Gazeti la The New York Times limeandika habari (ambayo nami nimehojiwa) kuhusu Kamusi Elezo ya Kiswahili. Mwandishi wa habari hii, Noam Cohen alihudhuria mkutano wa Wikimania kule Boston. Nilikuwa nikimtania sana ndugu huyu wakati wa mkutano huo kwakuwa yeye ni myahudi. Sitaki kusema matani yenyewe. Kwa mtani hunitoi na tena usijaribu! Bonyeza hapa usome makala yenyewe. (***NYONGEZA: makala niliyoizungumzia bado iko kwenye tovuti ya gazeti la the New York Times ila hivi sasa ili uisome unapaswa kulipia! Hivyo ninakupa kiungo kingine ambapo utasoma bure. Bonyeza hapa.

Na kwa wale ambao wamekuwa wakiniuliza juu ya picha yangu (ambayo haiko hapa kwenye blogu), utaona picha yangu hapo kwenye gazeti hilo. Ikitokea ukatakiwa kujiandikisha kabla ya kusoma habari hiyo, fanya hivyo maana ni tendo la dakika chache sana.