Sat 18 Nov 2006
Mkutano wa Wanablogu: nasaha za mwisho mwisho
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , wanablogu , mikutanoUkumbi wa mkutano umeanza kuwa kama ukumbi wa mkutano. Gumzo kabla ya habari linaendelea. Nilitaka kusema mawili matatu. Ningependa sana tutumie muda wetu vyema. Hivyo kila mshiriki ajitahidi kuwa ndani ya mada. Kwa baadhi yetu hili linaweza kuwa jambo gumu. Tujitahidi sana kuwa ndani ya mada.
Tafadhali unapoingia ndani ya mkutano tumia jina lako ili tufahamu wewe ni nani. Inawezekana ukatoa wazo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi. Hivyo tukahitaji kukufuata kujua “nyuma” unayotaka tujenge iwe ni ya mabati au vigae. Kama ni vigae, viwe vya rangi gani? Au tuezeke nyasi? Kwahiyo kuna umuhimu wa kufahamu nani anasema nini.
Iwapo wewe hujulikani kwa wanablogu, basi jitambulishe wakati wa kuingia. Unaweza kusema, “Mimi ni fulani bin fulani. Ni msomaji wa blogu.” Au, “Mimi ni fulani fulani, ninataka kuanza kublogu.” Kitu kama hicho.
Unaposhiriki, jua kuwa kila kitakachosemwa kitahifadhiwa na baadhi ya wanablogu wanaweza kuweka kwenye blogu zao. Iwapo unasema jambo ambalo hungependa lihifadhiwe, na una sababu za msingi, basi sema hivyo.
Naamini kuwa tutaendesha mkutano kwa heshima na busara. Bonyeza hapa kuingia ukumbini.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1311' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date