Nyongeza: nimekuwa najaribu kuingia kwenye Intaneti kwa zaidi ya saa moja bila mafanikio. Nilisahau kuweka kiungo ambacho kitakusaidia kuweza kushiriki na hata kutuma maswali kwenye mkutano huu. Bonyeza hapa.

Pia unaweza kufuatilia video ya moja kwa moja toka mkutanoni kwa kubonyeza hapa na kufuata maelezo utakayoyakuta hapa.

——-

Mkutano umeanza. Tatizo la mtandao usiwaya wa Intaneti ambalo limekuwa likitusumbua sana toka tufike hapa India bado linaendelea. Tatizo hili ndio limenifanya nikashindwa kuandika toka nifike hapa. Kila ninapofanikiwa kupata mawasiliano ya Intaneti ninachoweza kufanya ni yale mambo machache.

Hapa mkutanoni napo tatizo linaendelea. Lakini ukiacha tatizo hili nina furaha kubwa kuwa mwanablogu wa Kiswahili Egidio Ndabagoye yuko hapa mkutanoni. Amekaa kona ya kulia, viti kadhaa toka nilipokaa mimi. Na ataongea kwa Kiswahili na wana mkutano hapo baadaye. Wanablogu toka nchi mbalimbali wataongea kwa lugha tofauti katika kuonyesha kuwa “global voices” ziko katika lugha mbalimbali. Basi Egidio ataongea kwa Kiswahili.

Pia hapa ndani kuna mwanablogu toka Kenya, Mental Acrobatics na mwanablogu toka Uganda, Ishna.

*Kwakuwa naandika haraka huku nikishiriki kwenye mkutano, naweza kukosea herufi na pia naweza nisiwe na nafasi ya kuweka viungo na mambo kama hayo. Nitasahihisha baadaye.