Sun 8 Oct 2006
Habari ya Acolyte katika gazeti la Mwananchi Tanzania
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: siasa , wanablogu , lugha , tanzania , kenyaMuda mfupi ujao nitapandisha sehemu ya pili ya mada iliyotokana na aliyoandika mwanablogu wa Kenya, Acolyte. Sehemu ya kwanza kama hujaisoma, bonyeza hapa. Bonyeza hapa usome sehemu ndogo ya sehemu hiyo ya kwanza. Kwa sasa nilitaka kutaarifu wanaofuatilia suala hili kuwa makala niliyoandika kujibu shutuma za Aco (kama anavyoita na marafiki zake) haiko tu kwenye blogu bali pia kwenye gazeti la Mwananchi la jumapili iliyopita. Niliambiwa eti niache hili suala maana habari hii itatoka magazetini. Imeshatoka tayari! Bonyeza hapa uione. Sehemu hii ya pili niliyoikalia hivi sasa itajibu baadhi ya maswali na hoja alizouliza na anazoendelea kutoa katika blogu mbalimbali na pia kumalizia hoja nilizokuwa nashusha katika sehemu ile ya kwanza. Kwa wale wanaosema kuwa eti mambo yamekwisha napenda kuwaambia kuwa elimu haina mwisho. Makala hizi sio za kushambulia mtu binafsi. Ni makala za kujadili masuala. Ingekuwa ni mashambulio kwa mtu binafsi basi ningekubali kuwa kuna haja ya kuacha, lakini kinachojadiliwa hapa ni masuala.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1285' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date