Sat 28 Jul 2007
Tuache utani kila mtu lazima ana “Stela” wake. Stela wangu, ambaye nimeambiwa anaishi Himo, Moshi, kisa chake wengi mnakijua. Asiyekijua bonyeza hapa. Sasa kumbe Sankofa naye ana “Stela” wake. Kisa cha “Stela” wake nimekisoma kama nasoma riwaya moja kali mno ya mapenzi na mahaba. Bonyeza hapa ukisome. Halafu kaweka picha za “Stela” wakekwenye flickr. We! Brazili tutaenda wote, Sankofa! Haya, pole. Hebu wengine wenye “Stela” wao watueleze. Eeh, Tunga we vipi? Jeff na Simon hamna “Stela” nyie? Simon we inaelekea “Stela” walikuwa wengiwengi hivi…eeh? Egidio naona unataka kuingia mitini na kisa cha “Stela” wako.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1549' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date