Sat 2 Dec 2006
Ujenzi wa Jumuiya ya Wanablogu wa Tanzania: Maoni ya Rasta Luihamu
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , wanablogu , tanzaniaBaada ya Simon Kitururu kufungua njia ya mjadala kuhusu aina ya jumuiya ya wanablogu tunayoitaka, Ras Luihamu amepokea kijiti. Katoa mawazo yake. Bonyeza hapa umsome. Inaelekea kutakuwa na mjadala mkali sana hadi siku tutafikia uamuzi wa mwisho. Hili ni jambo zuri. Kuimarika kwa jumuiya tunayotaka kunategemea, pamoja na mambo mengine, mjadala mkali bila kutoana macho.
Hoja. Mawazo. Fikra. Hekima.
Nguzo za demokrasia.
Ukurasa ule wa Wiki uliotumika wakati wa maandalizi ya mkutano wetu bado uko hai. Utaendelea kuwepo na mambo yataendelea kuongezwa. Hata ninavyoandika hivi sasa kuna mambo mapya machache. Bonyeza hapa.
Halafu kuna habari ya mkutano wetu kwa lugha ya wale wajamaa zetu ambayo unaweza kuisoma hapa. Habari hii imeandikwa pia kwa Kichina! Kama unakijua, basi bonyeza hapa uisome.
Kisha bonyeza hapa usome muhtasari wa yaliyojiri kwenye blogu za Kiswahili wa mwezi uliopita aliotuandikia Nambiza (akataja mkutano wetu) kwenye blogu ya Global Voices Online.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1319' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date