Sat 24 Mar 2007
Teknolojia Afrika: Pikipiki ya Baiskeli au Baiskeli ya Pikipiki
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: teknolojia , afrikaUnajua kuna watu ambao wanadhani kuwa sisi Waafrika hatuwezi. Utawasikia wakisema, “wazungu achaneni nao.” Kumbe suala sio rangi. Ni mazingira, sera, na kuwezeshwa kwa wanafunzi, wanazuoni, na wananchi kwa ujumla. Blogu ya Afrigadget inasaidia kuondoa hisia potofu kuwa sisi Waafrika hatuwezi. Sio wanasayansi. Sio wabunifu. Sio wavumbuzi. Uwe ukiitembelea blogu hii kupata habari mbalimbali kuhusu wanasayansi wetu ambao hakuna anayewajali. Hata zile wizara zinazoitwa “wizara za sayansi” (na utumbo) hazina hata majina yao. Afrigadget inatupa habari na picha ya baiskeli yenye injini kama pikipiki iliyotengenezwa Mombasa, Kenya.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1428' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date