Wakati tukiendelea na demokrasia-shiriki ya kujenga Jumuiya ya Wanablogu Tanzania, soma habari kuhusu chama cha wanablogu wa Chile, Chilean Bloggers Association. Bonyeza hapa uisome. Bonyeza hapa uone tovuti yao.

Tafadhali shiriki kwenye ujenzi wa jumuiya yetu. Hivi sasa tunajadili muundo wa uongozi. Bonyeza hapa.

Ugandan Bloggers Happy Hour

Wanablogu nchini Uganda walikutana hivi majuzi. Nilidhani Innocent angehudhuria. Vipi Inno? Msome Jackfruity (Fenesi) alivyoandika kuhusu mkutano huo, orodha ya waliohudhuria na picha. Bonyeza hapa. Eti pamoja na mambo mengine wanablogu waliohudhuria kikao hicho walikubaliana kuwa Inktus ni chuma cha pua. Moto wa kuotea mbali. Naye akawajibu kwa kuwapandishia picha yake.

Inktus tulikuwa naye New Delhi mwezi uliopita. Alikuwa ni kati ya wanablogu waliowakilisha Afrika katika mkutano ule. Unaweza kumuona yeye na wanablogu wengine wa Afrika waliokuwepo katika picha ya pamoja aliyotupiga Boris Anthony. Bonyeza hapa utuzazame. Maelezo ya walioko kwenye picha: (toka kulia kwenda kushoto) Daudi Were wa Mental Acrobatics, ndesanjo macha (yaani mimi), Eloi Laban (mshikaji wake Egidio anayesoma India), Egidio Ndabagoye wa Pilikapilika Vyuo Vikuu, na bibiye Inktus mwenyewe (Egidio, naona hapo kwenye picha umemsogeleasogelea hivi…!).

Moto wa kikao cha wanablogu wa Uganda kimemfanya mwanablogu Fenesi kuamua kujitolea kuandaa mashindano ya Uganda Best of Blogs. Bonyeza hapa usome aliyoandika.

Nakubaliana na dhana ya Uganda Best of Blogs ila shughuli kama hii sioni kwanini iendeshwe na mwanablogu binafsi badala ya kuwa ni shughuli ya jumuiya nzima. Shughuli kama hizi ndio huchangia kufanya jumuiya kujiona na kujisikia kuwa ni jumuiya. Ningefurahi sana kama wangejadili suala hili kwenye kikao na kuamua kuendesha hii shughuli kwa pamoja.

———–

Habari hii ni kubwa hapa Marekani. Wanablogu wamepewa viti mahakamani kama waandishi wa vyombo vya habari vya jadi. Hizi ni ishara za kuzidi kukubaliwa kwa teknolojia hii na kazi tunazofanya wanablogu. Bonyeza hapa.

————

Huzuni. Mwanablogu Mangaliso Jere wa Malawi ametutoka kama Kachumbari, mwanakijiji aliyekuwa akiblogu nchini Kenya, alivyotutoka mwaka jana. Ni huzuni. Bonyeza hapa usome habari hii.

————

Mwisho: Fuatilia picha motomoto toka kwenye mkutano wa wakimbiza/wakamata wezi, Jukwaa la Kijamii Duniani, zinazoletwa na Maggid Mjengwa toka Nairobi. Bonyeza hapa.