Mon 30 Jul 2007
Anuani Mpya ya Blogu Ya Michuzi + Stela Tu? Je Michael?
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: mseto , wanablogu , hapa na paleBaada ya mwanablogu mpiga picha, Issa Michuzi, kukumbwa na kasheshe ya wachazaji (hackers) ambapo wamechukua anuani yake na hivyo akashindwa kuingia ndani ya blogu yake, amefanikiwa kuhamisha blogu yake kwenye anuani mpya. Badala ya neno “issa” kuwa na “s” mbili, sasa kuna “s” moja, yaani: http://isamichuzi.blogspot.com
Bonyeza hapa usome kisa chenyewe na upate kiungo cha mahojiano yake.
—
Halafu unajua wakati sisi tumekazania akina “Stela,” dada Jeni (Jennifer) anasema kuwa nao wanao akina Maiko (Michael)! Kumbe. Da Mija, Serina, Miriam, Shamimu…ninyi akina Michael wenu vipi? Bonyeza hapa umsome dada Jeni akiahidi kutupa kisa cha “Michael” wake.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1553' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date