambia.
The case, Kingaipe and Another v Attorney-General, involves two former Zambian Air Force (ZAF) employees, Stainley Kingaipe and Charles Chookole, who were allegedly subjected to mandatory testing for HIV without their knowledge and dismissed due to their HIV status. The two men are seeking reinstatement and damages for mental and emotional anguish.
Sun 17 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
afrika ,
safari ,
historiaToa Maoni
Amini usiamini, kuna mtandao usiowaya wa Intaneti kwenye piramidi za Misri! Lakini hili sio jambo la ajabu kama ukubwa wa piramidi zenyewe na mawe yaliyotumika kuzijenga na historia yake kwa ujumla. Kumbuka kuwa katika maajabu saba ya dunia (yale ya zamani), piramidi peke ndio zimebaki.
Nimeamini.
Nimeamini kabisa kuwa haya ni maajabu ya dunia. Usifikiri kuwa nilikuwa siamini. Ila kwenye picha sio sawa na kuziona piramidi zenyewe hapa kwa hapa. Waliozijenga (yaani mababu zetu) walikuwa na akili za pekee. Tazama picha hizi. Picha hii ni ya kichochoro cha kuingia ndani ya piramidi ya Cheops. Kichochoro hiki ni kidogo na ukuta wake ni mfupi kiasi ambacho inakubidi uiname ili uweze kuingia.
Sat 16 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
mikutanoToa Maoni
Wale wenye akaunti za “Second Life” wanaweza kushiriki kwenye mjadala ambao tunashiriki kuhusu vyombo vya habari na mafua ya nguruwe (swine flu). Kuhusu mjadala wenyewe:
The American University in Cairo’s Virtual Newsroom will broadcast live to the internet on Saturday, May 16 at 9 am EST. Anyone in the world with broadband access can participate in a live chatstream while the Center for Disease Control briefs journalists and bloggers on swine flu. Special guests include members of Global Voices.
Bonyeza hapa ujue zaidi kuhusu mjadala huu. Mjadala unaendelea ninavyoandika. Washiriki rasmi wako Marekani na Misri.
Kama hujui “Second Life” ni nini, bonyeza hapa na hapa. Halafu unaweza kutembelea tovuti ya jamaa wanaotania hii teknolojia na dhana nzima ya “Second Life.” Wao wanajiita “Get A First Life”!
++ Usisahau niko kwenye Twitter kwenye anuani hii: www.twitter.com/ndesanjo
Sat 16 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
diniToa Maoni
Kuna kazi.
Yuko mtu ametuma maswali 3 kwa Askofu Mkuu wa Walutheri. Najua watu hawa hawajazoea sana kuulizwaulizwa maswali. Mtu unatakiwa uende kanisa, usikilize tu (na kuimba, kusali na kutoa sadaka) kisha uende nyumbani. Basi huyu jamaa (anajijua) katuma maswali hayo hapo chini kwa Askofu Mkuu!
(more…)
Sat 16 May 2009
Tazama video hii tumemaliza kuitazama kuhusu mateso yanayowapata wanablogu nchini Misri. Halafu tazama tovuti hii ya mwanadada (mwanablogu), anayepambana vikali sana na serikali ya kidhalimu ya Mubarak kwa kutumia Intaneti. Tovuti yake inaitwa “Torture in Egypt.”
Sat 16 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
zanaToa Maoni
Nilikuwa najua kuhusu “The Grid” ya Afrika Kusini ila sikujua kuwa ipo pia Tanzania. The Grid ni mtandao wa watumiaji wa simu za kiganjani unaokuwezesha kujua marafiki zako wako wapi (inakuonyesha kwenye ramani) na kuwaonyesha wao wewe ulipo na pia mnaweza kupiga gumzo kutumia mtandao huu na mambo mengine.
(more…)
Fri 15 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
safari ,
pichaToa Maoni
Sijui.
Sijui kwanini mto Nile wasingeuita bahari kabisa kutokana na ukubwa wake! Bonyeza hapa uone sehemu ya mto huo (leo asubuhi). Na chakula cha kienyeji cha Wamisri, Koshary. Picha zaidi bonyeza hapa.
Fri 15 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
afrikaToa Maoni
Kuna picha zimewekwa pale Afrigadget, tembelea uzitazame uone uanasanyansi wa Waafrika. Afrigadget ni kati ya blogu bora Afrika, kwa maoni yangu. Uwe ukiitembelea. Bonyeza uone picha hizo.
