Nimechelewa kufika mkutanoni leo. Niliamka alfajiri na mapema kwenda Moshi. Hivyo nimekosa mengi yaliyozungumzwa asubuhi na mchana. Ila kwakuwa wapo wanablogu wengi wanaohudhuria mkutano huu, nitaweza kujua yaliyoendelea.

Kati ya blogu hizo ni Mwenye Macho.

Jana usiku, mmoja wa wasomaji wa blogu wa muda mrefu, mtengeneza filamu na mpiga picha Sankofa, alifungua blogu yake: Mwenye Macho. Ninavyomfahamu Sankofa na kamera yake, blogu hii itakuwa na sura na mchango wa aina yake. Itembelee blogu ya Mwenye Macho uone picha mbalimbali za matukio ya mkutano wa TEDGlobal 2007.