Tue 10 Apr 2007
Viongozi wa serikali ya Mugabe wanajulikana kwa maneno yao makali kuhusu nchi za Magharibi. Nchi hizo zilipofikia uamuzi wa kuzuia haki za viongozi hao kutembelea nchi za Ulaya na Marekani, Mugabe na wenzake walikuja juu wakasema, “nchi za kibeberu hizo nani anataka kwenda huko?”
Sasa kumbe pamoja na maneno yao makali kuhusu nchi hizo na madai kuwa hali ya kiuchumi Zimbabwe ni safi, watoto wao wako katika nchi hizo za kibeberu! Gazeti la Zimdaily limeanzisha kampeni ya kutaka watoto hao, wanaofikia zaidi ya 300, wafukuzwe toka nchi hizo ili warudi Zimbabwe wakaishi kwa tabu kama wananchi wengine badala ya kutumia kodi zao kujinufaisha.
Zimdaily imeamua kufanya hivi:
We are compiling below names of ZANU PF official’s kids either studying or living in these western countries and we shall continue to do so as we get more.
Wasomaji wa Zimdaily wameandika majina ya watoto hao kwenye sehemu ya maoni kwenye ukurasa huu.
Zimdaily imeweka katika tovuti yake majina, picha, anuani za wanakoishi, anuani za barua pepe, sehemu wanazopenda kutembelea, n.k.
Sijui ninyi mbinu hii mnaionaje. Mwanablogu Zimpundit, ambako ndipo nilipopata habari hii, hajui alalie upande gani kwenye kampeni hii. Bonyeza hapa upate viungo zaidi kwenye habari aliyoiandika.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1445' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date