Baada ya Google Suggest ya Kiswahili kuanza kazi, Facebook nao wametoa toleo la Kiswahili. Baadhi yetu wanaona Kiswahili lugha ya ovyo, sio kweli. Makampuni ya teknolojia yanatambua kuwa lugha hii ina nguvu kubwa hasa siku za mbeleni. Wako wazungumzaji zaidi ya milioni 100. Hii sio idadi ndogo.
Kuhusu Google Suggest toka Blogu ya Google
Tangu kuzinduliwa kwa Google Suggest Mwezi Agosti, wengi wamefurahia urahisi wa kupata vidokezi vya maneno papo hapo, kabla ya kuendeleza neno lote - iwapo wakitumia lugha ya kiingereza, kifaransa au Amharic.
Na Facebook kwa Kiswahili:
The social-networking website Facebook has launched in Swahili, targeting more than 110m speakers of the language.
Na Ndesanjo Macha, Maudhui:
mseto ,
global voicesToa Maoni
Kuna raha kubwa kuwa na uwezo wa kutumia teknolojia mpya za mawasiliano kwa uhuru bila woga au kizuizi chochote. Ziko nchi ambazo uhuru huu ni ndoto. Ndio maana kukawa na mradi wa Global Voices Advocacy (www.http://advocacy.globalvoicesonline.org/) ambao kazi yake ni kutetea uhuru wa kujieleza mtandaoni bila woga. Wakati tuko sisi tunaoweza kujieleza bila woga mtandaoni, wako wenzetu ambao wakifungua mdomo tu kukosoa wezi wenye vyeo kama rais, waziri mkuu, na wengine, basi jela itawaita. Kwa sababu hii, ninaupenda mradi huu na ninaupigia kura. Kura hii inaweza kusaidia mradi huu kupata dola 3,000 za Kimarekani. Kura yenyewe inapigwa kwa kuandika kuhusu GV Advocacy.
Hata wewe kama unaupenda unaweza kuupigia kura kwa kuandika kwenye blogu yako kama nilivyoandika. Maelezo yenyewe utayapata kwenye anuani hii: http://www.zemanta.com/bloggingforacause/
Zemanta Pays it Forward!
To demonstrate the power of blogging, Zemanta will donate its $3000 in prize money to the charitable causes that our blogging community loves the most.
This blog post is part of Zemanta’s “Blogging For a Cause” campaign to raise awareness and funds for worthy causes that bloggers care about.