Sat 19 Jan 2008
Kweli, Uhuru Hauna Kikomo + Blogu za Kiswahili GV
Na Ndesanjo Macha, Maudhui: blogu , Wapi tunakwenda? , tanzania , ushenziNi furaha kubwa kuona kuwa Ndimara Tegambwage hajanyoosha mikono hata baada ya lile shambulizi la kinyama kabisa lenye nia ya kunyamazisha watu wanaofichua uozo kwenye viambaza vya utawala wa “sisi twawala” wa Tanzania. Kweli uhuru hauna kikomo, kama inavyosema blogu yake. Ili kumuunga mkono na kuwatia haya majambazi yanayoitwa “waheshimiwa” nchini Tanzania, unaweza kutembelea blogu yake na kuacha ujumbe. Wakati huo huo kuna makala pale Global Voices Online kaandika Tungaraza kuhusu blogu za Kiswahili. Bonyeza hapa.
WordPress database error: [Table 'wp_comments' is marked as crashed and last (automatic?) repair failed]
SELECT * FROM wp_comments WHERE comment_post_ID = '1621' AND comment_approved = '1' ORDER BY comment_date