Leo saa kumi jioni kutakuwa na majadiliano kuhusu mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa (au kwa jina jingine: Umoja wa Marekani na wenzake wachache). Mahojiano hayo yataendeshwa na mhariri wa masuala ya siasa wa shirika la habari la Uingereza, Reuters, Paul Holmes. Holmes atakuwa akimhoji Ted Turner, mwanzilishi wa shirika kubwa la uongo duniani la CNN. Karibu miaka kumi iliyopita Ted Turner alitoa dola bilioni moja kwa ajili ya kusaidia Umoja wa Mataifa. Mahojiano hayo, au tuseme mazungumzo hayo yatahusu miaka kumi baada ya mchango wake huo (hakuna mtu binafsi ambaye amewahi kutoa fedha nyingi kiasi hiki kwa Umoja wa Mataifa) na mambo mengine yanayohusu vyombo vya habari. (bonyeza hapo chini umalize kusoma habari hii).Mradi wa Global Voices, ambao una uhusiano wa karibu na Reuters, utashiriki katika tukio hili. Baadhi ya wanablogu wake, nikiwa mmojawapo, watakuwa wanaandika habari zinazohusiana na Umoja wa Mataifa katika blogu zao na habari hizo zitatokea katika tovuti ya Reuters. Pia tutakuwa tukifuatilia mazungumzo hayo kupitia webukasti na pia IRC. Bonyeza hapa uone tovuti hiyo ya Reuters. Kona ya wanablogu iko chini kabisa. Pia baadhi ya wanablogu wa Global Voices watakuwepo hapo New York wakiwakilisha maswali na hoja za wana jumuiya wa Global Voices. Hata wewe unaweza kushiriki: kwa kutazama kupitia webukasti, IRC, au kutuma maswali ambayo ungependa Ted Turner aulizwe. Bonyeza hapa uone ushiriki wa Global Voices na jinsi wewe unavyoweza kushiriki. Bonyeza hapa kama unapenda kutuma maswali yako.

Katika blogu ya Global Voices habari ya tukio hili ina swali: Je watatusikiliza? Mimi nasema ndio. Watatusikiliza kama walivyotusikiza kuhusu Rwanda na sasa Darfur!

Kila mara suala la mageuzi ya muundo wa Umoja wa Mataifa linaponijia kwenye anga zangu, huwa sisiti kuimba wimbo alioutunga mwanamuziki Fela Kuti mara tu baada ya kutoka gerezani mwaka 1989 baada ya kufungwa kwa kuwa na mdomo mkubwa. Wimbo huu unaitwa Beasts of No Nation. Ninausikiliza dakika hii ninavyoandika sentensi hizi. Fela…acha tu.
Mara baada ya kutoka jela, Fela anasimulia, watu wengi walikuwa wakimtaka aimbe kuhusu maisha ya jela. Hakutaka kuimba kuhusu jela. Alitaka kuimba kuhusu maisha nje ya jela ambako anasema, “kuna wanyama wanaoongea kama binadamu!” Ni kama Tanzania jinsi ambavyo tuna wanyama ambao wamevaa ngozi za binadamu na suti na kila baada ya miaka mitano huja kutuomba kula (yaani kura).

Katika wimbo huu, pamoja na mambo mengine, amezungumzia suala la Umoja wa Mataifa. Umoja huu anauita, “Dis-United United Nations,” jina ambalo ninakubaliana nalo kabisa. Sasa nitakupa mistari michache ya wimbo huu. Nimeandika kwa kiingereza tofauti na kile alichotumia. Yeye alikuwa akitumia kiingereza kinachozungumzwa mtaani Nigeria.

Many leaders as you see them are in disguise
Animals in human skin
Animal puts on a tie
Animal wears agbada
Animal puts on a suit

These leaders in disguise
They hold meetings everywhere, they reach America
They call the place the United Nations
Hear oh another animal talk

What is united inside United Nations?
Who and who is united for United Nations?
There is no unity between Thatcher and Argentina
There is no unity between Reagan and Libya
Israel versus Lebanon
Iran versus Iraq
East West block versus West block East
Dis-United United Nations
One veto vote isequal to 92 (Or more)
What kind of sense is that, it is animal sense!

Haya, tafakari maneno yake hayo na fuatilia mazungumzo na Ted Turner kwa kufuata maelezo haya hapa.