Katika mkutano wa Global Voices Online kule New Delhi, India, siku ya pili tulijadili mambo mbalimbali likiwemo suala la uhamasishaji na mafunzo kwa wanablogu wapya/wachanga au wale ambao sio wanablogu ila wanaweza kufaidika na teknolojia hii. Bonyeza hapa usome baadhi ya mambo yaliyojadiliwa siku hiyo. Kutokana na umuhimu wa shughuli ya uhamasishaji, Global Voices Online imetangaza nafasi ya kazi: Outreach Director (Mkurugenzi wa Uhamasishaji).

Tangazo la nafasi hii linasema:

Global Voices is seeking a full-time Outreach Director. The outreach director will coordinate Global Voices’s efforts in promoting blogging, podcasting, videocasting, photoblogging and other forms of citizen media throughout the world. This will include responsibility for managing a grants program that will support innovative outreach efforts with microgrants, compilation of curiculum for blogging outreach and coordination of speaking and teaching engagements for Global Voices bloggers around the world.

Nafasi hii iko wazi kwa raia wa nchi yeyote na haitakuhitaji kuhama toka hapo unapoishi. Ila inahitaji mtu awe na huduma ya Intaneti ya uhakika. Hata kama huna Intaneti nyumbani kwako, malipo ya kazi hii yatakuwezesha kwenda kwenye mgahawa wa Intaneti na kusema, “kompyuta namba mbili nitakuwa naitumia kila siku kuanzia saa tatu hadi saa kumi jioni.” Kisha ukaingiza mkono mfukoni ukawapa malipo ya mwezi mzima! Bonyeza hapa ujue aina ya mtu anayehitajika.

Ukitaka kujua undani wa Global Voices Online, bonyeza hapa.