Tukizungumzia mapinduzi ya zana mpya za habari na mawasiliano, hatuwezi kuacha kuitaja YouTube (Broadcast Yourself). YouTube ndio mapinduzi yenyewe tunayozungumzia. Sitaki kuongelea YouTube bali tovuti mbalimbali za Afrika au zinazohusu Afrika ambazo nimeamua, ingawa zina tofauti kadhaa na YouTube, kuziita YouTube za Afrika. Tunaanza na Jambo Video ya Tanzania. Bonyeza hapa uitazame.

Kisha tunakwenda Kenya tunaikuta Kenyamoto. Bonyeza hapa. Halafu kuna jamaa wanaitwa Sanaga (sijui wako wapi) ambao wana tovuti yenye jina hilo Sanaga na nyingine ambayo imewahi kuitwa YouTube ya Afrika na mmoja wa waandishi wa Global Voices Online katika makala yake hii hapa. Tovuti yao hiyo nyingine inaitwa Mooziko.

Tukirudi Tanzania tunakuta jamaa wa SwahiliRemix na Mahusiano. Kisha Wakenya wengine wana KenyansUnited. Jamaa wa KenyansUnited wanasema:

The site enables Kenyans to watch videos, look at pictures, op-in to a SMS service which allows other Kenyans and businesses to deliver their news more quickly and easily. However, the main goal of the website is to bring Kenyans from all over the world closer and allow them to communicate with ease.

Makossa ni aina ya muziki ambao ukiutaja huna budi kumtaja Manu Dibango. Mwanamuziki Michael Jackson (hivi bado ni mwanamuziki?) alitumia maneno toka kwenye wimbo wa Manu Dibango (Soul Makossa) kwenye wimbo wake wa Wanna Be Startin’ Somethin’: mamase mamasa mamakossa…

Nirudi kwenye mada. Basi kuna jamaa wanaitwa Makossa.tv. Watazame hapa.

Ukija kwenye filamu, tulianza kuwa na Hollywood, kisha ikaja Bollywood (India), halafu Nollywood (Nigeria). Chemi anatuambia kuwa kuna Bongowood pia. Sasa kuna huduma ya kutazama sinema za Afrika hasa za Nigeria kwenye mtandao (kwa malipo) iitwayo iNollywood.
Wakizungumzia jinsi ya kutumia huduma hii wanasema:

Once you’ve set up your user account: Search for movies by entering the title, actor, director or keyword. Or, simply browse by genre. Choose from our vast selection of movie titles featuring Nigerian independent blockbuster films from the convenience of your home. Select your preferred credit card as a means of payment. Please note that all transactions will be processed via Paypal ® and iNollywood ® will NOT retain any of your sensitive financial details on our database. Once your payment has been verified, the movie is delivered as a VCD to you or streamed automatically from our servers to your computer.

Je Africast.tv umewahi kuwasikia? Wanajieleza wenyewe hivi:

Live news, sports, and entertainment brought to you directly from local broadcasters in several African countries. African cup soccer matches with all its excitement as the continent’s favourite sport. Breaking news from the major cities in Africa, the political debates, all brought to you through the eyes of Africans. The most popular television shows, special features and cultural programs. See what Africans see, feel what Africans feel. See and remember Africa as you knew it; see Africa as Africans remember it. Make Africast your home away from home.