Iwapo ungependa kufanya kazi bila kwenda kazini…na una sifa za kutosha, basi usisite kutuma maombi yako. Global Voices Online imetangaza nafasi ya kazi ya Co-Managing Editor. Kazi yenyewe ni ya mtandaoni, ndio maana nikasema “kufanya kazi bila kwenda kazini” maana hutakuwa unaamka asubuhi kwenda ofisini. Watuma maombi toka nje ya Ulaya na Marekani wanapewa kipaumbele zaidi. Kazi kwako. Hela utakayolipwa kama unaishi Tanzania itakuwezesha kukodi mgahawa wa Intaneti kwa mwaka mzima! Yaani utaingia pale kwenye mgahawa na kuwaambia wafunge kwani “kuanzia sasa hii itakuwa ni ofisi yangu!” Bonyeza hapa usome tangazo hilo. Kama hufahamu vizuri Global Voices ni nini, bonyeza hapa.