Nia kubwa ya makampuni ya kibiashara ni kuzalisha faida. Lakini, je makampuni haya yana wajibu wowote kwa jamii? Dhana inayoelekea kupata nguvu sana siku hizi iitwayo “corporate social responsibility” inaelezea wajibu wa kijamii ambao makampuni yanapaswa kuwa nao. Baada ya mjadala kuhusu Umoja wa Mataifa (mwanamuziki Fela Kuti alikuwa akiuita umoja huu: Dis-United United Nations!) mwezi wa tisa mwaka huu, shirika la habari la Uingereza, Reuters, litaendesha mjadala mwingine leo kuhusu hii dhana ya uwajibikaji wa kijamii kwa makampuni ya kibiashara. (bonyeza hapo chini umalize kusoma habari hii)

Bonyeza hapa usome niliyoandika kuhusu mjadala huo wa mwezi wa tisa. Bonyeza hapa kuhusu mjadala unaofanyika leo ambao unaweza kushiriki kwa kutazama, kusikiliza, au hata kutoa maoni yako. Swali kuu ni: je makampuni ya kibiashara yanawajibika kijamii katika nchi yako? (je yanajali mazingira, je yanashiriki kuondoa umasiki (au kuuongeza), je yanapinga rushwa, n.k.). Bonyeza hapa uende moja kwa moja kwenye ukurasa wa mjadala huo. Mjadala huu utashirikisha “wataalamu” mbalimbali. Na Global Voices itakuwa ikionyesha wasemayo wanablogu kuhusu dhana hii katika tovuti ya mjadala huu.

Kwa wale wanaotaka kujua saa za mkutano huu huko waliko (mkutano ni saa saa kumi na mbili na nusu jioni/ 6:30pm ET kwa saa za Marekani pwani ya mashariki) wanaweza kubonyeza hapa.