Sat 28 Oct 2006
Siku za nyuma niliandika kuhusu tabia ya vyombo vya habari na watu wengine kudhani kuwa kazi za wanablogu zinaweza kuchukuliwachukuliwa tu hivihivi kienyejienyeji. Kama ulipitwa na habari hiyo iliyohusu tovuti ya DarHotwire ya Tanzania na blogu ya mapishi ya MiRecipe, bonyeza hapa usome. Sasa wiki hii limetokea tukio jingine linaloonyesha kuwa vyombo vikubwa vya habari na uongo bado havijaamka na kujua nguvu za mapinduzi ya teknolojia ya blogu na hivyo kuwapa wanablogu heshima inayostahili. Gazeti la Kenya la Kenya Times limebeba makala iliyoandikwa na mwandishi wa blogu ya Kikuyumoja’s Realm na kuibandika kwenye gazeti hilo bila kuonyesha utamaduni wa ustaarabu wa vyombo vya habari, yaani kuwasiliana na mwenye blogu hiyo. Wameibeba makala nzima nzima wakaibandika kwenye gazeti hilo. (bonyeza hapo chini umalize kusoma habari hii)
Mwanablogu huyo, ukisoma aliyoandika, haonyeshi kuwa na tatizo la kazi yake kutumiwa. Ila badi ustaarabu utumike. Ustaarabu huu ni moja ya tamaduni zilizozoeleka kwenye nyanja za habari. Bonyeza hapa umsome mwenye anavyosema kuhusu kisa hiki.
Mwaka jana, gazeti la the Daily Nation la Kenya lilitumia kazi ya mwandishi wa blogu ya
Thinker’s Room bila hata kusema kuwa kazi hiyo imetoka wapi hasa. Mwanablogu huyu akawaandikia barua jamaa wa gazeti hilo kupitia mwandishi mahiri, Onyango Obbo. Gazeti hilo likaomba radhi na kuonyesha ukomavu na heshima kwa wanablogu. Barua ya kuomba radhi ya Onyango Obbo nimeipenda sana. Sehemu ya barua hiyo ilisema hivi:
“We are the leaders in standards in this region, and would like to put it on record that we agree with your position that Clay Muganda’s use of material from “Thinker’s Room” without full acknowledgement falls short of basic intellectual rights norms. Our own Editorial Policy policies require full disclosure of sources.”
Bonyeza hapa usome kazi waliyoitumia. Bonyeza hapa usome aliyoandika Thinker’s Room kuhusu kutumiwa kwa kazi yake. Bonyeza hapa usome barua aliyowaandikia. Na hapa utapata majibu yao. Kisa hiki kiliandikwa pia kwenye tovuti ya Global Voices, bonyeza hapa.
Haya. Nimesoma hiyo habari ya Kikuyumoja basi nikaamua niongeze historia kidogo.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1298' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date