Wed 9 Aug 2006
Wakati wa mkutano wa Wikimania, sikuhudhuria mada zote zilizokuwa zikijadiliwa. Zipo mada ambazo zilikuwa zikijadiliwa na watu ambao nimewasikiliza na kuwaona kwenye mikutano mingi. Watu hawa nawajua watakayoyasema. Hivyo nilitumia muda huu kujuana na watu, kujua wanashughulika na miradi gani, na pia nafasi yao katika vuguvugu zima la Wikipedia. Mmoja wa watu niliokutana nao ni Kevin Flaherty. Kevin anaishi Seattle katika jimbo la Washington. Mke wake anatoka nchini Kenya.
Kevin ni makamu wa rais wa kampuni iitwayo Wetpaint. Kampuni hii imetengeneza zana poa sana. Zana hii, Ambato itaanza kupatikana kwa lugha mbalimbali kikiwemo Kiswahili, inawezesha mtu yeyote kutengeneza tovuti bila kujua lugha kama HTML, XHTML au CSS ambazo kawaida huwa zinatumika katika ujenzi wa tovuti. Unapotumia zana hii ili kujenga tovuti yako au blogu unachotakiwa kujua ni jinsi ya kutumia tarakilishi. Unachofanya ni kuchagua na kubonyeza, mara una tovuti yako! Hii ni miradi muhimu sana kwa watu tunaotoka nchi za Kusini. Tembelea tovuti yao ujionee mwenyewe. Bonyeza hapa. Haya ndio mapinduzi ninayoongelea mara kwa mara. Au unabisha?
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1244' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date