Thu 22 Mar 2007
Amatomu: “Technorati” ya Afrika Kusini
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , blogu , afrika , zanaAfrika Kusini wanaelewa somo. Somo la Teknohama (teknolojia za habari na mawasiliano). Majuzi tulisikia kuhusu Gargoyle. Sasa gazeti la Mail & Guardian wamekuja na Amatomu. Amatomu ni kama Technorati. “Technorati” ya Afrika Kusini. Technorati imekuwa ikilaumiwa kwakuwa teknolojia yake ina upendeleo fulani kwa wanablogu wa nchi za Magharibi. Soma lawama hizo toka kwa Africa Media, Blacklooks, na mchango wa Grandiose Parlor. Katika mazingira kama haya, ujio wa Amatomu tunaushangilia.
Kuhusu Technorati, wikipedia inasema:
Technorati is an Internet search engine for searching blogs, competing with Google, Yahoo and IceRocket. As of December 2006, Technorati indexes over 55 million weblogs.
Vincent Maher anayefanya kazi Mail & Guardian ameandika kirefu kuhusu Amatomu. Amatomu inakuwezesha kujua yanayozungumzwa katika blogu za Afrika Kusini. Lakini pia unaweza kutafuta blogu zinazozungumzia mada fulani. Kwa mfano, nimetumia Amatomu ili kupata kwa urahisi orodha ya blogu za Afrika Kusini zinazozungumzia Amatomu. Bonyeza hapa uone.
Afrika Kusini wamekuwa wakifuata nyayo za wana teknolojia wa magharibi, hasa Marekani. Utaona kuwa teknolojia/zana/huduma maarufu kama Flickr, YouTube, Digg, n.k. zina wenzake Afrika Kusini. Tazama orodha hii fupi:
Blogger (Magharibi): iBlog (Afrika Kusini
Digg: Muti na Blik (Afrika Kusini)
Craigslist: YouPost (Afrika Kusini)
YouTube: MyVideo (Afrika Kusini)
Flickr: 24.com Albums (Afrika Kusini)
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1424' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date