Hivi ulidhani kuwa Maggid Mjengwa hataki kublogu? Hebu acha utani…bonyeza hapa. Karibu sana Maggid!

——

Huko nyuma niliandika kuhusu mahojiano yaliyofanywa na shirika la habari la Uingereza, Reuters na yule jamaa aliyetoa mamilioni mengi kwa ajili ya “Dis-United United Nations” (yaani Umoja wa Mataifa), Ted Turner. Bonyeza hapa usome niliyoandika kuhusu tukio hilo, kisha bonyeza hapa usome aliyoandika Rebecca MacKinnon kuhusu mahojiano hayo.