Fri 15 May 2009
“Blogging the Future” ni mkutano unaokutanisha wanablogu toka dunia nzima unaofanyika kwenye chuo cha the American University in Cairo (Misri). Chuo hiki kimehamia kwenye jengo jipya ambalo liko kama kilometa 40 toka Cairo ya zamani. Kuna Cairo mpya siku hizi. Unajua Cairo ndio mji mkubwa kuliko yote Afrika na Mashariki ya Kati. Umejazana watu na magari kiasi ambacho wameamua kujenga Cairo mpya ambayo nayo ni kubwa mno. Cairo ina watu kati ya milioni 16 -18!
Tazama picha za chuo hiki hapa na hapa.
Kufuatilia mkutano huu, bonyeza hapa (ukishuka chini kidogo utaona muhtasari wa yanayojadiliwa). Pia unaweza kusoma ukurasa wa Twitter wa Lawrence Pintak, Mkurugenzi wa Kamal Adham Center for Journalism Training and Research (ambao ndio wameandaa mkutano huu). Au hapa. Unaweza kusoma pia toka kurasa za Twitter za wana-Global Voices wanaohudhuria kwa kubonyeza hapa.
Wed 13 May 2009
Uchaguzi mkuu Malawi (lile tambiko danganya toto la kidemokrasi la kila miaka mitano) ni mwezi huu. Bonyeza hapa ufuatilie Twitter ya uchaguzi huo, Malawi Votes2009. Halafu tazama pia tovuti ya AfricanElections/Malawi.
**Kuna wasomaji wa Jikomboe wapo Cairo. Tafadhali acha namba yako au anuani kwenye sehemu ya maoni tupange kukutana kwa chai.
Fri 8 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
filamu ,
afrikaToa Maoni [1]
UN News Center inasema:
The Nigerian film industry has overtaken Hollywood and closed the gap on India, the global leader in the number of movies produced each year, according to a new United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO) report released today.
Bonyeza hapa kusoma habari yote.
Turudi nacho….pengine tunaweza kujiuliza, muhimu ni idadi ya filamu au ubora wa filamu? Sijui wewe, mimi sinema nyingi za Nigeria siwezi kuziangalia hadi mwisho. Sio zote, ila nyingi. Najua watu wengi wanazipenda. Watu tuna mitazamo tofauti.
Fri 8 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
zanaToa Maoni
Hakuna dalili nyingine ya kuwa nyanja ya habari na mawasiliano inabadilika kwa kasi kubwa mno kama mchuano uliotokea hivi karibuni kati ya mcheza sinema, Ashton Kutcher na CNN. Ashton Kutcher aliwaambia CNN washindane kuona nani atakuwa wa kwanza kuwa na wafuasi milioni moja kwenye tovuti ya aina mpya ya kublogu (microblogging), Twitter. Aisee, tuache utani teknolojia hizi za habari na mawasiliano zinabadili dunia kama tulivyokuwa tukiijua.
Ashton Kutcher challenged CNN in a video on the network’s Larry King live programme. He wanted to show CNN how an individual could potentially have an equal voice to a major network.
(more…)
Mon 4 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
teknolojia ,
zanaToa Maoni [1]
Kenya Airways inaelekea wanaelewa ulimwengu wa teknolojia ya mawasiliano unakoelekea. Watazame hapa kwenye Twitter. Kama hufahamu twitter ni nini, bonyeza hapa. Halafu kama wewe ni mwanaharakati au unafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali (kwa jina lingine shirika la ulaji wa fedha za wazungu!), bonyeza hapa usome mwongozo wa matumizi ya Twitter kwenye harakati. Mimi kwenye Twitter utanipata hapa.
Mon 4 May 2009
Ukitembea Afrika utakazama tabia za watu wa nchi mbalimbali utafurahi sana. Waafrika tuna tabia za kufurahisha sana. Msenegali, kwa mfano, kwa jinsi alivyoweka mbele uislamu (ule wa vitendo tu) anaweza akawa anakuibia huku akisema “Mungu mkubwa.” Halafu Msenegali akiwa na hela nyingi, akavaa zile nguo ndefu za Kisenegali, akawa anaamkiwa kwa heshima kubwa kisha akawa na wake wengi…basi! Amemaliza, hata akifa kunakuwa hakuna ubaya.
(more…)
Mon 4 May 2009
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
msetoToa Maoni
Kuna mwanablogu wa Kiswahili atakayehudhuria mkutano wa wanablogu duniani, “Blogging the Future” utakaofanyika kwenye kituo cha The Kamal Adham Center for Journalism Training and Research katika Chuo Kikuu cha Amerika pale Cairo, Misri? Kama yupo acha anuani yako kwenye sehemu ya maoni (anuani yako haitaonekana na watu wengine, iwapo una mashaka!). Hivyo hivyo kwa wale wanaosoma blogu hii ambao wanaishi Cairo.
Mada ya mkutano: Blogging The Future: A “Lessons Learned” summit of international bloggers and online journalists.