Wed 2 Jan 2008
Ukitaka kujua jinsi gani nchi zetu zina njia ndefu kufikia demokrasia halisi, soma habari hii inayoeleza kuwa eti Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya alipoulizwa kama Kibaki ameshinda alijibu kuwa hajui. Alisema hivi:
The magnitude of the Electoral Commission chairman’s admission and the further dent on the credibility of the election was captured in his answer when asked if indeed President Kibaki won the elections: “I do not know whether Kibaki won the election”.
Bonyeza hapa usome habari yote. Halafu tazama picha kwenye blogu za akina Joseph (hapa kwake kuna picha za kutisha sana. Kama una “roho ndogo” usiende hapo), Ory (ambaye kulikuwa na habari kuwa blogu yake imefungiwa), Daudi, Thinkers, Afromusing na wengineo. Pia pale Global Voices Online. Ninavyoandika hivi natafuta tiketi, nabisha hodi Kenya. Nataka kukutana na Kibaki nimweleze kitu fulani. Asiponisikia nimzabe kibao.
—-
Mpya: White African ana orodha ya blogu zinazoripoti na kujadilia hali ya kisiasa na kijamii Kenya hivi sasa. Bonyeza hapa.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1605' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date