BlogHer (mkutano wa wanablogu wanawake) mwaka huu ni Chicago. Wanablogu wa Afrika tumewakilishwa kwenye mjadala wa “Women Across the World” na Juliana wa blogu ya Afromusing. Mjadala huu umeongozwa na Georgia Popplewell toka Trinidad, ambaye ni Mhariri Mkuu wa Global Voices Online. Mwingine ni Amira Al-Hussaini, ambaye ni Mhariri wa Global Voices wa Mashariki ya Kati na Afrika Magharibi. Bonyeza hapa usome yaliyojadiliwa kwenye mjadala huo. Kisha bonyeza hapa usome aliyoandika Juliana tokea hapo mkutanoni.