Global Voices Online imetengeneza ukurasa maalum kuhusu hali ya kisiasa na kijamii nchini Kenya. Bonyeza hapa ili ufuatilia habari na picha toka kwa wanablogu wa Kenya.

Ushahidi ni zana mpya iliyotengenezwa na wanablogu wa Kenya inayotumia teknolojia mpya ya ramani ili kuonyesha maeneo yenye fujo. Kazi wanayoifanya ni nzuri sana na inafaa kuwa somo kwa watu wanaotazama njia mbalimbali za kutumia teknolojia kuripoti masuala ya maafa. Zana hii ni kati ya zana ambazo zimepewa jina la “mashup.

Zungu (White African) ameandika hivi kuhusu tovuti hiyo:

Ushahidi.com is a tool for people who witness acts of violence in Kenya in these post-election times. You can report the incident that you have seen, and it will appear on a map-based view for others to see. Ory and Daudi are working with local Kenyan NGO’s to get information and to verify each incident.

Jamaa wa Pambazuka nao wamefungua “Action Alerts Blog” kuhusu Kenya.