Ni kweli kuwa ndugu yetu Acolyte ameondoa ile habari aliyoandika akimtukana Rais wa Tanzania. Sielewi kwanini ameiondoa kama anaamini kwenye yote aliyoandika. Sasa ameandika kuhusu jambo hili akiuliza kwanini nimemzungumzia yeye peke yake wakati Wakenya wengi walizungumzia hilo jambo. Amesema pia kama kuna mtu aliyekerwa na aliyoyasema, basi mtu huyo angemwandikia waraka pepe akimtaka aondoe hiyo habari. Yaani yeye habari ameiweka kwenye blogu kila mtu asome, lakini sisi tumwandikie waraka pepe binafsi badala ya kutumia chombo kile kile alichotumia yeye, yaani blogu. Kwanini?

Kwahiyo nilichotakiwa kufanya ndugu zangu ni kumwandikia barua pepe kimyakimya ili atoe habari hiyo kimyakimya. Kwanini?
Halafu anasema kuwa jambo lenyewe alishasahau anashangaa kwanini nimengoja zimepita siku nyingi nikalizua. Kama amesahau hakuna ubaya. Tutamkumbusha. Suala sio muda, suala ni mada aliyozungumzia. Hata kama angekuwa amendika haya mambo mwaka juzi, mimi nikayasoma mwaka kesho, bado ningemjibu.

Anaandika:

I do admit that my post was a bit too strongly worded, but it was an off the cuff rant which many bloggers understood and did not take too seriously.

Hao wanablogu ambao walisoma habari hiyo na wakachukulia kuwa ni mzaha sio kipimo cha wanablogu wote. Haki yangu ya kuchangia katika mjadala alioanzisha yeye haitegemei eti wanablogu wangapi wamechukulia suala hili kuwa zito au la. Hata kama wanablogu wote duniani wangeelewa na kuona kuwa suala hili ni la mzaha (kama anavyosema yeye), mimi bado ningelivalia njuga kwakuwa mimi sio hao aliowaita “many bloggers” (takwimu hizo sijui amezipata wapi).

Wakati naandaa sehemu ya pili ya suala hili, soma aliyoandika kwa kubonyeza hapa. Mwanzoni anazungumzia masuala mengine kisha chini kidogo utakuta suala hili la Kikwete (Kiwete, kama yeye anavyomwita) kuwa “dumb bitch.” Nimeweka maoni yangu hapo kufafanua kidogo mambo mawili matatu, ila nitaongelea kwa undani katika sehemu ya pili. Bonyeza hapa usome maoni yangu. Na kama huelewi nazungumzia nini, yaani ukiwa hujasoma sehemu ya kwanza ya habari iitwayo “Kikwete kuwa dumb bitch na Watanzania kuwa maimuna,” basi bonyeza hapa ili upate picha halisi.