NYONGEZA: (kabla ya kusoma hii hakikisha umesoma niliyoandika jana kwa kubinya hapa. Hii ni nyongeza ya hiyo ya jana, kwa maneno mengine, “sehemu ya pili”).

(muhimu sana sana usome maoni katika viungo hivyo nilivyokupa hapo chini)

Mjadala bado unaendelea. Kila upande unarusha kete zake. Ningependa usome kwa makini maoni aliyotoa Kenyan Pundit ambayo ni changamoto kwa Waafrika. Anasema:

(tongue firmly in cheek, and wake me up as soon as “true” Africans plan, fund, and organize, the “true” African blogging indab…um..meet-up)

Maana yake, kwa tafsiri yangu ambayo sio ya moja kwa moja, anasema, Waafrika wanaojiita Waafrika halisi (maana Waafrikana, wazungu wa Afrika Kusini wametolewa kwenye kundi hilo la Waafrika na baadhi ya wachangiaji wa mjadala), wanasubiri nini wasiandae mkutano wao? Kwani lazima wakaribishwe?

Haya, kuendeleza mjadala yupo yule mwanablogu ambaye wanablogu wa Kenya hupenda kumuita “baba” wa blogu za Kenya, Mental Acrobatics. Ameingilia mjadala huu kwa staili ya aina yake. Yeye anasema mzozo mkubwa sio kuhusu waalikwa...bonyeza hapa usome. Halafu, Ethan Zuckerman naye ameamua kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu mkutano huu. Bonyeza hapa. Pia Sokari Ekine hajabaki nyuma. Anasema: White Blogging Africa. Msome hapa.