Mapema leo Kikwete aliongea na wana TEDGlobal 2007. Soma aliyosema toka kwa Ethan Zuckerman (kiingereza) na Sankofa (Kiswahili)

Wakati nafurahia tangazo la Waafrika 100 waliopewa skolashipu watapewa kompyuta mpya za mapajani za bure, nimepata habari nyingine ya kufurahisha. Mkurugenzi wa Google, Larry Brilliant, kaniambia kuwa atafanya kila awezalo ili wanablogu wa Afrika waweze kukutana barani Afrika.

Wafanyabiashara hawana Kiswahili kirefu. Nilipomgusia suala hilo, ameuliza maswali matatu: Watu wangapi wanatakiwa kuhuduria, utafanyika wapi, na gharama yake ni kiasi gani. Uzuri ni kuwa jana wanablogu kadhaa tulikutana kujadili suala hili hivyo nilikuwa na uwezo kiasi fulani wa kujibu maswali hayo.

Wanablogu tumekuwa tunakutana sana, ila tunakutana kwenye mikutano ya watu wengine. Kuna kila sababu ya sisi wanablogu kukutana kwenye mkutano wetu, kujuana, kujadili, kubadilishana mawazo, ushauri, n.k.